Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Kwanza hapo hakukuwa na ndoa. Bali kulikuwa nadhana ya ndoa haijalishi wameishi kwa kipindi cha miaka mitano au zaidi. Kama hawakufunga ndoa na hakukuwa na cheti.

Pili, huwezikufidiwa kusa eti umekaa na MTU kwa muda Fulani na mlikuwa mkiishi kinyumba. Sheria ya Tz ina mpa MTU haki yakupewa sehemu ya mgao kwakile walichotafuta pamoja wakuwa wanaishi pamoja.

Tatu, MTU anaedai fidia lazima adai fidia halisi (actual damages) na si vinginevyo. Yaani fidia inayohesabika.

Kwenye swala hilo huyo mwanamke hana chake anapoteza muda tu.
 
Naomba unifahamishe kama unauelewa na hili.

Nikioa mwanamke kwa ndoa na akanikuta na kampuni yangu ambayo tayari inafanya vizuri, yeye ana ajira yake ya kumuingizia kipato ambacho ni chake binafsi hakihusiki hata kidogo kwenye kuendesha familia, Je nikimpa talaka na yeye atakuwa na haki ya kupewa sehemu ya kampuni yangu kisheria kama mgawanyo Wa Mali?

Swali LA pili ni same scenario sema mwanamke haujamuoa, unaishi nae tu, vipi atapata chochote.
Ifahamike kuwa ndani ya ndoa kila MTU anayohaki ya kumiliki mali zake binafsi. Kuoa au kuolewa hakukuzui ww au mwenzawako kumiliki Mali binafsi.

Hivyo, ikiwa kampuni unamiliki kama maliyako binafsi na si umiliki wa pamoja, basi mke hawezi kuwa nasehemu ya mgao ktk hio kampuni. Sheria ya ndo kifungu cha 58. Kinampa mwanandoa kumiliki mali binafsi.
 
Msaada, Kuna Mwanamke nimefunga nae ndoa tumeishi miaka 4 ya mikiki mikiki sana na hatukujaliwa kupata mtoto, mwisho aliamua mwenyewe kwamba anaondoka nikabembeleza sana lakini ilishindikana na akutaka tusuluishwe na yeyote alikoenda alipatikana kipindi Cha mwanzo kwenye simu baadae simu yake aikupatikana Tena nilijaribu kwenda nyumbani na kumshilikisha mshenga pamoja na Mama yake mzazi lakini akutoa ushirikiano wowote ni miaka miwili Sasa imepita apatikani kwenye simu na ukiongea na ndugu zake wanasema anawatafuta yeye akitaka na akimaliza maongezi namba aipatikani tena.na katika miaka 4 tuliyoishi alinikuta na nyumba na biashara, ushauri Sasa ili Jambo nalifanyaje kisheria maana maisha lazima yaendelee
 
Hapo hakuna namna ziaidi ya kufile petition mahakamani ili mahakama iweze kuvunja ndoa. Kwasababu misingi yote na maana ya ndoa kwamujibu ya sheria imevunjwa.

Hapo ukimaliza maisha yaendelee vzur
 
Chakuongezea, kama swala lako hujalifikisha kwa viongozi wako wa kidini katika dhebu unalo abudu. Basi lifikishe kwanza swala hilo ili nawao waweze kulijua na kama ikiwezekana kulipatia ufumbuzi.

Hii nikutokana na ndoa kuwa ni yakidini na inamisingi ya kiimani pia. Lakini kama makosa au mapungufu yatakuwa hayawezi kurekebishika basi utachua hatua zaidi zakuomba mahakama iivunje ndoa.
 
Msaada, Kuna Mwanamke nimefunga nae ndoa tumeishi miaka 4 ya mikiki mikiki sana na hatukujaliwa kupata mtoto, mwisho aliamua mwenyewe kwamba anaondoka nikabembeleza sana lakini ilishindikana na akutaka tusuluishwe na yeyote alikoenda alipatikana kipindi Cha mwanzo kwenye simu baadae simu yake aikupatikana Tena nilijaribu kwenda nyumbani na kumshilikisha mshenga pamoja na Mama yake mzazi lakini akutoa ushirikiano wowote ni miaka miwili Sasa imepita apatikani kwenye simu na ukiongea na ndugu zake wanasema anawatafuta yeye akitaka na akimaliza maongezi namba aipatikani tena.na katika miaka 4 tuliyoishi alinikuta na nyumba na biashara, ushauri Sasa ili Jambo nalifanyaje kisheria maana maisha lazima yaendelee
Nawashukuru sana Ila bado naitaji msaada zaidi wa kimawazo. Mbarikiwe sana
 
...Hili Mimi naona pia linategemea na maamuzi yako Mkuu.
Mimi lingenitokea hili kazi ingekuwa ni kutoka Taarifa tu kwa Ndugu zake, Ndugu yangu na kabisa tulilofungia ndoa kwamba make wangu ameivunja nyumba kwa Mikono yake Mwenyewe...halafu musings life at ilia tena na ningeendelea na maisha yangu halafu....siku aibuke na kutaka kuleta za kuleta! Ndipo atakajua kwamba alikuwa hajui...!!!
 
Mkuu sana jMali, kwanza Amri ya Talaka haibebi maelekezo mengineyo kama hayajaombwa kimahakama.Pili, mali binafsi huruhusiwa kwa wanandoa.Ni wajibu wako kutunza nyaraka za kuthibitisha kuwa mali fulani ni zako pekee.Kinyume na hapo,itahesabiwa kama ni mali ya ndoa/machumo na itagwanywa inavyopasa.
Mkuu kwa mfano katika maisha ya wanandoa mali kama nyumba zilizojengwa hati zake zipo katika jina moja la mme pekee yake na jina la mke halipo popote kwenye hati hizo nyumba zitahesabika kama ni za mme pekee yake au za wanandoa wote kwa vile zilijengwa kipindi wapo pamoja?
 
Kwenye swala la mgawanyo wa Mali. Kinachoangaliwa ni mchango wa wanandoa katika upatikanaji wa Mali husika. (Economic contribution na domestic contribution) hivyo vitu viwili ndio hutumiwa kama kipimo cha kujua nani kachangia nini katika upatikanaji wa Mali husika. Na si vinginevyo. Sheria ikowazi
 
Pia sheria inaruhusu wanando kumiliki mali binafsi. Kwaio kuoa au kuolewa hakumzui mwanandoa kumiliki maliyake binafsi.

Unaweza kumiliki nyumba au gari nk. Kama vitu vyako binafsi sheria inaruhusu hilo.

Hati za Nyumba zawezakuwa na majina ya MTU mmoja lakini upatikanajiwake ni mchango wa mke na mume. Kitakachoangaliwa ni ushahidi wa namna malihizo zilivyopatikana na mchango wakila MTU. Ikiwa zilipatikana kwa jasho la wote wawili, basi mgao utahusisha jasho lakila mmoja ikiwa ushahidi utakuwa wazi.
 
Kwa hiyo mkuu siyo kwamba mali iliyopatikana kipindi wakiishi pamoja wote wawili watagawana nusu kwa nusu kama wengi wanavyodhani?
 
Japokuwa ni bandiko la muda mrefu lkn sina budi kukupongeza. Asante kwa ufafanuzi.
 
Kwa hiyo mkuu siyo kwamba mali iliyopatikana kipindi wakiishi pamoja wote wawili watagawana nusu kwa nusu kama wengi wanavyodhani?
Mgao unafwata namna kila mwanandoa alivyochangia katika upatikanaji wa Mali husika.

Hayomengine ni maneno tu, na sio sheria. Kwaio mchango wa wanandoa katika kupatikana kwa Mali husika nikigezo kikuu kinachotumika kufanya mgao pale watakapo achanishwa na mahakama.
 
Ikiwa ulikuwa na Mali kabla yakuoa then baada ya kuoa mume au mke akashiriki katika kuiendeleza hio Mali basi hilo nalo litaangaliwa katika sehemu ya mgao pale mtakapoachanushwa.
 
Na je, mke au mme anaweza kumshitaki polisi mwenza wake au mpenzi wa huyo mwenza wake pale anapowabaini kwamba wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi? Na akienda huko polisi shitaka lake litasomekaje?
 
Kwanza ieleweke kuwa polisi haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Madai. Kwaio swala la madai ya ndoa mlalamikaji anapaswa kulipeleka mahakamani moja kwa moja na si polisi.

Kuhusu kumshtaki MTU aliye na mahusiano na mke au mume wamtu sheria haijatamka wazi juu ya mahusiano. Isipokuwa sheria imezungumzia swala la kushiriki ngono (uzinzi) na mke au mume wa mtu (adultery). Kifungu cha 72 cha sheria ya ndoa, na kifungu cha 74 kimetoa muongozo wa adhabu.

Katika kushtaki, mshtakiwa anaweza kuachiwa ikiwa alikuwa hajui kama mtu aliyeshiriki nae uzinzi ni mke au mume wa mtu. Pia adhabu inaweza kutolewa kwakuzingatia sheria za kimila kulingana na jamii husika.
 
Na je, mke au mme anaweza kumshitaki polisi mwenza wake au mpenzi wa huyo mwenza wake pale anapowabaini kwamba wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi? Na akienda huko polisi shitaka lake litasomekaje?
Polisi haihusiki kabisa na maswala ya madai.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom