Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) 21(1,2) na Kamanda Kamuhanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) 21(1,2) na Kamanda Kamuhanda

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 14, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280


  Kama nilivyosema kwenye uzi mwingine ninaamini Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Michael Kamuhanda anastahili kutiwa pingu na kufikishwa mahakamani akiunganishwa na mtuhumiwa nambari moja wa mauaji ya Daud Mwangosi siku kadhaa zilizopita. Ninaamini - na ushahidi uko upande wangu - Kamanda Kamuhanda alipaswa kusimamishwa kazi mara moja, kushtakiwa katika mahakama ya kijeshi na kuvuliwa vyeo vyake ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa wengine (wale waliompiga Mwangosi wanatakiwa pia wawemo).

  Hata hivyo ninaamini kuna sababu kubwa mbili za kwanini kumchelewesha kumchukulia hatua Kamanda Kamuhanda kumetoa nafasi ya kuchezea ushahidi (tampering with evidence), kutishia mashahidi (intimidation of witnesses) na kwa namna yoyote kupindisha mwenendo wa uchunguzi na hivyo kuharibu mchakato wa kupata haki (obstruction of justice). Kwenye nchi ambayo inaheshimu utawala wa sheria kwa vile Kamanda Kamuhanda alikuwa ni shuhuda wa tukio (material witness) hakupaswa kuwa sehemu ya uchunguzi na kwa hakika hakupaswa kuendelea na wadhifa wake wakati uchunguzi wa mauaji yaliyotokea mbele yake na kwa sababu yake unafanyika. Kumwacha aendelee na nafasi yake ni mojawapo ya uvunjaji mkubwa wa haki ambao serikali imeruhusu na wanasiasa wetu wanavumilia.

  Sababu za kwanini Kamuhanda asimamishwe kazi na kufunguliwa mashtaka (asili ya mashtaka sitaki kuhisi sana lakini itakuwa ni kati ya matumizi mbaya ya madaraka hadi mauaji) ni hizi zifuatazo.

  a. Hakuwa na sababu ya kuvunja shughuli ya Chadema ambayo ilikuwa inafanyika kwa mujibu wa sheria. Kwa wale walioona video ya mazungumzo yaliyotangulia vurumai kati ya Kamuhanda na Waandishi hoja kubwa ilikuwa kama mkutano wa CDM ulikuwa ni "mkutano wa ndani" (internal meeting) au ulikuwa ni mkutano uliokatazwa. Waandishi - hasa marehemu Mwangosi - walisikika wakimpa nafasi nyingi Kamuhanda kubadilisha njia. Kwamba maana ya "internal meeting" siyo sawasawa na "inside meeting". Kwa maana ya kawaida ya lugha ya Kiingereza mkutano unaweza kuwani "internal" bila kuwa "inside".

  Kwa kauli yake mwenyewe kamanda Kamuhanda alifanya makusa zaidi pale alipodai kuwa yeye ana haki ya kutafsiri sheria zote na siyo kipengele kimoja. Kwa kweli yeye si mtafsiri wa sheria na kama angekuwa na hekima (na ushahidi unaonesha kuwa hana) alipaswa kuuliza mwanasheria wa serikali au mwanasheria mwingine kama mkutano ule ambao ulikuwa ni "internal meeting" unalindwa na haukuwa sehemu ya mikutano iliyopigwa marufuku.

  Kwa kutoa agizo la kuuvunja mkutano ule Kamanda Kamuhanda - japo inaweza kuwa ni katika bona fide - alivunja na kuingilia kati shughuli halali ya chama cha siasa kikifanya mambo yake ya ndani. Hakuwa na mamlaka, wala sababu ya kuingilia mkutano wa ndani na alikuwa na nafasi ya kutosha kuweza kujihakikishia kuwa agizo lake lilikuwa halali. Kinyume na watu wengine ambao wanataka kuwa CDM walipaswa kutii amri ya polisi binafsi naamini hawakutakiwa kutii amri hiyo ya kuwataka waondoke kwa sababu haikuwa amri halali, haikuwahusu na kwa hakika ilitolewa na mtu ambaye alitumia madaraka yake vibaya.

  b. Wakati tukio la kuanza kumpiga mwandishi Mwangosi limeanza Kamanda Kamuhanda alikuwa na haki na uwezo wa kuhakikisha haki za raia zinalindwa. Polisi wote wanajifunza sheria hii ambayo nimeweka hapo juu ambayo inaelekeza wazi kuwa polisi wanapomkamata mtu au kumzuia mtu asiwatoroke hawapaswi kutumia nguvu zaidi ya inayohitajika. Yeye kama Kamanda wa POlisi wa Mkoa aliona jinsi nguvu ya jeshi la polisi iliyokuwepo pale na kwa hakika hakukuwa na mtu hata mmoja ambaye alikuwa ni tishio kwa jeshi hilo.

  Lakini zaidi ni kuwa walipomkamata Daud Mwangosi hakuwa na kitu kingine chochote cha kutishia polisi zaidi ya kamera na laptop yake. Wingi wa polisi waliomzunguka - picha na video zinashuhudia - unathibitisha pasipo shaka kuwa kama polisi waliamini (kwa sababu yoyote ile) kuwa Mwangosi amefanya kosa na anastahili kuwekwa chini ya ulinzi, polisi walikuwa na uwezo na nguvu ya kuweza kumdhibiti bila kumpiga. Lakini kwa polisi kumkamata, kumpiga na hatimaye kumuua mbele ya Kamanda wa POlisi wa Mkoa inathibitisha tu kuwa kamanda huyu hafai kuongoza hata chipukizi! Alitakiwa avuliwe vyeo vyake na kuwekwa kizuizini mara baada ya mauaji yale ya Songea ambayo nayo yalitokea katika mazingira ya kutatanisha.

  Je atafikishwa mahakamani?
  Kwa jinsi polisi walivyochukulia hili na zaidi wanasiasa wetu (wa chama tawala) walivyokubali hili ni wazi kuwa Kamuhanda zaidi atakachofanywa ni kuhamishwa na kupelekwa mkoa mwingine (ningependa binafsi aletwe Dar kuchukua nafasi ya Kova). Kumshtaki mtu mkubwa kama huyu ambaye ushahidi dhidi yake ni mkubwa kuliko ule wa Zomba na kesi ya wauza madini utatikisa jeshhi la polisi. Na kwa vile jeshi hili ni la kulindana (IGP Mwema ndiye aliyemwamisha kutoka Ruvuma!) ni wazi kuwa njia pekee ya kuja kumshughulikia ni uongozi wa CDM kuweka rekodi ya watendaji hawa ili watakapoingia madarakani iwe ni watu wa kwanza kushughulikiwa. Ikumbukwe mauaji hayana muda wa kukoma kuchunguzwa.


  SWALI LA UCHOCHEZI:

  Polisi wamekuwa wakiendesha kampeni ya kuwataka raia watii sheria bila "shurti". Je, ni nani atawafanya polisi wawe wa kwanza kutii sheria bila kushurtishwa? Au wao polisi hawafikirii kuwa wanatakiwa kuwa ni mfano wa kwanza wa kutii sheria bila shurti?
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hizi sheria kwenye nchi hii ni kwa baadhi ya watu, wengine wako juu yazo.

  Hivi sheria inasemaje kuhusu raia mwenye ushahidi kumfungulia mashtaka huyu Kamanda muuaji?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,793
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Hivi mnadhani Kamanda Kamuhanda ana raha hapo alipo? Nadhani anatamani kukimbilia mashariki ya mbali ama ardhi ipasuke imumeze! Yeye alikanusha Polisi wake kuhusika kisha anamkamata Polisi wa chini yake kwa kuhusika na mauaji! Kuna watu walisema kabla ya kuuawa Mwangosi aliomba msaada kwa Kamuhanda lakini hakuupata. Moja jumlisha moja ni tatu.

  Kamuhanda hakika yupo kwenye supu ya moto. Jana nimemsikia akiongelea suala la kamati kuibiwa vifaa huko Iringa nikaona tena yamemkuta mzee mwenzangu kila kukicha afadhali ya jana.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280
  Thats to me is greatest indignity of all; Kamuhanda bado anakalia ofisi, bado anaweza kuamuru polisi, bado anapigiwa saluti na kina Nchimbi na Mwema hawaoni tatizo ya hili? Kama waandishi - na uzembe wao - wameshindwa kuandamana au kutaka huyu bwana ang'olewe na kama CDM nao wamekaa na kumlilia Rais amuondoee well wataendelea kupopolewa hadi watakaposema "inatosha"!

  KAMUHANDA ASHTAKIWE!!!
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,793
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Kama una ushahidi peleka kwa DPP ili aruhusu kufungua mashitaka!!! Hakuna private prosecutors kama akina Ken Starr hapa TZ.
   
 6. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,842
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ni upepo tuuu huo utapita kama pepo zingine zilivyo pita naona upepo wa dr Ulimboka saizi umetulia tuliii??
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,793
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Mkuu hakika waandishi wamepoteza fursa muhimu sana hapo ya kuandika japo kahistoria kadogo ambako kangesomwa na wajukuu zetu hapo baadaye kwamba:

  "Hapo zamani za kale paliondokea kuwa na Jeshi la Polisi katika nchi ya Tanzania na Jeshi hilo likawa linahusishwa na mauaji ya raia. Basi siku moja jeshi hilo likahusishwa na mauaji ya mwanahabari mmoja aitwaye Daud Mwangosi. Mauaji hayo yalitokea kwenye kijiji kimoja kijulikanacho kama Nyololo kilichopo barabara ya Iringa kuelekea Mbeya penye makutano ya kuelekea Igowole na mashamba ya chai huko Mufindi. Basi baada ya mauaji hayo, waandishi wote wa habari kwa umoja wao waliandamana na kupiga kelel kwa kutumia kalamu zao ambazo zilikuwa zikitoa wino mwekundu kuashiria damu ya Mwangosi iliyomwagika pale Nyololo. Maandamano yalipamba moto huku wakimtaka Mkuu wa Jeshi hilo mkoa wa Iringa (yalikotokea mauaji) ajiuzulu. Hali ikawa mbaya na shinikizo la waandishi likawa kubwa na mwishowe mkuu huyo akijulikna kama Kamanda Kamuhanda aliitisha kikao na hao waandishi wa habari na kuwatangazia kuwa anachukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu kutokana na kifo cha Mwangosi. Akaendelea kusema kwamba anawajibika tu kwa kuwa yeye ndiye alikuwa kamanda pale lakini hakuhusika katika mauaji yale. Waandishi wakashangilia na kumpongeza kwa uamuzi wa kishujaa. Kalamu zao zikaanza kuandika habari kwa wino wa blue; hadithi yangu imeishia hapo."

  Funzo: Tupiganie haki zetu bila kuchoka hadi wapokonya haki wasalimi amri.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280
  unajua sheria ina ruhusu wawepo... ila sijui ni kwa kiasi gani tumewahi kuwatumia.
   
 9. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Watawala wametufanya mafara kana kwamba hatujui lolote.Kamhanda angekuwa wa kwanza kuwajibika.but time will tel.
   
 10. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 46,399
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  Siku zote nimekuwa nikiamini nchi yetu si ya kidemokrasia na wala haina hata sababu ya kujiita inafuata haki na usawa kwa wote. Serikali iliyopo na zilizokuwepo madarakani zipo kwa maslahi ya CCM kama chama tu. Hivyo suala la kutetea maslahi ya raia bado itakuwa katika hali ya kimaandishi kwenye vitabu vya katiba na sehemu nyinginezo.
  MMK mimi naongezea jambo moja, aliyetoa amri ya shambulio la pale Nyololo alikuwa ni RPC Kamuhanda na ndiye askari mwenye cheo kikubwa aliyekuwepo katika eneo husika, kwa utaratibu wa kijeshi damage yoyote inayotokea katika operesheni maalum mtu ambaye atakuwa responsible na kujibu tuhuma zote ni yule muongoza hiyo operesheni. Sio kwamba RPC hakujua raia mwema anapigwa, alijua na mashahidi wapo.
  Kamuhanda awajibishwe kijeshi baada ya hapo afikishwe mbele ya pilato kujibu tuhuma za mauaji.
   
 11. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,842
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  je?? Mkuu ni uongo?? Sio wametufanya sisi ni mafala wa kutupa. Ujanja wetu ni kubofya bofya keyboard tuu kukesha na kutoa ushahidi na majigambo na umwamba
   
 12. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani kamhanda namchukia kuliko maradhi yote ninayo yafahamu
   
 13. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi naamina jko siku kamhanda atatinga mahakamani na finally atakula miaka yake jela.dunia yote itaimba nyimbo za kumtukuza MUNGU.
   
 14. Baba Kimoko

  Baba Kimoko Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  nadhani ipo sheria hiyo. kumbuka watu waliomshitaki godbless lema (japo kesi ya lema haikuwa ya mauwaji) kesi ya uchaguzi. walikuwa watu kama mimi na wewe tu. isipokuwa unatakiwa ufungue kesi ya namna hiyo kama una uhakika ina interests za madikteta wetu, or utayeyuka.
   
 15. N

  Nguto JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,274
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji asante sana kwa kutuletea hii sheria. Actually post zako zote zimeenda shule. Thanks a lot!! Hivi hawezi kutokea mtu, au wanasheria wakamshtaki huyu kamanda? Kamanda ndio mshtakiwa namba moja!! Kijana wa watu alidhani anamfurahisha mkubwa wake alipofyatua bunduki yake sasa wanamshtaki peke yake!! This is not fair!! Ila na yeye alikuwa mjinga sana ni kama mtu anakwambia kula kinyesi chako na wewe kweli unakula!!! Wanasheria please jitokezni mumshtaki huyu kamanda. Invyoelekea hatshtakiwa ila atapandishwa cheo. Nyie tusubiri tu.
   
 16. N

  Nguto JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,274
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Amen!!
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,793
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Kama sheria inaruhusu sasa mbona wansheria wetu hawachangamkii hizo fursa kutusaidia sisi ambao si wanasheria. Jamani wanasheria amkeni sasa.
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,793
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo ilikuwa kesi ya madai yaani Civil Case na siyo case ya jinai yaani Criminal case. Kesi ya madai mshitaki ni mtu yeyote anayedhani hakutendewa haki lakini kesi ya jinai huwa mshitaki ni Jamhuri mara nyingi.
   
 19. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,270
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  things are happening too fast,, brain ya mtanzania wa kawaida inashindwa kuprocess,,,,
   
 20. Mzalendo2015

  Mzalendo2015 JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 1,140
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa Mwanakijiji,

  Big up sana for this vital and necessary education to Tanzanians. Hakika umeongea kama vile uko kwenye ubongo wangu. Hii SHERIA IKO WAZI KABISA KWA KILA MTU yeyote mwenye akili timamu unless awe kichaa! Tangu mauaji ya Mwandishi wa Habari marehemu Daudi Mwangosi mpaka muda huu ninapochangia thread hii sipati picha KWANINI KAMANDA MICHAEL KAMUHANDA HAJAKAMATWA MPAKA SASA!!!!Hili jambo kwa binasfi yangu linaniuma sana tena sana! Mara nyingi nimekuwa nikisema na nitaendelea kusema kuwa JESHI LA POLISI TANZANIA LIMEJAA WATU WASIO NA AKILI,KWA MAANA HIYO HAWANA ELIMU ya kusoma,kuelewa,kutafakari na kutekeleza kile walichosoma au kufundishwa! JESHI LA POLISI TANZANIA LIMEJAA WATU WALIOSHINDWA SHULE(MAJORITY OF THEM NI CLASS 7,FORM 4 OR FORM 6 FAILURES)! KWA MAANA HIYO POLISI WENGI HAWAFUNDISHIKI!!!!!KAMA MTU AMEPATA DIVISION "O" HALAFU UNAMPELEKA CCP-MOSHI,UNATEGEMEA ATAFUNDISHIKA KWELI?? HUWEZI KUWA POLISI KAMA HUWEZI KUSOMA NA KUTAFSIRI SHERIA INASEMAJE MAANA MWISHO WA SIKU POLISI UNATAKIWA WEWE NDIYE USIMAMAME MAHAKAMANI KUMFUNGULIA MASHATAKA MTUHUMIWA!

  RPC Kamuhanda amehusika na kifo cha Mwangosi kwa 99% percent na 1% inayobakia pale ilikamilishwa na na hao askari waliokuwa chini yake. Tunashangaa kuona aliyekamatwa ni afande mmoja tu anayeitwa Cleophace wakati picha za mnato na video zinaonyesha kulikuwa na askari karibu ya 10 wakiwa wamemzunguka Mwangosi huku wakimsulubisha!!!!Kama kuna mtu amesikiliza mabishano/mahojiano yaliyorekodiwa na Wanahabari kule Nyololo kati ya RPC Kamuhanda na Wanahabari atakubaliana nami kwamba Kamuhanda hakuwa anajua ni sheria ipi iliyokuwa imempeleka Nyololo. Ukisikiliza kwa makini KAMUHANDA ALIKUWA AKIONGEA KAMA MLEVI(Yamkini alikuwa amepata 2/3 za kutoa nishai hakika!)Sikuwepo kwenye tukio wala kuwa na alcoholmeter(alcohol detector)lakini huyu RPC alikuwa akiongea kilevi kabisa na dalili zote zilonyesha kuwa alikuwa amekunywa kwa kiasi!

  Mpaka sasa hatujasikia tamko lolote la IGP Mwema au Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Nchimbi kuhusu hatima ya Kamanda Kamuhanda. Inasikitisha kuona Nchimbi ameunda Tume isiyo Huru kwenda kuchunguza tuhuma ya mauaji ya Mwangosi ilhali watuhumiwa wote bado wako kazini!!!!Hiki ni kichekesho. Kama Nchimbi na Mwema hawajui taratibu na sheria zinazo guide uundwaji wa Tume walitakiwa wafanye consultation hata kwa wanasheria kabla. Kule Bandari(TPA) tumeona Waziri Mwakyembe akiunda Tume kuchunguza Ufisadi lakini Uongozi wa Juu wa TPA UMESIMAMISHWA kwanza kupisha Uchunguzi wa Tume!!!Huo ndiyo utawala wa sheria,siyo jitu linakurupuka tu ili kujifurahisha. Kwa kitendo hiki kilichofanywa na kinachoendelea kufanywa na Serikali ya CCM ili kuwalinda Polisi kwa vile ni sehemu ya Utawala wake DHALIMU hakuna HAKI ITAKAYOTENDEKA hapa. Kinachoendelea kuhusu mauaji ya Mwangosi ni UIGIZAJI wa THE COMEDY SHOW ambayo mwisho wa siku RPC Kamuhanda ndiye Starring atakayeibuka kama "THE HERO" !

  Hakika inauma sana.
   
Loading...