Sheria ya kuwakata 15% wadaiwa bodi ya mikopo elimu yasainiwa

Ungeandika kumshukuru Mungu umezaliwa kwenye ukoo wa wenye nazo. Sisi maskini tungelipiwa na nani? Hata leo hii wakiweka sharti la mkopo ni 75% ya mshahara maskini hana chaguo
Huyo ni kama Marie Antoinette.Mkuu achana naye
 
Taarifa inayosambaa mitandaoni kuhusu kusainiwa kwa mswada unaohusu bodi ya mikopo ni uzushi. Mswada hauzungumzii kuhusu makato ya asilimia 15% kama inavyo trend kwenye media. Na mswada bado huko bungeni huajasainiwa na raisi kuwa sheria.
ingia kwenye website ya bunge utakubaliana na mimi, link hii hapa chini
Bunge Polis
NB: LABDA KAMA KUNA MSWADA MWINGINE TOFAUTI NA HUU ULIOSAINIWA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI TAREHE 13/10/2016
Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria zifuatazo
1: Sheria ya Mikopo,Misaada na Dhamana, Sura ya 134;
2:Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Sura ya 178;
3:Kodi ya Mapato, Sura ya 332;
4: Sheria ya Ardhi, Sura ya 113;
5:Sheria ya Barabara na Tozo za Mafuta, Sura ya 220 na
6:Sheria ya Tasnia ya Sukari, Sura ya 251
7:Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura ya 283.

Aidha katika kipengele kinachohusu sheria ya mikopo mswada unapendekeza marekebisho katika Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Sura ya 178. Marekebisho haya yanakusuidia kuruhusu wanafunzi wa stashahada na stashahada ya uzamili(diploma or higher diploma) katika fani ambayo Waziri ataamua ili kupata mikopo inayotolewa kwa wanafunzi wa elimuya juu kwa kuzingatia vipaumbele vyaTaifa.
upload_2016-12-1_12-23-38-png.441667


upload_2016-12-1_12-24-42-png.441669


"NAWASHAURI WATANZANIA HASA VIJANA TUSIAMINI SANA MITANDAO, WAKATI MWINGINE INATUMIKA VIBAYA KUPOTOSHA. TUJENGE UTAMADUNI WA KUPROVE MAMBO KABLA YA KUYAAMINI"
I regret to say u may be highly misinformed, hii ishu ya 15% tumeiona kwenye daily news na citizen
Huko Bunge waupdate tu website yao...
 
Hiii kitu imekaaa vibaya sana yani watu kibao hawalipi waliohama kikazi au majina hayafanani unakuta mtu bodi wameandika jina lake nala ukoo then mwajiri kaandika jina la baba hawalipi sasa usmart wao uko wapi hasa serikalini watu kibao hawalipi. Kama inakuwa hivi afu wao wanaona solution ni kutuongezea makato waziri husika ashughulike na hii issue duh shida nabaki na hela ya usafiri kwenda kazini
 
Tumekua mazombi wallahi....kweli naona tunaanza kuishi kama shetani...
15% loans board
10% nssf,ppf na wengineo
+
PAYE ...zaidi ya asilimia 30 inaishia juu kwa juu..bado rejesho la VITS ulokopa kazini..bado VICOBA...tumekoma baba
 
Siipendi hii serikali inatueletea mateso makubwa.Halafu anasema amechaguliwa na mungu na tumuombee! hivi ni mungu gani katili hivi?
Mmmmmmmm!!!! Oooooh MUNGU uliye Mkuu kuliko miungu yote, tunakuomba utusaidie.

Naomba wote tutubu na kufunga. MUNGU atatusikia tu.
 
Back
Top Bottom