Sheria ya Manunuzi Yaanza Kung’ata....Posho Zafyekwa, Vikao Vyapunguza Kutoka 12 Hadi 4

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
MAREKEBISHO ya Sheria mpya ya Manunuzi, yamewasilishwa bungeni yakitamka kufyeka posho za watendaji, wanaosimamia mchakato wa zabuni na kuondoa vikao vya bodi kutoka 12 kwa mwaka hadi vinne, ikisisitiza kuziba mianya ya rushwa na kuongeza uwazi.

Aidha, muswada wa marekebisho hayo, unataka kampuni au mshauri wa nje ili apewe zabuni katika shughuli zinazogharimiwa na fedha za umma, ahakikishe asilimia 60 ya wafanyakazi wa kampuni yake ni Watanzania.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, aliyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akiwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016.

Kupungua kwa vikao vya bodi, kumeelezwa na Dk Mpango kuwa kutapunguza gharama zinazotokana na posho ya vikao vya bodi ya zabuni na ada zinazolipwa kwa kamati zinazohusika na mchakato ya zabuni.

Aidha, posho zinazotokana na utekelezaji wa majukumu ya kazi ya kila siku ya washiriki itafutwa. Hata hivyo, imeruhusu kuwapo kwa vikao vya dharura pale Mwenyekiti wa Bodi akiona ni lazima.

Pamoja na kupunguzwa vikao, muda wa zabuni nao umepunguzwa na pia taasisi nunuzi itaruhusiwa kufanya majadiliano ya bei wakati wa mchakato wa zabuni kwa lengo la kupunguza bei ya ununuzi na kuongeza bei ya kuuza mali za serikali.

Dk Mpango alisema pamoja na kuongeza uwajibikaji, sheria hiyo mpya itapunguza vikao vya bodi hadi kuwa kimoja kwa robo mwaka na vikao vya dharura, kufanyika pale ambapo mwenyekiti ataona inabidi.

Pamoja na maelekezo hayo mapya, serikali pia itaanza kununua bidhaa na huduma kwa bei inayoendana na bei ya soko, iwapo wabunge watapitisha marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Pamoja na ununuzi wa bei ya soko, sheria mpya imelenga kuweka sharti la kisheria kutoa upendeleo katika zabuni mbalimbali, hasa kwa makundi maalumu kama vile wanawake, vijana, wazee na watu wenye mahitaji maalumu.
 
Kama itatekelezwa kwa ufasaa na hao watakoitekeleza basi itakuwa labda ni hauweni kwa matumizi ya serikali.
Ila kama itakuwa inatekelezwa na hao wapiga dili. Watatafuta namna na watu watapiga kama kawaida....
Hongera kwa serikali kwa nia nzuri, tusubirie kwa kwa watekelezaji kama nao watakuwa na nia nzuri....
 
Kama itatekelezwa kwa ufasaa na hao watakoitekeleza basi itakuwa labda ni hauweni kwa matumizi ya serikali.
Ila kama itakuwa inatekelezwa na hao wapiga dili. Watatafuta namna na watu watapiga kama kawaida....
Hongera kwa serikali kwa nia nzuri, tusubirie kwa kwa watekelezaji kama nao watakuwa na nia nzuri....

= ahuweni
 
kitu nachojua nchii hii hakuna waziri wa fedha,ebu soma paragraph ya mwisho alafu utafakari kwa kina.
 
unapunguza vikao toka 12 adi 4 alafu unaruhusu vya dharula,ni kwamba hivyo vilivyopunguzwa vitabadilishwa kuwa vya dharula.
Kiufupi sioni mantiki ya kupunguza hivyo vikao,kufanya vikao 12 kwa mwaka (wastani wa kikao kimoja kwa mwezi) sio mbaya.
 
Ni kweli vikao vya dharura na vyenyewe viwekewe utaratibu ili watu wasitumie kama mlango wa kupenyeza tenda zenye magumashi
 
Kuna wakat unalazimika kumpenda rais na serkali yake walau kwa ngazi ya theory. Katika Utekelezaj labda nitaandika kinyume! Mi siku zote nasema demokrasia haina maana kama haitupelek mbele. Hata nchi za kifalme zilipata kuendelea kama mtunza kibubu ana nia ya kweli. maendeleo ni from bad to good, better to best. 'Irresponsible' Democracy is just another wall ...!
 
Safi sana. Lakini bado kuna maeneo mengi. Eneo moja lenye matumizi makubwa serikalini ni magari. Nashangaa kwamba bado awamu hii nayo imeamua kukaa kimya kama vile haioni. Hii nayo ni "flow meter" nyingine ambayo fedha za serikali zinapotea kwa mamilioni. Tukiamua kufanya mageuzi ya kikweli na kuondoa kabisa "ubwanyeye" katika serikali yetu, ni lazima issue ya magari ya serikali ishughulikiwe pia.
 
Ushauri mwingine wa kupunguza matumizi makubwa serikalini: Punguza idadi ya magari na kuacha kwa watendaji wachache tu wenye dhamana kubwa (Labda Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu?) na wengine wote wauziwe na kupewa posho ya mafuta ili wajiendeshe wenyewe, na kugharamia matengenezo ya magari yao. Fedha yote itakayookolewa iende kwenye budget ya kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma. Tuachane na kuwapa mishahara ya shs 600,000 watumishi kama vile hatuelewi gharama halisi za maisha siku hizi. Mfumo wa sasa serikalini bado ni kibwanyenye sana. Yaani mtu anayepata mshahara mkubwa (Say Katibu Mkuu), ndiye pia aliyejaziwa privilege kibao ikiwemo gari la serikali, kulipiwa nyumba, umeme, simu, maji nk, wakati mtumishi wa kawaida anayepata mshahara mdogo sana, hana privilege yoyote. Mfumo huu unadhalilisha sana, na nawaonea huruma sana watumishi wa umma wa ngazi za chini.
 
Back
Top Bottom