Sheria ya "kufuta Kodi" ni kitanzi kwa Dkt. Mwigulu na Serikali yangu ya CCM

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu nimeuona muswada unaompa Waziri wa fedha nguvu ya kufuta kodi mbalimbali atakapoona inafaa. Ikumbukwe hili lilikuwepo miaka ya huko nyuma lakini lilirudishwa kwenye baraza la mawaziri baada ya mawaziri aidha kwa kuchomekewa au kwa makusudi kuitumia bila kuwa na tija kwa taifa;

Baadhi ya Mawaziri wa fedha waliowahi kukumbwa na kadhia ya nguvu waliopewa na sheria hii ni kama ifuatavyo;

Prof. Mbilinyi (enzi za Mkapa) Kilonsi Mpologonyi (alikuwa naibu wa wizara ya fedha enzi za Mkapa)

Daniel Yona na Basil Mramba hawa walikuwa mawaziri wa fedha nyakati tofauti enzi za Mkapa (Yona aliwahi kuwa waziri wa madini pia).Ikumbukwe hawa wazee walienda jela kutokana na nguvu hizi.

Kwa uchache, sheria hii ya kumpa waziri wa fedha mamlaka ya kusamehe kodi inachochea rushwa na ufisadi wa hali ya juu kwani wanufaika wa sheria hii ni wajanja wajanja na mara zote misamaha hii haina tija kwa taifa.

Ninashauri Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni raisi libaki na jukumu hili.

Kama hili litapita litakuwa shimo la kisiasa kwa Mwigulu Nchemba kwani wabaya wake watatatumia sheria hii kumtega na kummaliza kisiasa na haitaishia kwake, CCM watakuwa na mzigo wa kujisafisha nalo.
 
Bunge limefikia hatua ya kukubali kuentertain miswada ya namna hiyo sababu ya consequences za tamaa kutaka kuweka bunge, mahakama na serikali kiganjani kwake.

Bunge limejaa watu wasioelewa Taifa limetoka wapi.

Acha wapitishe hiyo sheria, lakini Mwiguru ajiandae kwenda kufagia hospitali ya sinza kama mramba.
 
Siyo wabaya wake tu bali hata yeye mwenyewe. Jamaa alivyo na tamaa ya madaraka na mali ataacha kula cha juu ili atoe msamaha kwa ''wajanja''? Ila yote tisa, kumi katiba mpya inatakiwa ili kuondoa ujinga kama huu.
 
Yaani Mwigulu apewe mamlaka ya kufuta Kodi? atakula sana 10% na wanufaika watakuwa ni wale wajanja wajanja tu
 
Kama hili litapita litakuwa shimo la kisiasa kwa Mwigulu Nchemba kwani wabaya wake watatatumia sheria hii kumtega na kummaliza kisiasa na haitaishia kwake, CCM watakuwa na
Naiona hatari kubwa ipo kwa Mwigulu. CCM wako vizuri sana ktk kuukwepa ubaya na kumvika waziri husika.
 



Sikiliza kodi ambazo mchina anataka afutiwe ili ajenge hiyo bandari; sasa unadhani itawezekana vipi bila ya waziri kuwa na mamlaka ya kufanya ivyo.
 
Back
Top Bottom