Sheria ya kuwakata 15% wadaiwa bodi ya mikopo elimu yasainiwa


mzee wa giningi

mzee wa giningi

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Messages
520
Likes
334
Points
80
Age
50
mzee wa giningi

mzee wa giningi

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2016
520 334 80
magufuli-jpg.442059


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli tayari amekwishasaini mabadiliko ya sheria yanayomtaka mwajiri kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu kwa ajili ya kulipa deni lake analodaiwa na Bodi ya Mikopo.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, ambapo amesema kuwa makato kkiwango hicho kimepanda kutoka asilimia 8 ya sasa.

Akijibu maswali ya wananchi kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoendeshwa kupitia mtandao facebook wa East Africa Television, Naibu Waziri Manyanya amesema sheria hiyo tayari imesiniwa na siku za hivi karibuni itaanza kutumika.

"Hii asilimia 15, kimsingi sheria ninavyofahamu ilishasainiwa, baada ya hapo kuna kuiangalia iendane na kanuni zetu, baada ya kuicheki imeendana na kanuni zetu kama kuna sehemu itahitaji kuboreshwa kidogo haitazidi miezi miwili au mitatu, baada ya hapo tutaweza kutumia hiyo 15%, na asilimia 15 ya safari hii ni tofauti na siku za nyuma, siku za nyuma tulikuwa tunachaji asilimia 8”, amesema Manyanya.


Hapo awali wadaiwa hao wa mikopo walikuwa wanakatwa asilimia 8, lakini sheria ya sasa itaruhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kukatwa asilimia 15 ya kipato chao.

Pia Manyanya amesisitiza kuwa kwa wale ambao hawajaajiriiwa, lakini wanafanya biashara zao wanatakiwa kuwasilisha angalau shilingi 120,000 kila mwezi na kuwashauri kuwa ni vema wakapeleka zaidi ili wamalize haraka madeni yao.

Kuhusu wasio na kazi, amesema haiwezekani mtu asome halafu akose shughuli ya kufanya na kuwataka kutafuta shughuli yoyote ya kufanya ili waanze mapema kulipa madeni yao ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu masomo.


Chanzo: EATV
 
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Messages
9,257
Likes
1,966
Points
280
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined May 1, 2009
9,257 1,966 280
hili jipu jingine, kwa mshahara gani?
 
M

mtoto wa maskini

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Messages
1,153
Likes
553
Points
280
M

mtoto wa maskini

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2013
1,153 553 280
Yani source yako facebook?
 
jme

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Messages
4,207
Likes
1,551
Points
280
jme

jme

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2013
4,207 1,551 280
Ivi hii ndo serikali inayojinasibu kuwa ni ya wanyonge
 
Daz denny

Daz denny

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2016
Messages
392
Likes
376
Points
80
Daz denny

Daz denny

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2016
392 376 80
""Daah aisseh! its xo sad news!
 

Forum statistics

Threads 1,274,090
Members 490,586
Posts 30,500,708