Sheria ya marekebisho ya katiba imekiuka katiba iliyopo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya marekebisho ya katiba imekiuka katiba iliyopo...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Apr 26, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Katiba ni sheria mama hivyo huwezi kutumia sheria za kawaida zinazopitishwa na wabunge kwa maana ya simple majority ya wabunge waliokamilisha koram ya siku hiyo ili kurekebisha sheria ambayo ilipitishwa kwa theluthi mbili ya wabunge kwa kila sehemu ya Muungano.

  Nimepitia jinsi Kenya walivyorekebisha katiba yao nikaelimika ya kuwa wao kwanza walikuja na muswada wa marekebisho ya katiba yao na kuweka vifungu vya kuupa utaratibu wao wa uwazi na ukweli kwa maana shirikishi nguvu kisheria ambao ulitoa mamlaka ya kuanzisha sheria za kuirekebisha katiba. Zaidi ya theluthi mbili ya wabunge walipiga kura ya kuvikubali hivyo vifungu vya kikatiba na hivyo baada ya kuifanyia marekebisho katiba yao waliweza kuunda sheria za kuunga mkono marekebisho tajwa ya kikatiba.

  Sisi tumetanguliza mkokoteni kabla ya farasi kwa maana ya kuunda sheria za kawaida kabla ya kuirekebisha sheria mama yaani katiba iliyopo ili kutoa mwanya wa hizo sheria tulizozipitisha kuirekebisha katiba ziwe hazikiuki utaratibu wa kikatiba wa kuirekebisha katiba tajwa.

  Matokeo yake sheria za marekebisho ya katiba zinapingana na muhimili wa kikatiba na ndiyo maana mchakato wake unaonekana ni batili kwa sababu haujatajwa ndani ya katiba iliyopo, hauna ushirikishi na unalenga kuzima kiu ya mabadiliko ya kweli ya kikatiba.

  Tusisahau JK and Co are mere turncoats..............si ccm manifesto au hata ngonjera za JK wakati wa kutuomba kipindi cha pili waliaahidi katiba mpya..................kwa hiyo hivi sasa wanaharakisha ili kuzima kiu ya kweli kwa kutuletea hili igizo la tasnia ya filamu babaishi.........

  Wengi ya wanaopinga sheria hii ya marekebisho ya katiba wamejikita zaidi katika kukosoa baadhi ya vifungu vyake wakati ulaini wa kufanya hivyo ni kuangalia katiba iliyopo mbona haitoi fursa za marekebisho tajwa kwa kuhusisha vyombo nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano?

  Mfano tu, uhalali wa hiyo tume kikatiba unatoka wapi? Haijatajwa ndani ya katiba iliyopo sasa inapata wapi uhalali wa kukusanya maoni ya kurekebisha katiba iliyopo? Ilipaswa kwanza katiba iliyopo itoe uhalali wa utaratibu huu mpya wa kutumia tume na hata hayo mabunge mawili katika kuipitisha katiba tajwa baada ya kufanyiwa marekebisho ambayo yataungwa mkono na theluthi mbili za wabunge wa pande mbili za Muungano.

  Haya hayajafanyika kwa sababu JK na wababaishi wenzie wanajua kabisa ndani ya nafsi zao ya kwamba hawana uhalali bungeni wa kupitisha utaratibu walioutumia kwa maana hawawezi kupata kuungwa mkono na theluthi mbili za wabunge na hivyo wakatafuta njia ya mkato ya kuanzisha mchakato wa kurekebisha katiba iliyopo bila ya kuzingatia katiba yetu imeweka utaratibu upi wa kuirekebisha na kwa kufanya vinginevyo wakawa wamekuja na sheria tajwa ambayo inakinzana na katiba iliyopo................huu ni ukiukwaji wa katiba iliyopo............

  Katiba iliyopo inatoa mwanya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania kurekebisha katiba iliyopo lakini tume, mabunge ya pande mbili za Muungano na hata kura ya maoni tajwa havijatajwa.........

  Nionavyo JK na vyama vya upinzani wanafikiri ya kuwa.................the ends can justify the means.........and vice versa......."they are dead wrong"..............well keeping the politics involved at bay I can confidently argue that this constitutional process is futile abinitio..........................badilisha katika katiba iliyopo vifungu kwanza ili ujipe mamlaka ya kuirekebisha katiba iliyopo..........acheni kutafuta njia za mkato tena za panya buku kuirekebisha katiba iliyopo...................mwishowe suala hili itabidi lifike mahakama kuu ili iamue kama kweli Bunge lina uwezo wa kikatiba wa kuunda sheria za kawaida tu.........ambazo zahitaji simple majority ya wabunge waliohudhuria kikao kile ili mradi koram tu itimie na kupitisha sheria ya kuinyambulisha katiba iliyopo ambayo ilipitishwa kwa theluthi mbili ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama siyo ukiukwaji wa katiba wa wazi kabisa..................??????????????????

  Longa maoni yako, pia...............................utusaidie kutafuta sheria bora na ambazo zitahakikishia kila mtanzania maisha bora na wala siyo hizi ngonjera tupu.........

  ENGLISH VERSION AVAILABLE TOO........


  THE HYPOCRISY OF ENACTING A NEW CONSTITUTION.


  For ccm and president kikwete, it is easier to expose their hypocrisy but with the opposition it is all a different gameplan altogether to do it! Neither did the ccm manifesto of 2010 nor did Kikwete campaign trail of the same year hinted of a political will to rewrite a new constitutional order and panning out of this both CCM and Kikwete are turncoats as far as this constitutional process is concerned. Both CCM and Kikwete embraced a new constitutional process just to stay relevant in our political terrain but have neither the determination nor the political will to bequeath to us a well meaning constitution. But the opposition ranks can easily deceive many if you have been keen at following the ear deafening decibels generated by them. To their credit some opposition parties had garnished a quest for a new constitutional order into their manifesto and made that an election issue, too. After a bungled 2010 election where the real winner of presidential race was flashed out by unjust electoral system well oiled by the government in power through NEC (a national electoral body carefully handpicked by an incumbent president to do him a favour and announce him as a president –elect) and TISS ( an intelligence national body that is notorious at rigging all our post-one party elections since 1995), the opposition went berserk demanding a new constitutional order that will assure them people's power that was perceived stolen from them by the treacherous electoral terrain.
  On their part, ccm through ministerial outbursts the impression we were getting was that the effort to rewrite the constitution was too costly and an exercise in futility. But ccm; seeing that it was getting the scissors whether from the streets or from the vociferous media waves, decided to cave in, in a manner that will protect the interests of the status quo ante. First ccm avoided to follow the law where in the hitherto constitution only the house has the power to effect the changes it deems fit. The problem for ccm were multifarious in many fronts: First almost one third of members of the House belong to the opposition bench and a number of young ccm MPs who refuse to kowtow the established party position is growing in line with the public opinion. Under this new political complexion, ccm mandarins felt insecure to follow the constitution in enacting the law that will guide the whole constitutional changing process.
  According to Rev. Mtikila v. Attorney General Case urging for independent candidates, the full bench of the Appeals court made it clear that it is only the House that has the legal power to change the constitution and if the process clearly laid down in the constitution was not followed the courts could be called to interfere and rectify the illegalities. But now ccm led constitutional process has defied the highest court of the land when it embarked to enact an act of parliament that has vitiated the constitutional onus of the House to rewrite the constitution! Out of this, unconstitutional creatures such as the presidential commission empowered to collate constitutional views, two Houses of Isles and of the United Republic of Tanzania let alone referendum leeway were enacted to confuse the electorate that we are on the right track to deliver a new order while the concomitant order was only being hacked to receive a cosmetic facelift.  Parliament has no powers to incorporate or delegate her constitutional authority in the existing constitution and by extension cannot seek solace via a simple majority voting process to revoke what the House has enacted in the constitution through a two third majority. The solution to this archaic encroachment to the existing constitution under frivolous excuses that the ends can justify the means is out right wrong and we ought to ask the constitutional court to rectify these colossal anomalies via court injunctions pending a final determination of the main constitutional dispute.
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Tatizo la nchi yetu kila kitu kinaendeshwa kishkaji tuu, ninaamini Kikwete angeajiri washauri makini pale Ikulu ujinga wote huu usingeweza kutokea, kwasababu kila kitu kinafanywa kimtandao bila kujali sifa ndo matokeo yake haya. Nchi hii vichwa ni vingi sana tatizo siyo wanamtandao.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Ezan unaamini kuwa ni kishikaji tu?
  Huoni ya kuwa hawa mafisadi wana malengo fulani ya kupitisha mambo yao kinyume na utaratibu wa kikatiba baada ya kuona ya kuwa hawana theluthi mbili za wabunge Bungeni kuhalalisha uozo wao?.........mimi ninaamini ya kuwa wanafanya kwa makusudi mazima ili kufnikisha dhamira zao......
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka huo utaratibuw a kuanza kurekebisha katiba kwanza uloishawahi kupendekezwa na Mnyika lakini wakamuona chizi. Kwa hakika, tunachokifanjya kinaweza kugeuka kuwa shubiri huko mbele ya safari kwa kutozingatia matakwa ya kisheria kama haya. Kuna baadhi ya watu wameshaanza kuloichukulia suala hili kisisasa zaidi. Na tatizo, wananchi wengi wa Tanzania wanaburuzwa tu bila kuelewa hasa kinachotokea ni nini.
  Mathalani, kama kweli wana nia ya kuwapa watu uhuru wa kuandika katiba wanayoitaka, kwa nini waweke masharti, kwa mfanop, msizungumze kuhusu kuuvunja Muungano! Kama hisia za watu ni kutoutaka Muungano, hivi watatoa maoni gani ya maana ambayo yataifanya katiba itokane na maoni yao wakati yale wanayoyafikiria wao wamekatazwa wasiyayaseme?
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Inatia uchungu, inauma, inasikitisha, inadhalilisha lakini yetu macho.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ruta,
  Hii ni zaidi ya ushkaji, Rais kama Mkuu wa nchi ndiye anayetakiwa kuunda tume ya marekebisho ya Katiba.
  Rais huyo huyo ni Mwenyekiti wa chama tawala ambayo inafaidika na ubovu wa katiba tuliyonayo
  Rais huyo huyo ndiyo chanzo cha ufisadi na ubadirifu mkubwa wa mali ya umma.

  Hapo usitarajie makubwa, na kilichotokea na kinachoendelea ni kuwa mazingira yoyote ya marekebisho ya katiba yataipendelea serikali ya Mkulu.

  Kwa maoni yangu,
  Kwa kuwa serikali yetu imeamua kukumbatia dola kwa maana ya Jeshi ili wajilinde na nguvu ya wananchi, bado suala la marekebisho yoyote ya katiba au jambo lolote lenye manufaa kwa maslahi ya umma lipo mikononi mwa wananchi wa tanzania.
  Watanzania waandaliwe vya kutosha kuelewa nini wanafanyiwa na serikali iliyopo, waandaliwe elimu ya demokrasia, waandaliwe kutambua haki zao pamoja na mambo mengine.
  Baada ya hapo tulianzishe la kigeto geto kitaeleweka tu.
  Nguvu ya umma haijawahi kushindwa popote duniani, ni kiasi cha kuwaanda tu watu, na pia jeshi lielewe kuwa wanalipwa kwa kodi za watanzania wanaoonewa na kudhihakiwa na serikali ya ccm.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 7. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hebu kwanza tujiulize sisi tunahitaji Katiba mpya au Uongozi mpya? Maana nimesikia mara nyingi ikisemwa "kama katiba ikirekebishwa, CCM lazima ishindwe".

  Mimi naungana Jenerali Ulimwengu kwamba tuchambue yale mambo ambayo wanasiasa wapenda madaraka wanayaona kwamba ndiyo "katiba" na tuyarekebishe na tuwaache wao wanagombania madaraka wakati sisi tunatafuta muafaka wa Kitaifa.

  Hoja kama tume huru ya Uchaguzi, mgombea huru (siyo binafsi), matokeo ya kura za Uraisi kuhojiwa mahakamani,haki ya kutangaza matokeo ya awali,jinsi ya kujiandikisha,kupiga,kuhesabu na kutangaza matokea ya uchaguzi ni mambo ambayo tunaweza hata kwa kutumia bunge hili hili tulilonalo tukayarekebisha na kuwapa "wanasiasa" wanachokitaka na sisi tukapata nafasi ya kutunga katiba mpya kwa manufaa ya nchi yetu.

  Eti kwa miezi kumi na nane tunatafuta muafaka wa kitaifa kwa taifa lililo na umri zaidi ya miaka 45, haya ni maskhara!!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Well said.......................Na kikubw ana kuruhusiwa kwa wagombea binafsi.................
   
 9. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Suala hili lilionekana mwanzo, na ninakumbuka hata kwenye kongamano la UDASA pale UDSM lilijadiliwa. Mh. Myika JJ alisema atapeleka hoja bungeni ili katiba ifanyiwe marekebisho kwanza kabla ya mchakato wa hii sheria ya mabadiliko kuanza kwani ukianza bila matakwa ya Kikatiba mchakato wote utakiuka katiba iliyopo kama wewe unavyosema.

  Cha kushangaza ni kwamba ile hoja imepotea kiajabu ajabu na hakuna mtu aliyejisumbua kuhoji huko Bungeni. Shukrani kwako kwa kuihoji huku uraian
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  kwa vile bunge limekataa kurekebisha katiba kuruhusu mchakato wa kuirekebisha katiba ukubalike basi ni mahakama tu ndiyo msuluhishi wa mwisho.............haiwezakni watu wakatafuta majibu mepesi kwa mswali magumu.......
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  twende mahakamani tusimamishe huu upuuzi wote khalafu wakajipange kwa upya kabisa................wajue TZ ina wenyewe
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  maudhui ya kipi kiwepo kwenye katiba au kisiweko yaje baadaye kwanza utaratibu lazima uingizwe kwenye katiba kwanza........
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  kigarama uko sahihi.................wasisingizie katiba mpya kukwepa kutekeleza majukumu yao.............ili kwenda uchaguzi ujao tunahitaji minimum refroms kama hizo ulizozitaja.....................lakini la katiba mpya twende nalo polepole...............na dawa yao ni kuweka injunction utaratibu huu wote mahakamani hadi suala hili la kimsingi limepatiwa ufumbuzi.........
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  niaafiki na hii misimamo namna rahisi ya kuwashtua hawa wababaishaji ni kuwawekea court injunction hadi suala la kimsingi litakapopatiwa ufumbuzi.......
   
 15. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja kwa asilimia 100.
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  tuifufue hoja tajwa katika mahakama kuu hawa akina mnyika wao ni nguvu ya soda tu..........kuna maana gani ya kuanzisha hoja khalafu ushindwe kuitetea mahakamani kama unaona bungeni umeelemewa?
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Waache wacheze makida, wakileta mchezo tutakutana kwenye kura ya maoni
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  kuraya maoni haijatajwa kwenye katiba kwa hiyo tukiwaruhusu kufika huko tutakuwa tunahalalisha ukiukwaji wa sheria na hiyo katiba itakuwa ni batili kutokana na ubatili wa utaratibu uliotumika......
   
 19. Mukhabarat

  Mukhabarat Member

  #19
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa sheria ya mabadiliko ya katiba kukataza wananchi wasijadili kuhusu kuwepo kwa muungano au la ila kwa nia ya kuuboresha tu huko ni kuminya uhuru wa kutoa maoni, na sheria hii inalazimisha kuwepo kwa muungano na kuwepo kwa serikali ya mapinduzi zanzibar, kwa hiyo hapo mwananchi anabakia na maoni ya serikali tatu au mbili kama zilivyo sasa, maana yake ni kuyaweka jela mawazo ya watu kwa kuwachagulia mambo ya kusema badala ya kuwaacha waseme wanavyotaka! serikali inaogopa nini kuwapa watu uhuru wa kutoa mawazo yao bila kuwapangia cha kusema? je kweli katiba hii itakuwa na haki ya kuitwa imeandikwa na wananchi wenyewe? tatizo ni nini iwapo mwisho wa siku watu watapiga kura ya maoni, mchakato huu ni sawa na mwalimu kuwachagulia wanafunzi topics 4 kutoka kwenye syllabus yenye topics 10 baadae anawapa mtihani kutokana na hizo topics 4 alizowafundisha halafu wakifaulu huo mtihani aseme wamefuzu kumbe si kweli kwa sababu ili wafuzu walitakiwa wawe na uelewa wa topics zote kumi za kwenye mtaala huo.
  Katiba mpya inaweza ikaja lakini naamini haitotatua sintofahamu ya muungano ndo maana mimi naungana na wazanzibari wanaotaka kwanza kura ya maoni kuhusu muungano halafu ndo tujadili katiba kwa maana matokeo ya kura ya maoni ndo yatakayoamua kama tunahitaji katiba ya muungano au vinginevyo.
  NB: KASHESHE ZA MUUNGANO ZITAENDELEA KUWEPO
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ta Ruta,


  Binafsi nilishasema kuwa JK na serikali yake hawana nia njema kwenye suala la katiba mpya. Toka mwanzo, Waziri Kombani na AG walikuwa wanajikanyaga kwani hawakujua kitu gani wananchi wanataka. Hata JK mwenyewe hakujua pia na alikiri hayo mbele ya vingozi wa CHADEMA.

  Hata Wabunge walipoptisha mswada wa hii sheria kwa mara ya kwanza, nilionga na baadhi yao na kuwaeleza kuwa wangetumia busara kidogo kujielimisha ni kitu gani hasa wananchi wanahitaji. Badala yake, viongozi wetu wameendekeza ushabiki.

  Kwa hapa tulipofika, tunahitaji akina Mtikila kuchukua hatua ili kutuepusha na huu usanii ambao unaweza kutuletea matatizo makubwa huko mbele ya safari.
   
Loading...