Sheria ya Ndoa na talaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Ndoa na talaka

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mkomatembo, Dec 17, 2011.

 1. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Salaam wana jamvi...

  mimi ni mgeni sana humu ndani, nimevutiwa na mambo mengi sana ambayo kwa kiasi fulani yanaelimisha na yanafunua upeo fulani.

  NAomba kuuliza swali ambalo siku zote huwa najiuliza sipati jibu au labda sina ufahamu nalo na wengine huenda wakawa na jibu.

  NAuliza hivi?

  Tunapofunga Ndoa (mimi ni muislamu) tunafungishwa Ndoa na Sheikh na ili Ndoa iwe sahihi kwa misingi ya dini ya kiislamu, lazima kuwe na walii (yaani mtoa idhini ya kuoza) baba na wengine ambao wameelezewa katika sharia' ya Ndoa , na pasipo walii au muozeshaji , muoa na muolewa basi Ndoa ile ni batili. Wakati Ndoa inapofungwa HAKUNA JAJI , WALA MTU YEYOTE KUTOKA SERIKALINI zaidi ya kitabu ambacho baada ya muda hupelekwa kusajiliwa kwenye daftarila uzazi na vifo. na serikali huikubali Ndoa hiyo kinaga ubaga. swali langu linakuja.

  Kama Ndoa hii ilifungwa kwa misingi ya kiislamu, na serikali ikaikubali ni Ndoa, je?

  KWANINI MWANAMME WA KIISLAMU ANAPOMUACHA MWANAMKE WA KIISLAMU KUTOKANA NA NDOA HIYO HIYO AMBAYO ILIFUNGWA KWA MISINGI YA KIISLAMU NA SERIKALI IKAKUBALI NDOA ILE PASINA NA MUWAKILISHI YEYOTE KUTOKA SERIKALINI KUTOKUWEPO INAPOFIKIA KUTOA TALAKA SERIKALI INASEMA HAIITAMBUI TALAKA ILE MPAKA UPATE YA MAHAKAMANI????! Au

  KWANINI MWANAMKE ANAAPOOMBA TALAKA kwa mwanaume anaambiwa aanze kwanza BAKWATA, na anapokwenda BAKWATA na BAKWATA wakajiridhisha kuwa sababu zote za kuivunja Ndoa ile zipo basi wao hutoa maelekezo kwa MAHAKAMA kuivunja NDOA ILE ! hapa mwanamke kupata shida sana , anapoenda mahakamani ! nenda rudi, ... mwanaume anaruhusiwa kuoa hata kama hajamuacha yule mwanamke lakini mwanamke haruhusiwi kuolewa mpaka apate hiyo talaka ya MAHAKAMA!

  Kwa sheria ya Kiislamu, NDOA HAIWEZI KUVUNJWA MPAKA IVUNJWE NA QADHI ! ndio maana BAKWATA kwasabau kuna MUFTI ambae hana cheo cha QADHI hana mamlaka kisharia kuvunja Ndoa ile. !

  Sasa mimi naomba niulize ! kwanini SERIKALI IKUBALI NDOA ILE AMBAYO IMEFUNGWA KIISLAMU BILA WAO KUWEPO? NA AT THE SAME TIME IKATAE TALAKA INAYOTOLEWA NA MUME KISHERIA YA KIISLAMU AMBAYO IMERUHUSU KAMA ILIVORUHU KWENYE NDOA ! je hapa hakuna mapungufu kweli.

  Na hata kama muem atatoa talaka BAKWATA basi huku nje utaambiwa serikali haitambui!

  Jamani sina nia mbaya! nauliza tu napenda kujua, na kama kuna watu wa kurekebisha sheria basi hili na talaka nadhani liwekwe ili kama mtu akipewa talaka serikali ikubali na tusiambiwe kuwa serikali haitambui talaka ya mume mpaka mahakamani!

  Mimi sijui sharia naomba nijuzwe..

  Salaam

   
 2. T

  TULIBAHA Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kaka ndoa ni private institution ambayo the state has got interest in it as it is the one which creates family then clan and finally the state. It is the source of the citizens.....being so it is in the interest of the state to regulate it
   
 3. H

  Hute JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,047
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  waislam wanawake mnapenda kuachwa? haya endeleeni kukaa kwenye hiyo dini ya uonevu.
   
 4. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yaani kwa kuwa ukimzaa mtoto wako serikali inamtambua basi unataka ukimuua serikali itambue mauaji au?
   
 5. U

  Uwilingiyimana Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani, baadhi ya wachangiaji hamjamsaidia mleta hoja. Badala yake mmemshambulia. Hilo linanifanya niamini kuwa baadhi ya waliojitokeza kumsaidia mleta hoja si wanasheria, maana wlichokifanya si sehemu ya utamaduni wa wanasheria...anyway, kama alivyochangia msomi mmoja ha juu, ndugu yangu ni muhimu uelewe kwamba serikali ina maslahi makubwa ktk muunganiko wa mtu mme na mtu mke, maana huko hutokea watoto na mali, na masuala mengine yenye manufaa kwa jamii nzima!
   
 6. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Umenisaidia, unajua ukisoma post nyingi humu jf ni kuwa kuna chuki kubwa juu ya dini! yaani mtu hata kama kile kitu kinamsaidia yeye atapinga mradi tu mtu aloleta mada sio wa dini yake! sijui tunaelelekea wapi! ninachotaka kusaidia kingine nadhani serikali inapaswa kurekebisha sheria zake katika katiba ili hiki kitu kieleweke! wanwake wengine wanateseka kwa mtindo huu.

  mwanamke kama hajaachwa na mume HAWEZI KUOLEWA mpaka apate talaka! kidini ! talaka ni ile inayotolewa na mume au Qadhi! na Talaka ya serikali HAIKUBALIWI kidini! umeona hapa!

  Hii humfanya mwanamke akae akisubiri apewe talaka ili aweze kuolewa tena au aendelee na maisha yake! huku mwanamme yeye ameruhusiw3a kuoa! mwanaume huoa na mwanamke hukaa akisubiria ! mpaka lini? nilikuwa najaribu kuangalia serikali inamsaidia vipi mwanamke kama huyu? lakini unapewa majibu ya ajabu ajabu! sikui kunyonga kumekuja vipi? acheni chuki
   
 7. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Reading btn the lines, swali lake linamaana tofauti na mineno miiingi aliyoandika hapa. Kuna kitu analenga. Think hard, utagundua ni nini anataka kutushirikisha.
   
 8. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu,
  Hata mimi nimeisoma nikaona anaji-mix sana...she's meaning something behind the curtain...

  Ila kama kweli anahitaji msaada basi aweke wazi jamvini tuu.
   
 9. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kabla sijajibu swali lako napenda ufahamu kwanza mambo ya msingi kuhusu talaka km yalivoainishwa ndani ya law of marriage Act,1971.

  Napenda kukufahamisha kuwa serikali inatambua talaka za kiislamu isipokuwa ili talaka itolewe hata kama ni kwa misingi ya dini ya kiislamu lazima hatua kadhaa zifuatwe na hii haijalishi hata kama ni kwa wakristo.(ingawaje wakristo wanaamini wao hakuna talaka ni mke mmoja na mume mmoja mpk kifo-kwao marriage is an indisoluble sacrament and what god has joined no man can put asunder..so kanisa haliwezi kutoa talaka ila technically mnaweza achana.

  1.Kwa mfano,talaka haitolewi mpaka mahakama ijiridhishe kuwa ndoa imevunjika beyond repair yani hairekebishiki..irreparably broken.

  2.ili kujiridhisha kuwa ndoa imevunjika beynd repair sheria inataka kabla hamjaenda mahakamani mpitie kwanza marriage reconciliatory boards-yani mabaraza ya usuluhisi...hapa ndipo unakuta bakwata,makanisa,na ustawi wa jamii na seyrikali za mitaa wanahusika..kwa hiyo siyo kweli kuwa ni nyinyi tu lazima mpitie bakwata hata wakristo lazma wapitie mabaraza.wao wanawasuluhisha na wakishindwa ndio wanawapa hati ya maandishi ambayo itaonesha wameshindwa kuwasuluhisha.
  3.mkitoka hapo mnaenda mahakamani na huko mahakama itaangalia sababu za kutaka talaka kwa mujibu wa sheria section 107(2)mfano zinaa,ukatili nk na pia lazima ijiridhishe pamoja nakuwepo kwa hayo mambo ndoa yenu imeharibika beyond repair.

  4.sasa suala lako la talaka kwa mujibu wa kiislam mahakama inatambua kwa mfano mi si muislamu ila najua kuna talaka ila,khului,nk isipokuwa ili ziwe valid pia bado hizo hatua zinatakiwa zifuatwe.

  Interestingly,hiyo talaka khului mwanamke wa kiislam anaweza kujiredeem yani kurudisha mahari na kujinasua kutoka kwny ndoa (talaka) yeye mwenyewe,(mnaita kujikhului)na kuna kesi ninaifahamu mahakama imetambua talaka hiyo.

  So sio kweli serikali haitambui talaka za kiislamu la hasha bali mnatakiwa kufuata procedure zilizowekwa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971,ambayo ni sura ya 29 ya sheria zetu!
  Ni hayo tu kwa sasa
   
 10. m

  maya empire Member

  #10
  Aug 13, 2017
  Joined: Mar 24, 2017
  Messages: 75
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 25
  Vipi kuhusu wakiristo ingawa umegusia,lakin bado ninashauku kubwa ya kufahamu taraka inavyotolewa Kwa wakristo tokea mwanzo mpaka mwisho Wa process

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
Loading...