MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,159
- 5,399
Duka wauzalo statute za kisheria mkoa wa Mbeya tafadhali.
Muelewe lamedius mbwalohi na amekupa mpaka kifungu cha sheriaUkweli ni upi sasa hapo wakuu zinahusika ama la!!
Upo sahihi sana
Sheria ya ndoa nadhani ni mojawapo kati ya sheria zinazohitaji kuwa reviewed, ipo biased sana.
Ukiwa na mali yoyote kabla ya ndoa na ikawa imeandikishwa kwa jina lako, itahesabiwa ni yako, ukioa, kama mkeo hajawahi ijua na hajawahi kujishirikisha kwa namna yoyote ktk mali hiyo itahesabiwa ni yako mkitengana, lakini tu, akijishirikisha vyovyote vile na mali hiyo, itahesabiwa amehusika kuiendeleza na mtagawana 50/50.
Mali zote mlizopata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikwa jina la mume, mtagawana 50/50, lakini tu, ikitokea mmezipata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikishwa kwa jina la mke, itahesabiwa kuwa ulimpa zawadi, na ni "transfer of ownership" na kwakweli hizo hupati hata senti tano.
ANGALIZO; Kuweni makini na mali mnazowaandika wake zenu!!!
rejea kesi ya Bi hawa mohamed na mumewakeKabla ya kuoa ulikuwa na mali zako ulizomiliki kama nyumba, gari na ardhi(shamba). Ukaja kuoa baadae mkazinguana na mwanamke mkatalikiana.
Sasa katika kugawana mali; je, zile mali ulizochuma kabla ya ndoa zitahusika ktk mgawanyo?! Msaada tafadhali wanasheria wasomi
nimejenga nyumba kwenye kiwanja cha mke wangu alichonunua tukiwa kwenye ndoa,je nyumba ni yake au yetu?..akichukulia mkopo bila kunishirikisha na akashindwa kurejesha,wakopeshaji wana haki ya kuiuza?rejea kesi ya Bi hawa mohamed na mumewake