Sheria ya manunuzi ya Umma ipitiwe upya huwezi fananisha manunuzi ya dawa na matofali

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Huu ni wito kwa watunga Sera

Upo umuhimu wa Sheria ya manunuzi ya umma kupitiwa upya.

Haiwezekani Taratibu za kununua matofali au karatasi zikafanana na manunuzi ya dawa na vifaa tiba.

yaani paracetamol au gloves zikiisha utaratibu wa manunuzi ulingane na ule wa kununua tofali la kujengea; hapa ni lazima tuangalie upya.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Sheria ya Manunuzi ya Umma ikisomwa vizuri na kwa weledi haijaacha ombwe lolote, tuache visingizio ili kukwepa taratibu za manunuzi, tuache visingizio vya ugumu wa sheria kwa manufaa binafsi.
 
Mleta mada huna ufahamu wa kutosha kuhusu jambo unalozungumzia. Taratibu za manunuzi zinapaswa kufanana, tofauti kubwa huwa kwenye thamani ya manunuzi ili kufanya manunuzi ya thamani kubwa kuchukuliwa na mamlaka za juu!

Kama dawa zinafikia kununuliwa zikiisha, hilo sio tatizo la sheria za manunuzi. Ni udhaifu katika demand forecast, au long lead times, au reorder points kuwa karibia na sifuri, au kukosekana kwa safety stock na mambo mengine kama kuwa na supplier asiyefaa. Madhaifu hayo sio ya sheria za manunuzi, ni wa mipango ya manunuzi (acquisition au requirements planning).
 
Back
Top Bottom