Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) 21(1,2) na Kamanda Kamuhanda

Hizi sheria kwenye nchi hii ni kwa baadhi ya watu, wengine wako juu yazo.


Hivi sheria inasemaje kuhusu raia mwenye ushahidi kumfungulia mashtaka huyu Kamanda muuaji?

hawa form four failure wataelewa hizo sheria zilizowekwa kwa kizungu? Hii nchi wanasheria sijaona kazi yao zaidi ya kuandika hukumu mbili mahakamani ili kupima nani ana hela wampendelee. Kuna mambo mengi sana ya kisheria wanashindwa kutufafanulia sie tuliokariri biology
 
Mwanakijiji asante sana kwa kutuletea hii sheria. Actually post zako zote zimeenda shule. Thanks a lot!! Hivi hawezi kutokea mtu, au wanasheria wakamshtaki huyu kamanda? Kamanda ndio mshtakiwa namba moja!! Kijana wa watu alidhani anamfurahisha mkubwa wake alipofyatua bunduki yake sasa wanamshtaki peke yake!! This is not fair!! Ila na yeye alikuwa mjinga sana ni kama mtu anakwambia kula kinyesi chako na wewe kweli unakula!!! Wanasheria please jitokezni mumshtaki huyu kamanda. Invyoelekea hatshtakiwa ila atapandishwa cheo. Nyie tusubiri tu.

Hawa Polisi Wanaonunuliwa Magari Makubwa VX V8!! Wengine Hata kuonja darasa Bado na unapewa Kuwa RPC Unategemea alinde Vipi Kazi yake kama sio Kuwanyamazisha Wahandishi na Kutumia "Ndumba" Kujishikizia!!
Kama hatutaepukana na Haya mambo ya Kutoa Vyeo kwa Kujuana Tusitegemee Mambo Makubwa Katika Haya Mauaji yanayoendelea!! Ni sawa unavyosikia Watu wanachuna Ngozi na Hukumu zinatolewa Kali ila watu Hawaachi Kuchuna!! Ndio Vivyo hivyo Hawa polisi wanaolinda Vyeo Vyao kwa upanga.!
 
well said mwanakijiji.
katika tukio la mauaji ya Mwangosi kulikuwa hakuna arrest ya mwandishi
kilichopo ni mauaji ya mwandishi akiwa kazini na sio arrest.
Nguvu iliotumika haihusiani na arrest kwa hivo mauaji yale yanahusika moja kwa moja na murder.
hatukuona sehemu anaresist kukamatwa bali aliomba ulinzi wa kamanda na tukio la kumwokoa mwenzie wa Nipashe
ukiisoma sheria na kifungu tajwa kwa makini utaelewa how to construe it to give a clear meaning.
kwa hivo kosa la kamuhanda halihusiani na kifungu ulichotaja bali murder c/s 196 of the Penal Code
 
Hizi sheria kwenye nchi hii ni kwa baadhi ya watu, wengine wako juu yazo.


Hivi sheria inasemaje kuhusu raia mwenye ushahidi kumfungulia mashtaka huyu Kamanda muuaji?

Kapotolo, hili ulilosema kweli, wataalam watusaidie make watawala hawajali.
 
Sijafahamu PGO itakuwa inasemaje juu ya hili.Hope kwa hiyo PGO ya kikoloni japo inawasaidia kina Kamhanda bado kwa hili ingemng'ang'aniza Kamhanda asote
 
sasa hawa wnaojiita wnaharakati wa haki za binaadamu mbona wako kimya? tgnp, lhrc, tamwa...mko wapi? kumbe mnaweza mkafungua kesi sasa mbona kimya? Bi Heleni Kijo Bisimba wa Lhrc ulisema utawapeleka the hegue, huko ni mbali, anzia hapahapa kwa kumshitaki kamhanda!
 


Kama nilivyosema kwenye uzi mwingine ninaamini Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Michael Kamuhanda anastahili kutiwa pingu na kufikishwa mahakamani akiunganishwa na mtuhumiwa nambari moja wa mauaji ya Daud Mwangosi siku kadhaa zilizopita. Ninaamini - na ushahidi uko upande wangu - Kamanda Kamuhanda alipaswa kusimamishwa kazi mara moja, kushtakiwa katika mahakama ya kijeshi na kuvuliwa vyeo vyake ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa wengine (wale waliompiga Mwangosi wanatakiwa pia wawemo).

Hata hivyo ninaamini kuna sababu kubwa mbili za kwanini kumchelewesha kumchukulia hatua Kamanda Kamuhanda kumetoa nafasi ya kuchezea ushahidi (tampering with evidence), kutishia mashahidi (intimidation of witnesses) na kwa namna yoyote kupindisha mwenendo wa uchunguzi na hivyo kuharibu mchakato wa kupata haki (obstruction of justice). Kwenye nchi ambayo inaheshimu utawala wa sheria kwa vile Kamanda Kamuhanda alikuwa ni shuhuda wa tukio (material witness) hakupaswa kuwa sehemu ya uchunguzi na kwa hakika hakupaswa kuendelea na wadhifa wake wakati uchunguzi wa mauaji yaliyotokea mbele yake na kwa sababu yake unafanyika. Kumwacha aendelee na nafasi yake ni mojawapo ya uvunjaji mkubwa wa haki ambao serikali imeruhusu na wanasiasa wetu wanavumilia.

Sababu za kwanini Kamuhanda asimamishwe kazi na kufunguliwa mashtaka (asili ya mashtaka sitaki kuhisi sana lakini itakuwa ni kati ya matumizi mbaya ya madaraka hadi mauaji) ni hizi zifuatazo.

a. Hakuwa na sababu ya kuvunja shughuli ya Chadema ambayo ilikuwa inafanyika kwa mujibu wa sheria. Kwa wale walioona video ya mazungumzo yaliyotangulia vurumai kati ya Kamuhanda na Waandishi hoja kubwa ilikuwa kama mkutano wa CDM ulikuwa ni "mkutano wa ndani" (internal meeting) au ulikuwa ni mkutano uliokatazwa. Waandishi - hasa marehemu Mwangosi - walisikika wakimpa nafasi nyingi Kamuhanda kubadilisha njia. Kwamba maana ya "internal meeting" siyo sawasawa na "inside meeting". Kwa maana ya kawaida ya lugha ya Kiingereza mkutano unaweza kuwani "internal" bila kuwa "inside".

Kwa kauli yake mwenyewe kamanda Kamuhanda alifanya makusa zaidi pale alipodai kuwa yeye ana haki ya kutafsiri sheria zote na siyo kipengele kimoja. Kwa kweli yeye si mtafsiri wa sheria na kama angekuwa na hekima (na ushahidi unaonesha kuwa hana) alipaswa kuuliza mwanasheria wa serikali au mwanasheria mwingine kama mkutano ule ambao ulikuwa ni "internal meeting" unalindwa na haukuwa sehemu ya mikutano iliyopigwa marufuku.

Kwa kutoa agizo la kuuvunja mkutano ule Kamanda Kamuhanda - japo inaweza kuwa ni katika bona fide - alivunja na kuingilia kati shughuli halali ya chama cha siasa kikifanya mambo yake ya ndani. Hakuwa na mamlaka, wala sababu ya kuingilia mkutano wa ndani na alikuwa na nafasi ya kutosha kuweza kujihakikishia kuwa agizo lake lilikuwa halali. Kinyume na watu wengine ambao wanataka kuwa CDM walipaswa kutii amri ya polisi binafsi naamini hawakutakiwa kutii amri hiyo ya kuwataka waondoke kwa sababu haikuwa amri halali, haikuwahusu na kwa hakika ilitolewa na mtu ambaye alitumia madaraka yake vibaya.

b. Wakati tukio la kuanza kumpiga mwandishi Mwangosi limeanza Kamanda Kamuhanda alikuwa na haki na uwezo wa kuhakikisha haki za raia zinalindwa. Polisi wote wanajifunza sheria hii ambayo nimeweka hapo juu ambayo inaelekeza wazi kuwa polisi wanapomkamata mtu au kumzuia mtu asiwatoroke hawapaswi kutumia nguvu zaidi ya inayohitajika. Yeye kama Kamanda wa POlisi wa Mkoa aliona jinsi nguvu ya jeshi la polisi iliyokuwepo pale na kwa hakika hakukuwa na mtu hata mmoja ambaye alikuwa ni tishio kwa jeshi hilo.

Lakini zaidi ni kuwa walipomkamata Daud Mwangosi hakuwa na kitu kingine chochote cha kutishia polisi zaidi ya kamera na laptop yake. Wingi wa polisi waliomzunguka - picha na video zinashuhudia - unathibitisha pasipo shaka kuwa kama polisi waliamini (kwa sababu yoyote ile) kuwa Mwangosi amefanya kosa na anastahili kuwekwa chini ya ulinzi, polisi walikuwa na uwezo na nguvu ya kuweza kumdhibiti bila kumpiga. Lakini kwa polisi kumkamata, kumpiga na hatimaye kumuua mbele ya Kamanda wa POlisi wa Mkoa inathibitisha tu kuwa kamanda huyu hafai kuongoza hata chipukizi! Alitakiwa avuliwe vyeo vyake na kuwekwa kizuizini mara baada ya mauaji yale ya Songea ambayo nayo yalitokea katika mazingira ya kutatanisha.

Je atafikishwa mahakamani?
Kwa jinsi polisi walivyochukulia hili na zaidi wanasiasa wetu (wa chama tawala) walivyokubali hili ni wazi kuwa Kamuhanda zaidi atakachofanywa ni kuhamishwa na kupelekwa mkoa mwingine (ningependa binafsi aletwe Dar kuchukua nafasi ya Kova). Kumshtaki mtu mkubwa kama huyu ambaye ushahidi dhidi yake ni mkubwa kuliko ule wa Zomba na kesi ya wauza madini utatikisa jeshhi la polisi. Na kwa vile jeshi hili ni la kulindana (IGP Mwema ndiye aliyemwamisha kutoka Ruvuma!) ni wazi kuwa njia pekee ya kuja kumshughulikia ni uongozi wa CDM kuweka rekodi ya watendaji hawa ili watakapoingia madarakani iwe ni watu wa kwanza kushughulikiwa. Ikumbukwe mauaji hayana muda wa kukoma kuchunguzwa.


SWALI LA UCHOCHEZI:

Polisi wamekuwa wakiendesha kampeni ya kuwataka raia watii sheria bila "shurti". Je, ni nani atawafanya polisi wawe wa kwanza kutii sheria bila kushurtishwa? Au wao polisi hawafikirii kuwa wanatakiwa kuwa ni mfano wa kwanza wa kutii sheria bila shurti?

Nakumbuka Zombe baada ya kutekeleza mauaji ya wachimbaji wa madini akiwa kaimu kamanda wa polisi kanda maalum dar, alihamishiwa rukwa baada ya tume ya jaji kipenka kumtia hatiani sheria ilichukua mkondo wake.
Kamuhanda it just a matter of time utapanda kizimbani
 
Juzi nilimuona Juma Duni Haji pale jangwani akisema "NCHI HII KUNA WATU WENYE HAKI YA KUISHI NA WATU WENGINE WANA HAKI YA KUFA "
kwa hali hii Kamuhanda ni ngumu kujiuzulu maana alikuwa anatekeleza amri ''HALALI '' ya bosi wake.
 
Tuwasubirie washitaki maarufu kama C Mtikila kuja kumshitaki huyu bwana Kamuhanda

Vinginevyo huwa nakubali vifungu vya hotuba ya The former South African president , alisema hivi "Bynow every one of us has seen it practically that the Blacks cannot rulethemselves. Give them guns and they will kill each other" P W Botha -August 18, 1985
 
unajua sheria ina ruhusu wawepo... ila sijui ni kwa kiasi gani tumewahi kuwatumia.
sio kwamba tu inaruhusu wawepo, ni kwamba wapo, na private prosecutor wengi tu wamekuwa wakiendesha kesi hapa tz. nilishawahi kukutana na issue kamahizi mara kadhaa mahakamani, ila wanachotakiwa, ni kuwasiliana na ofisi ya mwanasheria mkuu/dpp ili wawe chini ya maelekezo ya ma state attorney.
 
well said mwanakijiji.
katika tukio la mauaji ya Mwangosi kulikuwa hakuna arrest ya mwandishi
kilichopo ni mauaji ya mwandishi akiwa kazini na sio arrest.
Nguvu iliotumika haihusiani na arrest kwa hivo mauaji yale yanahusika moja kwa moja na murder.
hatukuona sehemu anaresist kukamatwa bali aliomba ulinzi wa kamanda na tukio la kumwokoa mwenzie wa Nipashe
ukiisoma sheria na kifungu tajwa kwa makini utaelewa how to construe it to give a clear meaning.
kwa hivo kosa la kamuhanda halihusiani na kifungu ulichotaja bali murder c/s 196 of the Penal Code

Asante sana; na nadhani ya kwako hili ni muhimu zaidi kwa sababu kama hawakuwa wanamkamata au kumzuia asitoroke then kilichotokea kama unavyosema it was a pure criminal act but police thugs under Kamuhanda...
 
well said mwanakijiji.
katika tukio la mauaji ya Mwangosi kulikuwa hakuna arrest ya mwandishi
kilichopo ni mauaji ya mwandishi akiwa kazini na sio arrest.
Nguvu iliotumika haihusiani na arrest kwa hivo mauaji yale yanahusika moja kwa moja na murder.
hatukuona sehemu anaresist kukamatwa bali aliomba ulinzi wa kamanda na tukio la kumwokoa mwenzie wa Nipashe
ukiisoma sheria na kifungu tajwa kwa makini utaelewa how to construe it to give a clear meaning.
kwa hivo kosa la kamuhanda halihusiani na kifungu ulichotaja bali murder c/s 196 of the Penal Code

Asante sana; na nadhani ya kwako hili ni muhimu zaidi kwa sababu kama hawakuwa wanamkamata au kumzuia asitoroke then kilichotokea kama unavyosema it was a pure criminal act but police thugs under Kamuhanda...
 
uko sahih mheshimiwa mwanakijiji ila naomba nam nichangikia kuhusu kamuhanda kuwa mshtakiwa number moja(principal offender), kwa common laws kamuhanda ni accesory na sio mshitakiwa number moja, kwa mtu kuwa mshtakiwa number moja ktk makosa yanayojumuisha watu weng lazima kuwe na utimilifu wa actus reus na mens rea, kwa hiyo mtuhumiwa number moja ni yule askar aliyefikishwa mahakaman ila kwa provision uloleta kamuhanda is also liable as an accesory though ana makosa ya mal-administration, so lile group lote la askar wote kisheria wanahitajika kushtakiwa
 
Back
Top Bottom