Sheria ya kuanzisha Serikali ya Mseto Zanzibar kujadiliwa leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya kuanzisha Serikali ya Mseto Zanzibar kujadiliwa leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 23, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Baraza la Wawakilishi Zanzibar linaanza mkutano wake leo ambapo pamoja na mambo mengine litajadili muswada wa kihistoria wa sheria ya kuanzishwa kwa serikali ya Mseto.

  Idadi kubwa ya wakazi wa Zanzibar wakiwamo wanachama wa CCM na CUF, wasomi na wanasheria mbalimbali wameendelea kusisitiza kuwa kuupigia kura za maoni muswada huo ni kupoteza fedha na muda kwa kuwa tayari Baraza la Wawakilishi lilishatoa uamuzi kwa niaba ya Wanzibari.

  Je nini maoni yako kuhusu kupigiwa au kutopigiwa kura ya maoni kwa huo muswada
  Je kama BLW likiamua kutopigiwa kura ya maoni litaonekanje kwa baadhi ya viongozi hasa wa Ccm bara wanaodai kura ya maoni kabla ya kuundwa kwa serikali ya mseto.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  Luteni, nadhani wanajadili kesho na sio leo. Naangalia kama nitapata nafasi, nitadamkia barazani na kuwapasha mjadala utakavyokuwa. Kama kweli ni leo, basi nimeshachemsha!.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  Luteni, kwa uhakika kikao cha BLW kinaanza kesho na ajenda ya kwanza ilikuwa ni kujadili muswada wa kura za maoni. Taarifa kutoka Zenj, kesho kikao kinaanza ila mjadala wa kura ya maoni sio kesho.
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,740
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mabadiliko ya katiba lazima yawahusishe watu,kwa tafsiri halisi,wawakilishi mamlaka yao yanaishia kutoa maamuzi kwa yale mambo ambayo sheria inaelekeza.Lakini kutungwa kwa kipengele cha sheria ambacho hapo awali hakikuwepo,na hasa mabadiliko ya katiba ,umma lazima ushirikishwe kikamilifu.Huo ndo uwakilishi makini.
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Mayenga, huo ushilikishwaji ni lazima uwe referendum? Katiba zetu zina viraka vingi tu, lakini sikumbuki kama kuna kura ya maoni iliwahi kupitishwa ili kupata maoni ya watz/zanzibari kwa kila mabadiliko yaliyofanywa kwenye katiba hizo. Mambo ya muungano ni mfano mmojawapo.
   
 6. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pasco tupe habari za kinachoendelea
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimekupata mkuu nini mawazo yako kuhusu referendum
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  .Ilikuwa nitie timu huko leo ili kesho niamkie barazani, lakini mjadala wa kura ya maoni sio kesho, nimeahirisha mpaka nitakapojuzwa ni lini.Interest yangu kubwa kwa Wazanzibari kuhusu hii kura ya maoni kwa kitendo cha SMZ kuivalia njuga hayo maoni kuruhusu serikali ya umoja wa kitaifa.Katiba ya Zanzibar inamruhusu rais kuteua yoyote kuwa waziri, sio lazima atoke chama chake, kwa maoni yangu, hii kura ya maoni ni wastage of time and resources wakati ni wazi itapita kwa asilimia 100.Kitu cha kushangaza ni issues muhimu, nyeti na zinazogusa sovereinity ya Zanzibar kama nchi, zimeachwa zikipita juu kwa juu, bila hata kuwauliza Wanzazibari ama kura za maoni, ukiwemo muungano na mpaka leo wanaishia kupiga kelele na kulalama kutwa kucha, wamepata nafasi ya kura ya maoni, wanauliza swali moja tuu la kujibu ndiyo au hapana!. Hiki ni kichekesho!.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  Luteni, referendum ni kitu kizuri kufanyika kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu mustakabali wa taifa lolote. Binafsi suala ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar halikuhitaji referendum, kama jambo kubwa kama kuupoteza utaifa wa Zanzibar na kujiingiza kwenye muungano, limefanyika bila referendum, hiyo serikali ya mseto/umoja wa kitaifa is nothing!.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Naamini kabisa kuna kitu ambacho hatujaambiwa ambacho ndicho hasa kinachotafutwa na haya tunayoyaona ni kama kanyabwoya tu. many time will tell
   
 11. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kitu kama kipi Mkuu!!!!?
  Kuvunjwa Muungano?
  Kuanzishwa Serikali tatu?
  Au Serikali moja?
  Sema nini wasi wasi wako mkuu??
   
 12. C

  Calipso JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mbona kuna mambo mengi tu wananchi hawajashirikishwa? umesahau suala makamo wa rais lilivoondolewa? na mengi tu yapo.. lkn kwa sababu ya wapinzani kuingia kwenye madaraka,ndio vitatokea vijisababu vingi...
   
 13. T

  Tall JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kura ya maoni ni muhimu.
   
Loading...