Sheria ya mtandaoni: Mtu anaefanya kosa akiwa nje ya nchi akirudi nchini anaweza kushitakiwa?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Mtu yuko nje ya nchi na akafanya kosa la mtandaoni kama vile kutukana,n.k akiwa katika ardhi ya nchi ya kigeni, mtu huyo akirudi hapa nchini(Tanzania) anaweza kushitakiwa?

Yaani sheria hii inavuka mipaka ya nchi?

Mwenye majibu tafadhali.
 
Mtu yuko nje ya nchi na akafanya kosa la mtandaoni kama vile kutukana,n.k akiwa katika ardhi ya nchi ya kigeni, mtu huyo akirudi hapa nchini(Tanzania) anaweza kushitakiwa?

Yaani sheria hii inavuka mipaka ya nchi?

Mwenye majibu tafadhali.
Mange asked?
 
Swali ni sheria inasemaje maana bila shaka wako wengi tu na sio huyo tu.

Sheria ya makosa ya mitandaoni inasema kuwa inatumika Tanzania Bara na Visiwani. Sheria hii haivuki mipaka ya nchi. Hata hivyo, hii haina maana kuwa kwa kuwa umetenda kosa la kimtandao nje ya mipaka ya nchi basi utasalimika.

Kuna sheria za kimataifa juu ya mamlaka ya kumshtaki mtuhumiwa aliyetenda kosa nje ya nchi. Kwa kawaida mahakama za Tanzania zina mamlaka juu ya makosa yalitendeka nchini (territorial jurisdiction).

Kwa mfano, nakatiza zangu Tandika ghafla nakutana mbongo mwenzangu espy mara anaanza kunitwanga mangumi bila sababu za msingi na kuishia kunijeruhi mie pamoja na kwamba nina "restraining order" dhidi yake. Hapo polisi wa Makonda watamtafuta hata kama kakimbilia Kibiti watamkamata na kumfikisha mahakamani kujibu mashataka. Hii inaitwa "objective territoriality".

Haya baada mbongo Heaven Sent anayeishi Sweden kuambiwa kuwa shosti wake espy kasekwa ndani anaamua kunishambulia kwa kunisemea mbovu hapa JF. Anatengeneza maphotoshop dhidi yangu na kusambaza kwenye magroup ya whatsup bongo kinyume na sheria ya makosa ya mitandao. Je, mahakama za Tanzania zinaweza kuwa na mamlaka juu yake?

Jibu ni ndiyo kwa sababu sehemu kubwa ya kosa limefanyika Tanzania. Kosa limeanzia Sweden alikopost hizo picha ila picha kazisambaza kwenye magroup ya whatsup Tanzania. Mahakama ya Tanzania itakuwa na mamlaka (subjective territoriality) kwa sababu Heaven Sent popote alipo ni Mtanzania na mie pia mbongo.

Ila sasa itakuwa ngumu kwa polisi wa bongo kumnasa huyu kiumbe na kumfikisha mahakamani kwa sababu anaishi Sweden. Labda kwa njia za kijasusi. Hali inaweza kuwa complicated zaidi kama akikimbilia Finland (the best place in the world for a woman to live). Ila akirudi Bongo tuu polisi wanae kwa kusambaza picha ovu dhidi yangu kwenye mitandao kinyume na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Tanzania ina mamlaka juu raia wake kwa makosa yaliyoodhereshwa na sheria za Tanzania. Kwa mfano, mahakama za Tanzania zina mamlaka juu ya raia wa Kitanzania aliyetenda kosa la ugaidi kwenye nchi nyingine. Kigezo ni kuwa ni raia wa Tanzania.

Tuseme Tanzania inakubali uraia wa nchi mbili, na Heaven Sent ni raia wa Sweden na Tanzania na nchi hizo mbili zinataka kumshtaki kwa kutumia kigezo cha uraia wake. Hapa mamlaka yataenda kwa nchi ambayo Heaven Sent anaishi na kufanya kazi au yalipo makazi au familia yake. Obviously hapa itakuwa Sweden.

Tuseme espy ni Mkenya na alitenda kosa lake tulipogongana Kenya. Bado Tanzania inaweza kuwa na mamlaka ya kumshtaki kwa sababu mie mjeruhiwa ni raia wa Tanzania. Tatizo litakuwa jinsi ya kumkamata huyu kiumbe wa Kenyatta unless kama kuna extradition treaty baina ya nchi hizo mbili juu kosa husika.

Vipi kama espy na mie wote wabongo na tulikutana Zambia ndo akanifanyia hivyo? Hapa Tanzania itadai mamlaka ya kumshtaki espy kwa sheria za bongo kwa kigezo cha usalama au maslahi ya Tanzania kutoathiriwa na makosa yaliyofanywa na raia wake kwenye nchi nyingine (protective principle).

Vipi kama espy na mie ni wabongo na tulikutana on transit airport Amsterdam? Hapa atashtakiwa mbele ya mahakama ya Holland hata kama yeye na mie tulikuwa tunapita njia tuu. Kigezo kinaweza kuwa kosa alilotenda ni serious na linatambulika kimataifa kiasi cha kuipa Holland mamlaka ya kumshtaki (universal jurisdiction).

So, espy be warned! Comply with the restraining order or otherwise....
 
Back
Top Bottom