sheria ya ndoa inasemaje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sheria ya ndoa inasemaje

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by alan, Jul 17, 2012.

 1. a

  alan Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilikuwa na mwanamke naishi naye nimeishi naye kwa zaidi ya miaka minne sikuwahi kufunga naye ndoa wala sikumtolea mahali,nimezaa naye watoto wawili sasa tumehitilafiana naye akabeba kila kitu ndani mwangu akaondoka navyo pamja na watoto na kuhamia kwa mwanamme mwingine.vitu wanavyotumia nivya kwangu je?nina haki ya kwenda kumyangaya vile vitu?naomba msaada wa kisheria kifungu kwa kifungu
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,251
  Likes Received: 2,931
  Trophy Points: 280
  Nenda WLAC au NOLA hapo utapata msaada mzuri wa kisheria japo sijajua uko mkoani au wilayani. Wanasheria watakufafanulia ufanyeje kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971
   
 3. a

  alan Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi niko dar.lakini kuna mtu aliniambia mwanamke ukiishi naye kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mkeo na anahaki ya mali uliyonayo sasa je?nayeye anahaki ya kuchukua mali yangu na kwenda kuitumia na mwanamke mwingine ok ntakwenda huko uliko nielekeza kaka
   
 4. C

  Cartoons Senior Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ukiishi na mke kwa zaid ya miaka miwili bila kufunga ndoa ,kisheria hiyo inahesabka km ndoa.
  Hata km mke anaamua kuondoka bado sheria ya ndoa haimpi fursa ya kubeba kila kitu,labda km alipata kabla ya ndoa au anavimiliki yeye.
  Kumchukua mke wa mtu ni kosa,unaweza kumshitaki na ukaombwa kulipwa fidia.
   
 5. a

  alan Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok ni kifungu gani cha sheria kinacho sema hivyo maana nayasikia sikia tu na wanaosema hivyo hawatoi vifungu vya sheria
   
 6. MFYU

  MFYU JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  160,sheria ya ndoa ya mwaka 1971
   
 7. MFYU

  MFYU JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ikikumbukwe kwamba kifungu hiki kimeekwa kumlinda mwanamke...! Kwake ye inatumika kama ngao kwake katka mgawanyo wa mali na wewe..na sio kumpa nguvu ya kuamua atakavyo! Kuhusu Mgawanyo wa mali.
   
 8. a

  alan Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na kama kinamlinda yeye kama ngao kifungu hicho hakiwezi kumubana yeye kutoka kwa mwanamme na kwenda kuishi na mwanamme mwingine.kwa madai kuw sijafunga naye ndoa wala sijamtolea mahali kwao?
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna matatizo mawili makubwa ambayo pengine uamuzi wake unaweza kuhusisha sheria tofauti. Kwanza hilo la kuchukua mali zako na kuzihamishia kwa mwanaume mwingine limekaa kijinai (naona kama kuna harufu ya wizi/unyang'anyi). Toa taarifa polisi kuwa mali/vitu vyako vimechukuliwa kinyume cha sheria.

  Hilo la yeye, kuondoka kutoka kwako pamoja na watoto wenu na kwenda kuishi na mwanaume ndio pengine sheria ya ndoa itaingia ili kujibu baadhi ya maswali (je kulikuwa na ndoa? Je ndoa hiyo kama ilikuwepio imevunjika/hairekebishiki? Je utaratibu na mustakabali wa watoto unakuwaje?). Na kama ndoa ilikuwepo, kunaweza kuwepo na kesi nyingine (kama utaamua kuifungua) ya madai dhidi ya huyu 'mkeo' na huyo 'mwanaume' mwingine.
   
 10. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,620
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Ukiishi na mwanamke bila kufunga nae ndoa hata kama ni miaka mitano bado sheria inawachukulia kama nyie ni mahawara ila endapo kutakuwa na mgogoro ambao utapelekea wawili hao kuachana ndio sheria inapoingia kuona haki ya kila mtu ni ipi. Sasa hapa ndugu alan anatakiwa awaone wanasheria kwa msaada zaidi wengine sie ni wazee wa kuangalia TV kuhusu elimu ya sheria hatupo nondo sana ila hili la kuhamisha vitu na kwenda kwa mwanaume mwingine nalo ni neno unless kama angekuwa anaishi mwenyewe maana kama kwako amekimbia siku wakikorofishana huko nako itakuaje maana hizo mali ni za hao watoto aliotoka nao kwako na si za yule bwana na watoto watakaozaliwa na yule mwanaume
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  La kwanza kabisa sheria inasema kuwa ukishakaa na mke kwa zaidi ya miaka miwili katika nyumba moja na mkalala kitanda kimoja na jamii iliyowazunguka ikaamini kuwa nyie ni mke na mume, hata kama hamjaoana inasema nyie ni wanandoa hadi hapo itakapothibitika vinginevyo. Hivyo basi hivyo vitu kama mlichuma mkiwa pamoja inabidi mgawane kutokana na kila nguvu ya mtu ilivyotumika katika kuvichuma vitu hivyo. Ili upate ufafanuzi wa mgawanyo nenda kwenye vyombo vya sheria itatoa muongozo zaidi kwani kutakuwa na maswali mengi ambayo mtaulizwa nyie wote wawili ili kuthibitisha hayo ya kuishi pamoja kama mke na mume, nani alikua na kitu gani kabla na baada ya kuishi pamoja, na maswala ya watoto yanakuaje baada ya wawili nyie kutengana. Lakini mwisho ya yote kila mtu atapata stahiki yake. Pole sana
   
 12. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Inakuwaje anakuwa na ujasiri wa kubeba na watoto kwenda ishi nao kwa mume mwingine, na huyo mume mwingine anakuwaje na ujasiri wa kulea watoto wa mtu mwingine? chunga mjomba vinasaba vinasemaje?
   
 13. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  There is a rebutable presumption of marriage! It does not come automatically that one is your wife/husband. Suppose one of you has a subsisting monogamy marriage? Waendee wanasheria, kuna technicalities za marriage law nyingi hapo
   
 14. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Angekuwa yeye ndio kapeleka watoto wakalelewe na mama wa kambo vinasaba vingeuliziwa?
   
 15. a

  alan Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa kwa mfano nimekwenda kupima vinasaba imegundulika wale watoto siyo wa kwangu na nimewalea zaidi ya miaka minne na hadi hivi sasa bado anakuja kuchukua pesa kwa ajiri ya watoto sasa je? watoto wakigundulika siyo wa kwangu je naweza kumshitaki na kwa kosa gani.wanasheria hebu fungukeni hapo
   
Loading...