Sheria ya Mafao miaka 55, wafanyakazi wamehusishwa?

Acha hizo wewe wabunge wa magamba a.k.a wagonga meza wanaweza kumshirikisha mtu katika maslahi yao kweli??Think twice!!

Vipi KIJOME huwezi kuangalia mbali zaidi ya UREFU WA PUA yako? Kitendo tu cha kumpigia kura mbunge wa Magamba tayari umeshirikishwa. Sema jingine? haiwezekani Watanzania wote twende Dodoma, ndiyo maana tunachagua wawakilishi aka Wabunge. Hautuwezi wafanyakazi wote kwenda SSRA kujadili hiyo hoja, ndiyo maana tuna viongozi wa TUCTA.

Make no Mistake mimi napinga sheria hii mbovu. Lakini utetezi wa KUTOSHIRKISHWA ni utetezi ambao hauna mashiko because TUCTA na Wabunge wameshirikishwa hadi kupatikana kwa sheria hii.
 
Ilijadiliwa na kupitishwa kwenywe BUNGE la APRIL 13, 2012. JK akasign chapuchapu na imeanza kutumika tangua JULY 1, 2012.
Wakati sheria hii inaandaliwa na kujadiliwa, kilichokuwa kikisemwa kuwa ni dhamira ya sheriahiyo ni kuungnisha mifuko ya hifadhio ya jamii ili kuiweka chini ya chombo kimoja - SSRA. hili la kukatisha kuchukua sent zetu wala halikusemwa.
 
Wakati sheria hii inaandaliwa na kujadiliwa, kilichokuwa kikisemwa kuwa ni dhamira ya sheriahiyo ni kuungnisha mifuko ya hifadhio ya jamii ili kuiweka chini ya chombo kimoja - SSRA. hili la kukatisha kuchukua sent zetu wala halikusemwa.

KUSEMWA na KUANDIKWA ni vitu viwili tofauti, halikusemwa because dhamira yake ilikuwa mbaya na wanafahamu wafanyakazi tungelipinga. Lakini liliandikwa, wale wote walioshiriki mchakato huo (SSRA, TUCTA, WABUNGE) kwa kuusoma muswaada wenyewe kila kitu kilikuwa kimeandikwa IN BLACK AND WHITE.
 
Vipi KIJOME huwezi kuangalia mbali zaidi ya UREFU WA PUA yako? Kitendo tu cha kumpigia kura mbunge wa Magamba tayari umeshirikishwa. Sema jingine? haiwezekani Watanzania wote twende Dodoma, ndiyo maana tunachagua wawakilishi aka Wabunge. Hautuwezi wafanyakazi wote kwenda SSRA kujadili hiyo hoja, ndiyo maana tuna viongozi wa TUCTA.

Make no Mistake mimi napinga sheria hii mbovu. Lakini utetezi wa KUTOSHIRKISHWA ni utetezi ambao hauna mashiko because TUCTA na Wabunge wameshirikishwa hadi kupatikana kwa sheria hii.
Tatizo mkuu magamba wengi sio chaguo la wananchi kwa mfano mi natokea jimbo la segerea makongoro hatukumchagua yeye ni mbunge wa nec na alishasema hamkunichagua ni juhudi zake binafsi sasa hapa kuna uwakilishi kweli?mtu kama mgulu anamtambua raia wa iramba choka mbaya kweli?Hili ni changa la macho hakika wanataka kutudhulumu pesa zetu....
 
Huku ndiko kusimamia masilahi yetu? SSRA ACT 2008 section 5.
Xs4JtU4hBqHUOMQahxCjUOocQg1DqHGIdQ4hP5rHMaT+qkob1DjCPQHXzo2WYtDdbMAAAAASUVORK5CYII=
5(1)
ldYHJeicWQngdPOKqUFgd4jdI+sFtruRpuL7kC2FDPO2uUFgSiR9zRS5dVZnc675eE3VfFwoP4pnvWH3Vl0YdX6HwCOqbVigUCmug7utCoVBYA3VfFwqFwhr4B+bOOL7prttCAAAAAElFTkSuQmCC
5(2)
AGD0iT5bqzEuAAAAAElFTkSuQmCC
 
Kinachonishangaza wamepitisha hii sheria bila kuangalia wafanyakazi wa sekta binafsi ambao guarentee ya kazi zao si miaka 55 kama wanavyodani wao huko serikalini.
**Sekta binafsi wanaweza kufanya kazi mwaka mmoja au hata usizidi na kuachishwa kazi au kuacha ..na sasa ajira zilivyokuwa ngumu ...
Hili sijui wameliangalia vip?????????????????????
 
UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKOYA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.


1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.


2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.


3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.


4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.


5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika


6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.


7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.


8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.


9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.


Wenu.


Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU
 
Kwa hili wahusika wawe makini. Bora watambue kuwa ni rahisi sana kuzuia maandamano ya waumini, wanasiasa na wafanyakazi kuliko haya ya wanachama wa NSSF maana tuko wengi na haitakuwa rahisi ktulizwa pale ambapo sera za kipumbavu zinataka kuingilia maslahi zetu. Kumbuka kuwa life-expectancy ya mtz ni 47 na maisha ya mtz mwenye mshahara mdogo anaishi kwa shida sana akitegemea kupata chochote cha kumuinua pale aachapo au kuachishwa kazi.

Sasa hii miaka 55/60 imeletwa na nan jamani kama c kuleta balaa! mim siamini kama ni kweli,yangu macho.
 
Jamani maandamano na migomo ndiyo suluhisho la hizi haki zetu tunadhulumiwa mchana kweupeee jamani tuungane kudai haki zetu
 
Kwanza huu ni wizi ,kwanini unipangie namna ya kutumia pesa zangu? Je maisha ya mtanzania ni miaka 55?je wafanyakazi wanamkata na Mungu wa kuishi Miaka 55-60? Hakika nashaka na hii mifuko,mwaka 2015 lazima kieleke kama watapitisha hii sheria ya kuiba mafao ya watu.CHADEMA mpoo!!!!!!!!!!
 
Tuweke tofauti zetu pembeni tuungane, kauli iwe moja tu 'HATUTAKI DHULMA' kama serikali haitaki kusikia kilio chetu basi TOOLS DOWN. Huo ndiyo ushauri wangu.
 
Serikali imepitisha sheria rasmi kuwa hakuna mtumishi yeyote anaeweza kuchukua mafao yake katika mfuko wowote wa pensheni mpaka tu afikie umri wa kustaafu miaka 55 kwa hiari au 60 kwa lazima.

Uamuzi huu unazua maswali yafuatayo:-

1. Je, mdau wa kwanza katika hili ambaye ni mfanyakazi amehusishwa katika maamuzi haya?
2. Je, Mifuko hii ya Pensheni itaongeza riba katika michango? maana ikumbukwe kuwa thamani ya milioni moja ya leo si sawa na milioni moja baada ya miaka 10 ijayo.
3. Iwapo mtumishi hahitaji tena kuajiriwa na kuchangia katika mfuko, kwanini pesa hii asipewe afanyie kazi anazozijua mwenyewe za kimaendeleo?
4. Kwanini serikali inawakumbuka wananchi pale tu inapohitaji jasho la wananchi?
5. Kwanini serikali impangie mtu binafsi mahitaji yake?
6. Uwezo wa kutumia mafao haya kujipatia mkopo wa nyumba ni kweli au changa la macho?

Majibu mengi yanahitajika katika hili kuweza kuwasaidia wafanyakazi kujua nini faida na hasara za kusubiri hadi umri wa kustaafu ndipo mfanyakazi aweze kuchukua mafao yake.

Inaonekana Watanzania wengi tunashindwa kujua nini hasa maana ya pensheni na hifadhi ya jamii. Kwanza kwa kifupi kabisa nianze kwa kudefine hifadhi ya jamii. Hifadhi ya Jamii ni utaratibu uliowekwa unaomlinda mtu dhidi ya majanga mbalimbali ya maisha yanayopelekea kumuondolea au kumpunguzia kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa kupata kipato. Majanga hayo ni kama; uzee, ugonjwa, ulemavu kufiwa na unayemtegemea na mengineyo.

Hifadhi ya jamii ina misingi ya bima, yaani inakuwa na hali ya kuchangiana.Unapopeleka mchango wako ni kama unalipa premium, ila tofauti yake na normal insurance ni kwamba pale ambapo hutapata janga na ukafariki kabla ya kustaafu wategemezi wako wanapata mpaka kipindi fulani ambacho inakadiriwa wataweza kuishi bila kutegemea mtu, therefore kwa principles za social security, you can only access benefits zako only when unapata matatizo yatakayopelekea kuondoka kwa uwezo wako wa kuzalisha kipato.Hizi withdrawals zilianzishwa kimakosa, very contrary to the principles of social security.

Hii mifuko pia ipo ya aina mbili,Provident na Pensheni. Kwenye provident (akiba) mchango wako unawekezwa na unapata interest on ule mchango, na iwapo mfuko unapata hasara inakula kwako. Kwenye pensheni unakuwa una package ambayo inakuwa pre determine na formula. Unapostaafu unapata what the formula brings up regardless ya return on investment ya mfuko husika. Ndio maana utasikia kwamba inahitajika mtu achangie for certain period ii aqualify kupata pension, na usually what you get is much higher than what you contributed na pension inakuwa calculate using ur last salary au average of certain number of last salaries hence hate kama umefanya kwa miaka 40, what you get as pension itakuwa meaningful at the time unaanza kuipata.
 
Hii serikali ina watu waliochafuka na kunuka rushwa. Kama ni sheria wamepitisha iwe ni kwa wanachama wapya kama walivyofanya kwenye misamahaa ya kodi ya mafuta kwenye makampuni ya uchimbaji madini. Mbona wamesema sheria inafanya kazi kwa makampuni mapya ila wale wa zamani haitawahusu.

Kuna matatizo makubwa sana katika utendaji wa watu serikalini na viongozi wa ccm wamekuwa katika mbio za kumuua mfanyakazi. Mtu anaanza kazi na miaka 20 au 25 anaacha kazi na miaka 35 na kufanya biashara, pesa zake ndio asubiri mpaka miaka 55 kweli! Na siku atakapoenda kudai hii mifuko itakuambia katuletee risiti za michango,utapata wapi na makampuni mengi yanakufa na mengine kuondoka.

Wanasema watakupa mikopo ya nyumba, je ni wangapi wanahitaji hizo nyumba na ni wangapi watakuwa na uwezo wa kukopa kwa mishahara ilivyo midogo. Je na mtu akikopa nyumba akashindwa kulipa kwa kutokuwa na kazi atasamehewa au watasubiri mpaka kizazi chake kife wachukue nyumba.

Kama tu serikali inasema kampuni inapofanya redundancy mtu anatakiwa kulipwa mshahara wa wiki moja kwa kila mwaka wa kazi kwa miaka isiyozidi kumi,huyu mtu ataponaje kwa kweli. Mwaka 2007 serikali ilikuwa inagawa viwanja kwa sh 1.5mil mpaka 4mil kwa low density sasa hivi kila sqm 1 ni sh elfu kumi ina maana medium low utakuta winaenda mpaka mil 15 sasa hii mifuko inaweza kufidia hii inflation?

Iweke na risk allowance kwani hakuna mtu anaamini ataweza kufika miaka 55 kitu ambacho ni risk na inahitaji return kubwa zaidi (the higher the risk, more return). Hawa wanaojiita madokta sijui wamesomea wapi? Very stupid.

Angalieni insurance policies umri ukiwa mkubwa unalipa premium kubwa sana kwenye life insurance wanajua wewe wa kufa tu na ni hasara. Hizi sheria wanatunga kwa ajili ya kumnyonga mfanyakazi huku wenyewe wakijitafutia safari zisizo na maana kula kodi zetu na michango yetu. Magamba you'll definitely pay for this sooner or later!


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom