Sheria ya Urithi, Mirathi na Wosia ya Tanzania

TanzaniaLaw

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
1,298
482
SHERIA YA USIMAMIZI WA MIRATHI SURA YA 352 YA SHERIA ZA TANZANIA

Mirathi Ni nini?

Mirathi ni mali aliyoacha marehemu kwa ajili ya kurithishwa warithi wake halali. Sheria imeweka taratibu maalum zinazoongoza ukusanyaji, uangalizi, usimamizi, ugawaji na umiliki wa mali za marehemu pamoja, na kulipa madeni aliyoacha marehemu wakati wa uhai wake au gharama zitokanazo na mazishi yake

SHERIA HII INASHUGHULIKA NA MAMBO YAPI NA INA LENGO GANI HASA?

Lengo kuu la sheria hii ni kutoa utaratibu wa kusimamia mali za marehemu baada ya kifo chake ikiwamo kuhamisha umiliki wa mali hizo kutoka kwa marehemu kwenda kwa watu wenye haki ya kuzipata mali hizo.

Nia hasa ni kwamba mali alizoacha marehemu zisibaki zikiharibika na kupotea bure,au warithi halali au watu wenye maslahi na mali za marehemu,kwa mfano wale wanaomdai hawapotezi haki hiyo, bali awepo mtu ambaye atazisimamia na kuzigawa kwa wahusika wakiwamo wadai na kuepusha mgongano katika jamii husika.

Hivyo sheria inamuweka msimamizi wa kugawa mirathi husika na mamlaka yake.

MAHAKAMA ZIPI ZINA MAMLAKA YA KUSIKILIZA MASUALA HAYA
Mirathi inaweza kufunguliwa katika mahakama mbalimbali kutegemea na sheria itakayosimamia mirathi husika.

Kama sheria ya kimila itatumika katika kugawa mirathi basi shauri la kuomba usimamizi wa mirathi litafunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo.Msimamizi wa mirathi anatakiwa airidhishe mahakama kwamba marehemu kutokana na maneno yake,mfumo wake wa maisha au maandishi aliyoacha,alionyesha nia kwamba mirathi yake alitaka iendeshwe kwa kufuata sheria za kimila.

Kama sheria itakayotumika ni ya kiisilamu basi shauri la kuomba usimamizi wa mirathi litafunguliwa Mahakama ya Mwanzo.Msimamizi wa mirathi anatakiwa airidhishe mahakama kwamba marehemu kutokana na maneno yake,mfumo wake wa maisha au maandishi aliyoacha,alionyesha nia kwamba mirathi yake alitaka iendeshwe kwa kufuata sheria za kiislamu.


Read more » SHERIA YA MIRATHI YA TANZANIA
 

Attachments

  • 2190057_Ijue-Sheria-Sheria-ya-Urithi-Mirathi-na-Wosia.pdf
    778 KB · Views: 38
This is so informative TzLaw. Asante sana....wacha niendelee kujifunza kiundani zaidi
 
shukrani kaka kuendelea kutuelimisha maana hapa dunia mengi yanatokea hasa wanapopatiakana ndugu wenye tamaa na mali za marehemu hata watoto wanakosa msaada wengi wetu wanakuwa ni omba omba baada ya wazazi wao kufariki
 
Back
Top Bottom