Sheria ya ndoa ni suluhisho la mimba za utotoni?

papaayenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
765
500
Inashangaza sana kuona watu wanapoteza nguvu na muda wa kuendesha kesi kwa masuala ambayo mizani yake haiowani na tatizo halisi.

Mara nyingi sana watu wenye fikra zilizo huru na migandamizo huwa wakitumia busara kufumbua tatizo kuliko kutumia mihemuko ya giza katka utafutaji wa suluhu juu ya tatizo.

Kipindi hiki limezuka tatizo kubwa sana sana la wasichana kubebeshwa mimba wakiwa mashuleni awe chini ya miaka 18 au zaidi ya miaka 18.

Wala taifa halijawa na janga la wasichana wengi kuolewa chini ya miaka 18, na kama ikitokea ni nadra sana, na sasa shangwe na vigeregere vilionekana mahakamani kwa kile kilishosemekana kuwa tumeshinda.

Sasa sheria ya kuolewa ni umri wa miaka 18, sawa hebu tutulize akili tuone hiyo sheria ndio itakuwa suluhisho la mimba za utotoni zinazopatikana nje ya ndoa na kuharibu ndoto za wasichana wengi?

Aghalabu mtu mwenye afya njema ya akili lazima atajiuliza hivi ni kipi chenye ahueni kati ya binti wa umri wa miaka 15/16 kupata ujauzito akiwa ndani ya ndoa kwa kupenda kwake, au akiwa nje ya ndoa?

Muumba aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo yeye alipanga kipindi maalumu cha kupevuka kwa kila kiumbe.

Anapofikia umri wa kupevuka kutoka katika hali ya utoto na kuingia katika hali ya ukubwa yaani production stage maumbile yake hubadilika awe binadamu, mnyama, mdudu au mti.

Mabadiliko haya huchochea baadhi ya viungo flani kufanya kazi yake. Hapo ndipo utoto huisha na ukubwa huingia. Na yeye Muumba kwa binaadamu akawawekea sheria ya matumizi halali ya viungo hivyo nayo ni ndoa.

Katika ndoa akaweka ridhaa kwa muolewaji na muoaji. Sasa hawa wanaharakati wa umri wa kuolewa wao wangeshinikiza iwepo sheria ya HAKI YA MSICHANA KTOLAZIMISWA NA WAZAZI KUOLEWA AWE NA MWAKA 15 AU 100 ASILAZIMISHWE. Hapo ingeonekana wana jambo la akili wanalotetea.

Haki hii wamepewa watoto wa kike na muumba wao na mara nyingi wazazi huipora haki hii.

Mwisho, taifa linahitaji sana kipindi hiki wanaharakati watakokuja na tiba za mimba za wasichana mashuleni sio umri wa kuolewa msichana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom