Sheria ya Gharama za Uchaguzi yarudishwa Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Gharama za Uchaguzi yarudishwa Bungeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Apr 12, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Bunge la Tanzania ambalo linaanza mkutano wake wa 19 kesho mjini Dodoma limekubali kulirejesha suala hilo kwenye chombo cha kutunga sheria baada ya mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuwasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge kutaka Bunge lipitie upya sheria hiyo na kuifanyia marekebisho kabla ya kuanza kutumika.

  Bunge limefikia uamuzi huo ukiwa umebakia mwezi mmoja kabla ya mchakato wa uchaguzi mkuu kuanza kwenye ngazi ya vyama. Slaa aliwasilisha pendekezo hilo katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  "Kamati ya Uongozi ya Bunge ilikutana kupanga ratiba ya vikao vya bunge, lakini baadaye Dk Slaa, kama mjumbe, akawasilisha pendekezo hilo na sisi tukaona ni vyema suala hilo likapata ufafanuzi zaidi kwa kuwashirikisha wabunge wote," alisema spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta.

  "Tumeona katika sheria hii mambo mengi yako kinadharia, kwa mfano; sheria inasema kuwe na wajumbe wa kampeni wasiozidi 20 kwa mbunge na 10 kwa diwani na wagombea hao wawe wameidhinishwa na DASS au WEO.

  "Hili ni jambo jema, lakini tafsiri yake ni kwamba serikali sasa itakuwa na ruhusa ya kukubali au kukataa nani aingie kwenye kampeni hizo na nani asiingie; na kama hiyo ndiyo tafsiri, kimsingi inaleta shida."

  Spika Sitta alifafanua kuwa katika bunge hili, wabunge watazitazama tena kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo na kuzifanyia marekebisho.

  "Kama tatizo ni sheria itabidi ijadiliwe upya na kama tatizo ni kanuni, tutamtaka waziri mkuu aziboreshe."

  Alipoulizwa endapo kama suala hilo lijadiliwe bungeni katika mkutano unaoanza kesho, Spika Sitta alijibu: "Kwa nini isiwezekane?, Tumepanga kuwa na kikao cha siku nzima kuipitia sheria hiyo na kanuni."

  Kwa mujibu wa Spika Sitta, ikiwa katika kuangalia sheria na kanuni zake tatizo likaonekana kwenye kanuni, waziri mkuu ndiye mwenye wajibu wa kuzirekebisha, lakini kama tatizo litakuwa ni sheria yenyewe, lazima irudishwe na kujadiliwa upya.

  Awali, Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa amewasilisha mapendekezo hayo kutokana na kile alichodai kuwa Rais Kikwete amedanganywa na kusaini sheria hiyo kimakosa.
  Alisema aliamua kuliwasilisha suala hilo kwanza kwenye kamati ya uongozi ya Bunge ili kama angepuuzwa, alifikishe suala hilo bungeni mwenyewe kwa namna anayoona inafaa.

  "Mapambano ndio yameanza; mimi ni mjumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge na leo (jana) tulikuwa na kikao, nimehoji suala hilo kabla sijalifikisha bungeni kwa namna ambayo nitaona inafaa," alisema Dk Slaa.

  "Bado nasisitiza kuwa Mwanasheria Mkuu amedanganya kwa kusema vifungu hivyo viko sahihi kwa kuwa Ofisi ya (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera na Uratibu wa Bunge-, Phillip) Marmo ndio iliyovifanyia marekebisho. Ofisi ya Marmo haina mamlaka ya kubadili vifungu vya sheria iliyopitishwa na Bunge.

  "Lengo langu sio kumvunjia heshima Mwanasheria Mkuu na yeye anajua kuwa namheshimu sana, lakini lazima Watanzania tuone serikali yetu inafanya kazi kwa uwazi, ukweli na uwajibikaji," alisema.

  Alisisitiza kuwa kilichojadiliwa bungeni ni vikundi vya sanaa na Bunge liliagiza viingizwe vifungu vya ufafanuzi na sio mabadiliko ya vifungu.


  Chanzo: Gazeti la Mwananchi

  nani zaidi kati ya Marmo, Mwanasheria Mkuu, Slaa na aliyeisaini kwa mbwembwe
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  upuuzi tu.. tumewaambia sheria mbaya tangu mwanzo wakadhani tunawaonea wivu!!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi kinachonichekesha ni jinsi mwanakwetu mtoto wa Chalinze anapomwaga wino kwenye sheria ambayo kachomokea madubwana na yeye anachekelea tu...kweli Rais tunaye
   
 4. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tanzania tunaandamwa na hasara, tunapata hasara kupita kiasi. Sahihi hazina tena maana kwetu Tanzania. Sasa tunataka kuunda njia ipi mbadala ya kuidhinisha mambo? Maana Richmond nalo lilitiwa wino kama masihara! lol! Ee Mungu okoa nchi yangu Tanzania wape watu nguvu ya kutambua na kuamua kwa kura zao!
  Kwa sasa naweza kufanya hilo tu kwa nchi yangu Tanzania!
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sielewi ofisi ya mwanasheria mkuu inafanya nn, sielewi wizara ya sheria na katiba inafanya nn, sielewei kamati ya kusimamia uchaguzi inafanya nn.
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Teh teh teh Mkuu sio wivu tuuu bali ni ujinga na upompompo mwingi walio nao vichwani mwao, na hao walioko ikulu na ndio wanao mvisha aibu JK sijui mle IKULU kuna jinamizi gani ambalo halifukuziki ndilo linaiweka hata nchi yetu pabaya wele watendaji mle IKULU nao wakiwa smart hakuto tokea mauzembe sehemu zingine. pia tujaribu pia kuangaria serikali za wenzetu walio endelea katika uongozi wao ulivyo tengenezwa

   
 7. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Siku watu watakapoanza kuwajibika kwa sahihi zao ndo wataanza kuwa makini. Sasa hivi unaweza ku weka sahihi kwenye kitu chochote na kusiwe na lolote litakalotokea. Kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa makini kwani hakuna atakayeuliza kesho "kwa nini uliweka sahihi hapa?".

  Lakini siku zaja, na si mbali, hawa wanaotia sahihi bila kuuliza watakapotakiwa kutoa maelezo ya sahihi zao!
   
 8. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kila siku problem iko kwa Watendaji! Nadhani problem kubwa anayo yule anayewaajiri watendaji wa Ikulu na problem kubwa zaidi anayo huyo anayemwajiri anayewaajiri watendaji. Kila wakati Ikulu inaaibioshwa hata Mkuu wa nchi anaaibishwa, nadhani Rais wetu anajiaibisha pia maana anao uwezo wa kuwaajiri watendaji smart. Mbona wakati wa Mkapa Ikulu ilikuwa smart? Au Mkuu wa nchi aliwatimua wote na kuajiri upya?
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Ndio maana kazi ya ubunge ni dii kubwa Tanzania. Richmond ilichukua miaka mitatu na bado mpambano ukawa bila bila, EPA na aina za ufisadi mwingine pia. Sheria ya uchaguzi!!!
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  WASOMI na wanasiasa nchini wamesema kitendo cha kurejeshwa bungeni kwa sheria ya gharama za uchaguzi kwa lengo la kujadiliwa upya ni ishara kwamba serikali haipo makini na inafanya kazi kwa kukurupuka.

  Kurejeshwa bungeni kwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge mwezi Februari na kutiwa saini kwa mbwembwe Machi 17 mwaka huu na rais Jakaya Kikwete , kunafuatia hoja ya mbunge wa Karatu Dk Willbrod Slaa kuwasilisha mapendekezo katika Kamati ya Bunge ya Uongozi iliyokutana juzi jijini Dar es Salaam.

  Juzi Spika wa Bunge Samuel Sitta aliliambia gazeti hili kwamba sheria hiyo itarejeshwa bungeni kujadiliwa upya baada ya kugundua kasoro nyingi.

  Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jana, Profesa Abdallah Safari, Dk Sengondo Mvungi na Profesa Mwesiga Baregu walisema kuwa pamoja na mapungufu yaliyolalamikiwa na Dk Slaa, sheria hiyo haina jipya na imejaa mapungufu.

  Profesa Safari alifananisha sheria hiyo kuwa ni sawa na kumweka farasi nyuma ya mkokoteni ili ausukume badala ya kumweka mbele ili auvute.

  Alisema mbali na mapungufu yaliobainishwa na Dk Slaa pia sheria hiyo imejaa utata na kwamba ipo kwa ajili ya kukadamiza wapinzani.

  "Hatua ya Bunge kuridhia kurejeshwa kwa sheria hiyo kujadiliwa upya Bungeni ni ishara ya serikali kutokuwa makini na kukurupuka katika utendaji wake ambao mara nyingi inazingatia kuwaridhisha watu fulani.

  "Hii sheria itaendelea kukosolewa tu kwa kuwa haikidhi vigezo vya sheria za kimataifa kama vile tamko la dunia kuhusu haki za binadamu na sheria ya kimataifa kuhusu haki za kisiasa na kiraia," alisema Profesa Safari

  Profesa Safari alifafanua kwamba athari za sheria hiyo ya gharama za uchaguzi zinaweza kuonekana zaidi katika sheria nyingine za uchaguzi ikiwemo Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Uchaguzi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Aliongeza kwamba athari hiyo pia zinaonekana kupitia ripoti mbili maarufu za tume ya Jaji Nyalali ya mwaka 1992 na ile ya Jaji Kisanga ya mwaka 1998.

  Alisema Sheria ya Gharama za Uchaguzi yenye vifungu 32 ambayo ni fupi ikilinganishwa na sheria nyingine nchini ina mapungufu katika vifungu kadhaa ambavyo alivikosoa.

  Alivitaja vifungu vyenye mapungufu kuwa ni kifungu cha 8 (1) na (2), kifungu cha 9 (1),(2),(3), kifungu cha 11(4), 12, 13 na kifungu cha 15 (1)na (2).

  "Moja ya madhumuni ya sheria hii ni kuweka utaratibu utakaowesha serikali kuchangia gharama za kampeni na uchaguzi kwa vyama vya siasa, kifungu cha 32 kimefanya nyingeza kidogo tu katika kifungu cha 13 (2) cha sheria ya vyama vya siasa.

  Hivyo hakuna utaratibu mpya wa serikali kuchangia gharama za uchaguzi zaidi ya ule ulioainishwa na vifungu vya 13 (1), 16 na 17 ya sheria ya vyama vya siasa," alifafanua Safari.

  Naye Dk Sengondo Mvungi alisema matatizo hayo yanatokana na kutofuatwa kwa katiba ya nchi.

  “Utawala bora wa sheria hatufuati kabisa, hatumo katika nchi zinazofuata utawala bora, tumeingia kwenye mtaro moja kwa moja,”alisema Dk Mvungi na kuongeza:

  "Katiba inaeleza juu ya kutunga sheria, lakini sasa inashangaza sana kuwepo na makosa kwenye kitu muhimu kama sheria ya uchaguzi."

  Alifafanua kuwa makosa yaliyojitokeza yalitakiwa yafanyiwe kazi nje ya bunge na kurekebishwa kama marejeo ya sheria hiyo.

  Kwa upande wake Profesa Mwesiga Baregu alisema rais Jakaya Kikwete alisaini Sheria ya Udhibiti Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi kwa mbwembwe akilenga kuwaonyesha nchi wahisani kuwa anaongoza kwa kupambana na rushwa nchini.

  Alisema pia rais alisaini sheria hiyo ili kuwaonyesha wananchi kuwa ametimiza ahadi aliyoahidi mwaka 2005 alipoingia madarakani.

  "Hii ni dalili ya kukosa umakini kwa serikali na Bunge, kwa sheria iliyopitishwa na Bunge na kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania ikasainiwa kwa mbwembwe katika viwanja vya Ikulu, kuhudhuriwa na mabalozi kurudishwa tena bungeni ikiwa haijaanza hata kutumika!

  "Rais Kikwete alitaka kujionyesha kwa mabalozi kuwa ni makini katika kupamba na rushwa na kuwaambia wananchi kuwa anachoahidi anatekeleza," alisema Profesa Baregu.

  Profesa Baregu alieleza kuwa kurudishwa bungeni kwa sheria hiyo ni funzo kwa serikali na Bunge na kwamba iache kufanya mambo yenye maslahi kwa taifa kwa pupa na bila umakini.

  “Hii ni aibu sana, kama ingekuwa nchi nyingine iliyoendelea, vyama vya upinzani vingeshinikiza rais ajiuzulu. Lakini kwa sababu hapa kwetu ndiyo chama hiki kimoja tuu kikubwa hali inakuwa tofauti,” alisema Profesa Baregu.

  Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashid alisema kuwa mjadala huo unarudi bungeni kwa kuwa Dk Slaa hakuridhika na majibu ya mwanasheria mkuu wa serikali.

  “Dk Slaa aliniambia hiyo ni moja ya mambo ambayo atataka ufafanuzi wa kina, sitaki nimsemee sana lakini ni hoja ya msingi,” alisema Rashid.

  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kuwa sheria hiyo pamoja na kuamuliwa kurudishwa bungeni, ni vigumu kutekelezeka kwa kuwa ina makosa mengi na imetungwa kwa maslahi ya watu binafsi.

  Alisema kuwa wataalamu wamefanya kazi sio kwa utaalamu wao bali kwa kutumwa na kufuata maagizo ya wenye maslahi yao.

  “Tulisema wataalamu waachiwe wafanye kazi yao, lakini muda walioutumia wa miezi miwili haukutosha na ndiyo maana haina kichwa wala miguu na imetungwa kwa nia mbaya, vile vile uongo umeshakuwa ni uhai wa taifa hilo,”alisema Mbatia.

  Alisema sasa inatakiwa serikali irudi kwenye katiba kwa kuwa makosa haya ni madogo tu sheria nyingi zina makosa, na zinahitaji marekebisho makubwa.

  “Kutungwa kwa hii sheria hakuna nia ya kupambana na fedha chafu bali ni maslahi ya watu wachache,”alisema.

  Naye Ismail Jusa wa Chama Cha Wananchi (CUF), ambaye hivi karibuni baada ya muafaka wa Chama Cha Mapinduzi CCM na CUF Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa mbunge wa kuteuliwa, alisema kitendo cha sheria hiyo kusainiwa ikiwa na mapungufu hayo na sasa kurudishwa tena bungeni inaonyesha jinsi serikali isivyokuwa makini juu ya masuala muhimu yenye maslahi na taifa.

  “Serikali ingekuwa makini yote haya yasingetokea, pesa za walipa kodi zinateketea bure, siku moja kwa bunge kukaa ni gharama kubwa sana, hii inaoyesha kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchini,” alisema Jusa.

  Juzi Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa amewasilisha mapendekezo hayo kutokana na kile anachoamini kuwa Rais Kikwete amedanganywa na kusaini sheria hiyo kimakosa.

  Alisema aliamua kuliwasilisha suala hilo kwanza kwenye kamati ya uongozi ya Bunge ili kama angepuuzwa, alifikishe suala hilo bungeni mwenyewe kwa namna anayoona inafaa.

  "Mapambano ndio yameanza; mimi ni mjumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge na leo (jana) tulikuwa na kikao, nimehoji suala hilo kabla sijalifikisha bungeni kwa namna ambayo nitaona inafaa," alisema Dk Slaa.

  "Bado nasisitiza kuwa Mwanasheria Mkuu amedanganya kwa kusema vifungu hivyo viko sahihi kwa kuwa Ofisi ya (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera na Uratibu wa Bunge-),Phillip Marmo ndio iliyovifanyia marekebisho. Ofisi ya Marmo haina mamlaka ya kubadili vifungu vya sheria iliyopitishwa na Bunge.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=19165
   
Loading...