Sheria Ya Madawa Ya kulevya Nchini Ni Lazima Ifanyiwe Marekebisho

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Wana Jamvi mtakubaliana na mimi kuwa Vita dhidi ya madawa ya kulevya Ni kubwa sanaa na Inahitaji Nguvu ya Hali ya juu sana!

Hii vita sio ya Mkoa mmoja Dar tuu hapana! Bali inatakiwa iwe ya Mikoa yote Tanzania na Sio Dar peke yake kwasababu Madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa kwa kila mkoa! Japo naamini wapo wakuu wa mikoa wengi watakao mfuata Makonda katika hili kwenye mikoa yao Lakini umakini na Nguvu kubwa inahitajika!

Hii vita sio dhidi ya Wasanii tuu lakini hadi watu wengine japo naamini huu ni mwanzo! Ingawa Watu wanasahau kuwa Bangi na Mirungi ni madawa ya kulevya lakini naona Wamebase kwenye unga tuu!! Hii vita nadhani Mkoa wa Arusha na Kanda ya ziwa nguvu ingekuwa kubwa sana! Japo wapo viongozi wanaojihusisha na Kuvuta bangi na mambo mengine!

Moja ya nguvu zinazotakiwa ni Pamoja na Kuifanyia Marekebisho sheria ya Madawa ya kulevya! SHERIA YETU INASEMA KUKUTWA NA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA NI KOSA KISHERIA! LAKINI SIJAONA SEHEMU INAYOSEMA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA NI KOSA KISHERIA

Hii inamaana kwamba Mtu anae tumia madawa ya Kulevya ukimkuta ametumia madawa ya kulevya na hujamkuta nayo, HUWEZI KUMFUNGA MAANA SHERIA HAISEMI HIVYO! sasa katika vita kama hii mtu akiwa Anawasheria makini atashinda kesi na Mtmkuta mtaani.....Sasa wote walio Tajwa sijaona mtu alie Kamatwa na Madawa ya kulevya ila wanahisiwa kujihusisha na madawa ya kulevya either kusafirisha au kuuza au kutumia! Hii vita Makonda pekee Haitaiweza!

Mwakyembe,Nchemba,Majaliwa,Mkuu wa Mkoa na Rais JPM wanahitaji nguvu ya Pamoja katika kupambana na hii vitaa kubwa!

Tujikumbushe tuu hii sheria haijanza leo ilikuwepo Tangu Na Tangu toka kipindi kile RAY C anasaidiwa na RAIS wa nchi kuondoka katika utumiaji wa Madawa la kulevya baada ya kutokuwa na msaada na kuchoka kabisa RAIS wanchi ndie alie muinua na Kumsaidia kuondokana na Matumizi ya madawa ya kulevya Tukumbukwe hakukutwa akitumia ila alikuwa mtumiaji ndo maana sheria haikufuatwa maana Angeshinda kesi!

Mimi sio mzuri wa sheria lakini Wanasheria mtatusaidia katika hii sheria!
 
Nimekusoma Mkuu..

Hili unalolisema nimeona hata mahali fulani Advocate Albert Msando akiliongelea kama mojawapo ya mapungufu ya Sheria hii ya madawa ya kulevya.

Kwamba inamtaja anaekutwa na anaesafirisha madawa ndio wenye makosa.

Sheria haisemi mtumiaji wa madawa ya kulevya ana makosa.

Ngoja wanasheria watusaidie zaidi kwenye hili.
 
Hii sheria inatakiwa irekebishwe na iseme wazi kuwa unapotuhumiwa na kutajwa tajwa na watu tofauti wasiopungua 5 kuwa fulani ni mnufaika wa biashara hiyo AFUNGWE si chini ya miaka 5. Bila kujali unafanya biashara hiyo au la na kwamba umekutwa na ushahidi au la.

Lengo hapa ni kwamba Tufike mahala kila mtu afqhamike biashara au kazi yake na si kuishi kimagumashi magumashi.
 
Nimekusoma Mkuu..

Hili unalolisema nimeona hata mahali fulani Advocate Albert Msando akiliongelea kama mojawapo ya mapungufu ya Sheria hii ya madawa ya kulevya.

Kwamba inamtaja anaekutwa na anaesafirisha madawa ndio wenye makosa.

Sheria haisemi mtumiaji wa madawa ya kulevya ana makosa.

Ngoja wanasheria watusaidie zaidi kwenye hili.
Hakika mkuu lazima umakini katika sheria uzingatiwe
 
Mkimaliza kurekebisha sheria ya madawa ya kulevya warudi kwenye boda boda hili dude linamaliza nguvu kazi ya Taifa kuliko hata hayo madawa

Cc MOI watathibitisha nisemayo wodi zimejaa majeruhi wa boda boda

Mikoani huko ndio usiseme jamani boda boda ni janga lá kitaifa
 
pia adhabu ya faini kwa wanaokamatwa na madawa ya kulevya iondolewe badala yake ibaki kifungo na kutaifisha mali kwani biashara hii inahusisha watu wenye nguvu wenye uwezo wa kuhonga majaji,polisi na taasisi nyingine za kisheria
 
Watanzania, salaam!
History ya MADAWA ya kulevya nchini inasikitisha - vijana wetu wanaharibika kutokana na kubwiya Unga. Mwisho wake taifa litakuwa na vijana wasiokuwa na tija katika uzalishaji mali.

Hata hivyo binafsi nikiwa na uelewa mdogo kuhusu Vitengo hivi vinavyopambana na dawa za kulevya ni kuwa:-
1. Upo uwezekano mkubwa askari wengi ni dealers wa unga - hii inathibitishwa na ukweli kwamba haiwezekani wasiwe wametekeleza kabisa wauza dawa.

2. Takribani tangu kifo cha hayati Mhe. Amina Chifupa (mb) ambaye tayari alibainisha kutaja dealers wote doc ikiwepo mpaka sasa tuwe hatujatengeneza kikosi matokeo kwa ajili ya kufuatilia safari na maisha ya wauzaji dawa,

3. Kwa kuwa tatizo la dawa za kulevya linaathiri jamii za watanzania ilikuwa ni wajibu wa polisi kushauri vita hii ifanywe kitaifa ili kumonitor mienendo ya wauzaji MADAWA ya kulevya,

4. Nisingeshauri kuanza kukamata baadhi ya wakazi na wasanii bila kuwakuta na mzigo - mipango ya kuwatia hatiani wakiwa na dawa za kulevya mahakamani tungetembea kifua mbele zaidi ya kwenda kushindwa kesi hizo dhidi yao,

5. Kitengo hicho wakati mwingine ilipaswa iwapo ni butu kibadirishwe na askari wa awali kuhamishiwa interior district ili wasiambukize wapya hulka ya KUPENDA utajiri wa haraka hivyo,

6. Afande Ernest Mangu namtakia mafanikio ktk vita hii.
 
Back
Top Bottom