Sheria ya kelele: NEMC yatangaza rasmi kiama kwa wachafuzi wa kelele kwenye makazi ya watu

D

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Messages
4,578
Points
2,000
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2014
4,578 2,000
1-jpg.1147743

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeagiza wamiliki wote wa kumbi za starehe, baa pamoja na nyumba za ibada kuhakikisha wanadhibiti uchafuzi wa kelele katika maeneo ambayo ni makazi ya watu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka alisema NEMC imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi sehemu mbalimbali nchini kutokana na kushamiri kwa kelele na mitetemo chafuzi. “Tumepokea malalamiko kutoka kwa wananchi mbalimbali juu ya kelele na mitetemo chafuzi zinazotoka katika maeneo ya Kumbi za starehe, baa pamoja na nyumba za ibada,” alisema Dk Gwamaka.

Dk Gwamaka alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake zinakataza uwepo wa kelele na mitetemo chafuzi. Sheria na kanuni hizo zinakataza uwepo wa kelele na mitetemo chafuzi, hivyo ni vyema shughuli hizo zikaendeshwa katika maeneo yaliyorasimishwa au katika majengo yaliyojengwa katika muundo wa kudhibiti sauti zisitoke nje na kuwa kero kwa wananchi wa eneo husika, alisisitiza Dk Gwamaka.

Hata hivyo NEMC imebaini kuwa tatizo hilo limechangiwa na kumbi hizo, baa pamoja na nyumba za ibada kujengwa kwenye makazi ya watu. “Katika utafiti wetu, tumegundua kuwa tatizo hilo kwa kiasi kikubwa limechangiwa na ujenzi holela usiofuata sheria ya mipango miji hali ambayo ni rahisi sana kukuta viwanda, nyumba za kuabudia na kumbi za starehe katika makazi ya watu,” alifafanua Dk Gwamaka.

Agizo hilo limeungwa mkono na baadhi ya wananchi waliozungumza kwa nyakati tofauti kuonyesha kukerwa na uchafuzi huo wa kelele katika maeneo ya makazi hususani kwa nyakati za usiku. “Binafsi naunga mkono tamko hili la NEMC kwa kuwa limekuja katika wakati ambao linauhitaji kwa wananchi kwani tumekuwa tukiathirika na uchafuzi wa kelele hususani kwa mikesha ya miziki na ibada zinazofanyika katika maeneo ya wazi ambayo pia ni makazi ya watu, alisema Yasini Mbalami mkazi wa Mbagala Kuu.

Mohammed Twaha ambaye ni mkazi wa Kigamboni kwa upande wake licha ya kupongeza tamko hilo la NEMC, alisema kuwa limechelewa kutolewa kwani maeneo mengi yamekuwa yakiathirika na kelele hizo zinazotokana na ala za muziki kutoka kwenye kumbi za starehe. Huku mitaani hali ni mbaya, kumbi za starehe na wakati mwingine ni maeneo ya wazi imekuwa ni wazalishaji wakubwa wa uchafuzi wa kelele hali inayotufanya tushindwe kulala vizuri hasa kwa wakati wa usiku, alisema.

NEMC imefanunua kuwa tamko hilo halihusu ibada fupi kama vile adhana misikitini, kengele za kanisani ambazo huita waumini kwenda kufanya ibada za muda mfupi.
 
walitola

walitola

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2014
Messages
2,491
Points
2,000
walitola

walitola

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2014
2,491 2,000
Dah nakumbuka nyumbani ikifika jpili tulikuwa tunaondoka kabisa mana nyuma ya nyumba yetu kuna kanisa la kilokole yani makelele yake kwa kweli ni kero kubwa sana afadhali hii sheria itasaidia sana
 
J C

J C

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2013
Messages
2,284
Points
2,000
J C

J C

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2013
2,284 2,000
Kumbuka sio makanisa tu hata harusi, komuniyo,kipaimara,ibada za Iddi,birthdays hawa hutumia subwoofer au kingine chochote kile kinachotoa sauti inayovuka uzio wa Nyumba yako na kuwafikiwa wengine. Sheria hukata kote. Wazungu ndio wamechemka amjasikia wale walioenda mahakamani kwa kuwika kwa jogoo. Kama tumeshindwa kuvumiliana ulimwengu utajaa wazimu. Tulivyo wajinga tunaona makanisa tu hatujui hata ma subwoofer ya kichina nayo yanasababisha noise pollution.
 
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Messages
4,578
Points
2,000
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2014
4,578 2,000
Dah nakumbuka nyumbani ikifika jpili tulikuwa tunaondoka kabisa mana nyuma ya nyumba yetu kuna kanisa la kilokole yani makelele yake kwa kweli ni kero kubwa sana afadhali hii sheria itasaidia sana
huenda ikawa nguvu ya soda! lakini kama na viongozi wengine wakilitolea tamko itaongeza nguvu ya polisi kuwakamata
 
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Messages
4,578
Points
2,000
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2014
4,578 2,000
Kumbuka sio makanisa tu hata harusi, komuniyo,kipaimara,ibada za Iddi,birthdays hawa hutumia subwoofer au kingine chochote kile kinachotoa sauti inayovuka uzio wa Nyumba yako na kuwafikiwa wengine. Sheria hukata kote. Wazungu ndio wamechemka amjasikia wale walioenda mahakamani kwa kuwika kwa jogoo. Kama tumeshindwa kuvumiliana ulimwengu utajaa wazimu. Tulivyo wajinga tunaona makanisa tu hatujui hata ma subwoofer ya kichina nayo yanasababisha noise pollution.
sheria inagusa kote; vigodoro, sherehe, miziki mikubwa na milipuko kama ya sherehe za wahindi na ile ya miamba katika makazi ya watu ni marufuku!
 
J C

J C

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2013
Messages
2,284
Points
2,000
J C

J C

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2013
2,284 2,000
Mk
sheria inagusa kote; vigodoro, sherehe, miziki mikubwa na milipuko kama ya sherehe za wahindi na ile ya miamba katika makazi ya watu ni marufuku!
Mkuu ondoa Neno mikubwa. Weka hivi sauti yoyote inayovuka mipaka yako ya umiliki na kwenda kwa Jirani. Nadhani wataalamu wa sheria wanafahamu hili kuna neno la kisheria nadhani ni nuisance. Hata kuwasha moshi ukavuka na kusambaa kwa Nyumba za Jirani au mti wako kuotea na kuvuka mpaka matawi yake ni kosa. Yaani hapa ni patamu hasa. Tutaheshimiana tu. We Liza li subwoofer lako au music system yako tunakula kichwa milioni kumi fasts na fidia juu. Kesi zitajaa haswaa mahakamani na wengi watafungwa sio bure. Ustarabu una wazimu wake. Ila kikubwa tungevumiliana tu.
 
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Messages
4,578
Points
2,000
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2014
4,578 2,000
Mk

Mkuu ondoa Neno mikubwa. Weka hivi sauti yoyote inayovuka mipaka yako ya umiliki na kwenda kwa Jirani. Nadhani wataalamu wa sheria wanafahamu hili kuna neno la kisheria nadhani ni nuisance. Hata kuwasha moshi ukavuka na kusambaa kwa Nyumba za Jirani au mti wako kuotea na kuvuka mpaka matawi yake ni kosa. Yaani hapa ni patamu hasa. Tutaheshimiana tu. We Liza li subwoofer lako au music system yako tunakula kichwa milioni kumi fasts na fidia juu. Kesi zitajaa haswaa mahakamani na wengi watafungwa sio bure. Ustarabu una wazimu wake. Ila kikubwa tungevumiliana tu.
kwa kuanzia sheria na kanuni hizi zimetaja kutogusa ibada fupi kama zile za azana ambazo ni za dakika 1 hadi 5
 
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
38,540
Points
2,000
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
38,540 2,000
Kumbuka sio makanisa tu hata harusi, komuniyo,kipaimara,ibada za Iddi,birthdays hawa hutumia subwoofer au kingine chochote kile kinachotoa sauti inayovuka uzio wa Nyumba yako na kuwafikiwa wengine. Sheria hukata kote. Wazungu ndio wamechemka amjasikia wale walioenda mahakamani kwa kuwika kwa jogoo. Kama tumeshindwa kuvumiliana ulimwengu utajaa wazimu. Tulivyo wajinga tunaona makanisa tu hatujui hata ma subwoofer ya kichina nayo yanasababisha noise pollution.
Kula like mkuu
 
J C

J C

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2013
Messages
2,284
Points
2,000
J C

J C

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2013
2,284 2,000
kwa kuanzia sheria na kanuni hizi zimetaja kutogusa ibada fupi kama zile za azana ambazo ni za dakika 1 hadi 5
Tutakata rufaa kelele ni kelele tu haijalishi muda. Hiyo ni ibada na wakristo nao ni ibada yao kuwa fupi wamependa na ni maaagizo ya msahafu wao nasi kuwa ndefu ni kwa mujibu wa msahafu wetu hivyo tuheshimiane kila mmoja asikike within his boundaries and not out. Msilete mambo ya ajabu hapa. Yaani tunahitaji sauti za ndege tu mitaañi migari au miboda boda inayotoa sauti mbaya mbaya tupe kule ikiwemo na adhana.
 
J C

J C

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2013
Messages
2,284
Points
2,000
J C

J C

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2013
2,284 2,000
As
Kula like mkuu
Asante Mjumbe. Unajua kuna life style tunaiga za kishenzy sana. Tumeshindwa kuvumiliana sasa tunataka kujawa na wazimu wa kizungu. Afrika haiko hivi tunaishi kwa kuvumiliana sana na ndio utamaduni wetu sasa tukitaka kujawa na wazimu utakuwa wazimu kweli. Naona kanuni uchwala zinaanza kuwapendelea waislamu ati wako ni dakika 4 mpaka 5. Ni nani yuko ana interest na wanachokifanya?. Kama sio kuvumiliana tu.
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
40,628
Points
2,000
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
40,628 2,000
Ok.....

Ushambiwa ukatapo Pata taarifa hii mtaarifu na mwenziyooo.....

Ova
 
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Messages
4,578
Points
2,000
D

dmkali

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2014
4,578 2,000
As

Asante Mjumbe. Unajua kuna life style tunaiga za kishenzy sana. Tumeshindwa kuvumiliana sasa tunataka kujawa na wazimu wa kizungu. Afrika haiko hivi tunaishi kwa kuvumiliana sana na ndio utamaduni wetu sasa tukitaka kujawa na wazimu utakuwa wazimu kweli. Naona kanuni uchwala zinaanza kuwapendelea waislamu ati wako ni dakika 4 mpaka 5. Ni nani yuko ana interest na wanachokifanya?. Kama sio kuvumiliana tu.
acha ujinga! mtu akupigie vuvuzela masikioni halafu useme kuvumiliana, MTU afunge spika usiku kucha halafu useme uafrika kuvumiliana; kwanza waafrika tul8shi msituni hakukuwa na sabufa wala disco
 
MzaramoTz

MzaramoTz

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2017
Messages
807
Points
1,000
MzaramoTz

MzaramoTz

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2017
807 1,000
Mie mpaka nimeshasahau kuwa tupo episode ya ngapi na season gani naona zinaongozana kwa kasi tu yaani.
 
Forum statistics

Threads 1,316,455
Members 505,652
Posts 31,890,972
Top