Sheria ya "kufuta Kodi" ni kitanzi kwa Dkt. Mwigulu na Serikali yangu ya CCM




Sikiliza kodi ambazo mchina anataka afutiwe ili ajenge hiyo bandari; sasa unadhani itawezekana vipi bila ya waziri kuwa na mamlaka ya kufanya ivyo.

Huyu mama ni tatizo I am telling you amezungukwa na mafisadi ambao wanamuhakikishia miaka 10 bila ya kujua na wao wana agenda zao.

Acha kubeti wewe ,Toka kwny kivuli cha Hayati mwendazake uishi kwa amani.
 
Acha kubeti wewe ,Toka kwny kivuli cha Hayati mwendazake uishi kwa amani.
I am at peace and realistic.

Kwanza siwezi kumuabudu binadamu, ata huyo Magufuli nilikuwa namkosoa. Pili siwezi kuishi kwenye kivuli cha mtu especially a decesead individual.

People come and go; ideas live on.
 
Ungendelea kuwa wakala wa kuuza kadi za Chadema,ubongo wako sio wa hoja
Naona maccm mnaparuana. Haya mkimaliza mtuite tuje tuwajengee hoja. Kwa sasa acha tuangalie huu mtanange wenu unaoelekea kutuvutia watazamaji!
 
Hii mjue atakayekuwa anafuta ni raisi na waziri atakua rub stamp tu, but why ssh why madame?!
 
Labda aanze kwa kusamehe paye ndo ntajua wana Nia njema kweli
 
Ndugu zangu nimeuona muswada unaompa Waziri wa fedha nguvu ya kufuta kodi mbalimbali atakapoona inafaa. Ikumbukwe hili lilikuwepo miaka ya huko nyuma lakini lilirudishwa kwenye baraza la mawaziri baada ya mawaziri aidha kwa kuchomekewa au kwa makusudi kuitumia bila kuwa na tija kwa taifa; Baadhi ya Mawaziri wa fedha waliowahi kukumbwa na kadhia ya nguvu waliopewa na sheria hii ni kama ifuatavyo; Prof.Mbilinyi (enzi za Mkapa) Kilonsi Mpologonyi (alikuwa naibu wa wizara ya fedha enzi za Mkapa) Daniel Yona na Basil Mramba hawa walikuwa mawaziri wa fedha nyakati tofauti enzi za Mkapa (Yona aliwahi kuwa waziri wa madini pia).Ikumbukwe hawa wazee walienda jela kutokana na nguvu hizi. Kwa uchache, sheria hii ya kumpa waziri wa fedha mamlaka ya kusamehe kodi inachochea rushwa na ufisadi wa hali ya juu kwani wanufaika wa sheria hii ni wajanja wajanja na mara zote misamaha hii haina tija kwa taifa. Ninashauri Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni raisi libaki na jukumu hili. Kama hili litapita litakuwa shimo la kisiasa kwa Mwigulu Nchemba kwani wabaya wake watatatumia sheria hii kumtega na kummaliza kisiasa na haitaishia kwake, CCM watakuwa na mzigo wa kujisafisha nalo.

Hivi ulielewa kauli ya mwendazake ya "wapinzani wanatuchelewesha kuleta maendeleo? hadi akafikia kusema kuwa tusimchanganyie betri na magunzi? Hii ndiyo ilikuwa maana yake ili waweze kupitisha sheria zao za hovyo
 
Ndugu yangu wee, hii nchi watu kama hao hawaendi jela. Wezi wa kuku ndiyo wanaenda. Halafu huyo jamaa ni timu ''wajanja wajanja''. Hakuna kiongozi hapo.

Hakuna marefu yasikyokuwa na nchi anaweza kuja kutokea kiongozi akaja kuibua makando kando yake na akawekwa ndani,abaya alifanya ufirauni utwala wa jiwe bila kuguswa lakini mambo yanabadilika sio kila homa ni malaria ,sasa yupo kisonjo analala mchongoma.
 
Endelea kulala hujui unachoongea
Hivi ulielewa kauli ya mwendazake ya "wapinzani wanatuchelewesha kuleta maendeleo? hadi akafikia kusema kuwa tusimchanganyie betri na magunzi? Hii ndiyo ilikuwa maana yake ili waweze kupitisha sheria zao za hovyo
 
Hizi ni miongoni mwa sheria maalum kwa ajili ya kukusanya pesa kwa ajili ya chaguzi kwa chama tawala.

Safari Bado ni ndefu Sana.
 
Ndugu zangu nimeuona muswada unaompa Waziri wa fedha nguvu ya kufuta kodi mbalimbali atakapoona inafaa. Ikumbukwe hili lilikuwepo miaka ya huko nyuma lakini lilirudishwa kwenye baraza la mawaziri baada ya mawaziri aidha kwa kuchomekewa au kwa makusudi kuitumia bila kuwa na tija kwa taifa;

Baadhi ya Mawaziri wa fedha waliowahi kukumbwa na kadhia ya nguvu waliopewa na sheria hii ni kama ifuatavyo;

Prof.Mbilinyi (enzi za Mkapa)
Kilonsi Mpologonyi (alikuwa naibu wa wizara ya fedha enzi za Mkapa)

Daniel Yona na Basil Mramba hawa walikuwa mawaziri wa fedha nyakati tofauti enzi za Mkapa (Yona aliwahi kuwa waziri wa madini pia).Ikumbukwe hawa wazee walienda jela kutokana na nguvu hizi.

Kwa uchache, sheria hii ya kumpa waziri wa fedha mamlaka ya kusamehe kodi inachochea rushwa na ufisadi wa hali ya juu kwani wanufaika wa sheria hii ni wajanja wajanja na mara zote misamaha hii haina tija kwa taifa.

Ninashauri Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni raisi libaki na jukumu hili.

Kama hili litapita litakuwa shimo la kisiasa kwa Mwigulu Nchemba kwani wabaya wake watatatumia sheria hii kumtega na kummaliza kisiasa na haitaishia kwake, CCM watakuwa na mzigo wa kujisafisha nalo.
Ni kweli ilifaa kama Kuna kodi anataka kufuta ipelekwe Baraza la mawaziri kwa approval japo ndo hivyo urasimu utaongezeka.

Au kuwe na japo la kupendekeza kufutwa afu Waziri atangaze
 
Huenda wana nia njema.

Sasa kama matharani hayakusanyiki labda imethibitika kuwa bad debts wasiyafute?
Au haiwezekani kukusanyika kwa sababu moja ama nyingine yatabaki hivyo kwa miaka mingapi?

Sema umakini inahitajika.
 
Tusubiri
Huenda wana nia njema.

Sasa kama matharani hayakusanyiki labda imethibitika kuwa bad debts wasiyafute?
Au haiwezekani kukusanyika kwa sababu moja ama nyingine yatabaki hivyo kwa miaka mingapi?

Sema umakini inahitajika.
 
Back
Top Bottom