Sheria ya Ndoa inasemaje? Alikimbia na mwanangu (hatukuwa na ndoa)

dj afro fan

Senior Member
Jan 16, 2017
103
74
NAOMBA MSAADA WA KISHERIA

Niliishi na dada mmoja lakini tuliachana na akaondoka na ujauzito wangu wa wiki 2 na kuniambia hata nisikae nikafikiria kuhusu hiyo mimba sababu anaenda kuitoa hawezi kunizalia mimi kinyago mtoto. Kwa kweli kwa mazingira na ugomvi tuliokuwa nao hata mimi niliamini ataenda kutoa mimba hawezi kunizalia mtoto. Tukawa hatuna mawasiliano lakini baadae nikasikia huyu binti ana mimba, nikawa najiuliza ina maana hakutoa au?

Sikuwahi kuonana nae wala kuwasiliana nae mpak baadae nilisikia taarifa kaolewa na amejifungua mtoto. Hapo ndo nilianza harakati za kumtafuta bila mafanikio. Nilikuwa najiuliza huyu binti hii mimba ni yangu kweli yani hajaitoa au amebeba mimba ya mtu mwingine?

Baadae miezi nane baadae nilifanikiwa kupata mawasiliano na huyu binti mtoto akiwa na miezi 9. Huyu binti hakuwa na furaha na mimi baada ya kuona nimepata mawasiliano nae. Alinitukana sana, akaniambia ameolewa nimkome kabisa. Nikamwambia mimi sihitaji tuongee kuhusu mahusiano wala sijakutafta kwa ajili hiyo. Nikamwambia mimi nakutafuta ili nijue habari za mtoto maana uliondok na ujauzito wangu.

Kusema hivyo alinitukana sana na kusema ujauzito haukuwa wangu, nikamuuliza ni ujauzito wa nan akasema wa mumewe anae ishi nae saivi. Nikamuuliza mtoto umejifungua mwezi gani akaniambia amejifungua mwez wa 9, ukifanya hesabu kama ungekuwa ni ujauzito wangu basi hapa ungekuwa umetimia miezi 7 na sio tisa ya kujifungua. Nikaona nifatilie maana nikama simwamini huyu binti.

Kwanza nilianza kuulizia kwa rafiki zake wa karibu alijifungua lini majibu nilio pewa ni tofauti na huyu ex wangu alivo niambia. Rafiki zake walisema amejifungua mwezi wa 11 miezi ambayo hata mimi nilikuwa ndo naitarajia ili kutimia miez 9. Baada ya kuona huyu mwanamke ananiambia uongo ilibid nimtafute mumewe ili tuwekane sawa kama mtoto ni wake mim niwaache waendelee na maisha yao.

Nilifanikiwa kukutana nae tukaongea vizuri tu nikamuuliza kiukweli aliniweka wazi kuwa mtoto sio wake alimuoa huyo binti na mimba yake na yeye ndo alie ilea mpka hapo mtoto alipo fikia. Aliniambia amesha tumia gharama zaid ya mil 2. Nilimwambia kama akinisaidia mimi nitambulike na mtoto ntamlipa hizo gharama zote. Tukawa tumekubaliana hivo, pia tulikubaliana asimwambie mke wake kuwa tumekutana kwa ajili ya mazungumzo.

Lakini mambo hayakuwa kama tulivo kubaliana, maana huyu bwana hajawahi tena wasiliana na mimi, simu zangu hajibu wala mesej hajibu na yeye ndo nilidhani atanisadia mtoto wangu anijue. Kumbe walienda wakaambiana mimi nilishangaa tu napokea tena mesej za matusi kutoka kwa mwanamke kuwa nisiwafatilie.

Mpaka sasa sijui nifanyeje ili nipate haki ya mtoto angalau anijue nimhudumie mwanangu. Sijisikii vizuri akilelewa na mtu mwengine. Nisaidieni nipate nafasi hata niwe namsalimia tu mwanangu pia niwe namhudumia kwa sasa bado ni mdogo sana sihitaji kumchukua. Nimebahatika kuona picha yake anafanana na mimi sana.

Asanten
 
Ulimkosea huyo dada? Kama jibu ndiyo na mtoto unyimwe tu hakuna namna
 
Sijui chochote kuhusu sheria za ndoa, ila mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto wa mwanamke na si mtoto wa mwanaume aliemzalisha
 
Kimsingi mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto wa mama na anahaki zote za kurithishwa mali za mama ila sio za baba... Unless otherwise iwe ni presumption marriage
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom