Sheria ya gharama za uchaguzi yapita kwa mbinde


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,975
Likes
5,347
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,975 5,347 280
1265982749_jajiw.jpg

Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema.
MUSWADA wa sheria za gharama za uchaguzi jana ulipita kwa mbinde huku ukiibua malumbano makubwa baina ya mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema na Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge pamoja na wabunge wengine kuhusu vipengele mbalimbali vya muswada huo...
Mwanasheria Mkuu wa serikali alipingana waziwazi na Chenge aliyekuwa mwanasheria mkuu wa zamani hali iliyomlazimu naibu spika kuingilia kati mara kwa mara.

Muswada huo ulimlazimisha mwanasheria wa serikali kusimama kwa zaidi ya mara 11 kwa ajili ya kutoa ufafanuzi huku akitahadharisha kuwa yeye ni Jaji, hivyo kuwataka wabunge kuwa watulivu baada ya kubaini kuwa baadhi yao walikuwa wakizungumza kwa sauti za juu wakati mwanasheria huyo aliposimama.

Wanasheria hao pamoja na wengine walikuwa wakibishania katika kifungu cha saba ambacho hakikuwa na ufafanuzi kuhusu gharama za watu wanaosaidia katika kampeni ambapo Chenge alitaka baadhi ya mambo yaongezwe ili kupanua wigo kwa wapiga kampeni hao katika kugharamiwa baadhi ya mambo ikiwemo chakula na malazi.

Chenge alitaka kifungu hicho kiwekwe kwani kwa mtazamo wake ni halali kwa mgombea kuwalisha na kuwagharamia watu ambao wanamsaidia katika kampeni jambo lililotafsiriwa vibaya na baadhi ya wabunge.

Baada ya kusimama kwa zaidi ya mara mbili katika kifungu hicho, ilimlazimu Werema kusimama zaidi ya mara mbili na kuanza kubishana kwa vifungu vya sheria, kabla ya Werema kumtaka Chenge akubaliane na mapendekezo ya serikali.

"Mheshimiwa Mwenyekiti naomba mheshimiwa Chenge akubaliane na mapendekezo hayo, kwani hata nikiangalia naona kuwa hakuna kanuni inayoruhusu mbunge kutoa mapendekezo yake kwa kutumia njia kama aliyoitumia Chenge hivyo ni kama alileta bila ya kufuata utaratibu," alisema Werema na kuongeza.

"Namshauri Chenge akubaliane na hilo kwa kuwa sheria inazaliwa na inakuwa, kwa hiyo katika jambo kama hilo asiwe na wasiwasi ikibidi kurekebisha tutafanya hivyo."

Baada ya hapo alisimama Dk Willibrod Slaa ambaye alimtetea Chenge kwa kusema kuwa alitumia Kanuni ya Bunge kifungu cha 10, hivyo alikuwa sahihi mapendekezo yake kuangaliwa na Bunge na ikibidi yafanyiwe kazi.

Hali ilikuwa ya mvutano na kumfanya Naibu Spika, Anna Makinda kutumia uzoefu wake kuwatuliza wabunge ambao walitaka kusimama bila ya kufuata utaratibu, huku wengine wakilazimisha kusimama zaidi ya mara mbili katika kifungu kimoja.

Baada ya kuona hivyo mwanasheria aliamua kunong’ona na Waziri Marmo kabla ya kusimama na kukubaliana na wazo la Chenge la kuingiza gharama hizo ingawa alitoa masharti ya kutaka iwekwe idadi kamili ya watu watakao kuwa katika kundi la kampeni.

"Kama ni hivyo nakubaliana na wazo la Chenge, lakini nasema kuwa iwekwe idadi kamili ya watu wa kampeni kwani anaweza mtu akatumia njia hiyo kwa kuwa na wapiga kura karibu jimbo zima."

Wabunge wengine ambao walionekana kuwa moto na muswada huo ni pamoja na Halima Mdee, Dk Slaa, John Cheyo na Peter Serukamba.

Licha ya msaada huo kupitishwa, baadhi ya wabunge walionekana kutoridhishwa kufuatia Naibu Spika kupitisha baadhi ya vifungu huku wabunge wakiwa wamesimama ili kutoa hoja.

Muswada huo ulipitishwa jana na leo Bunge linatarajia kujadili muswada wa sheria ya uchaguzi.

Wakati huo huo, Mbunge wa Njombe Kaskazini (CCM), Jackson Makweta jana aliwapiga vijembe wanaopinga muswada wa sheria ya uchaguzi unaojadiliwa; akisema unawasuta na kwamba, bila kuwepo utashi wa kisiasa sheria hiyo haiwezi kutekelezeka.

Akichangia muswada huo jana Makweta alisema: "Ningekuwa mwalimu ningeuliza; hapa ni nani kati yetu ameingia hapa hakutoa hongo?."

Alisema hata nguvu ya hayati Mwalimu Nyerere ilitokana na usafi wake na kusisitiza kuwa kitu kichafu hakiwezi kusafisha uchafu.

Makweta akimpongeza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kusema alitangaza umaskini ambao viongozi wengi wanaotumia tamaa na ujasiri wanaukimbia.

Mbali na kumpongeza Pinda, Makweta alisema anashangaa watu wanaosema wasomi wagombee uongozi akisema Bunge si la wasomi pekee, bali linahitaji viongozi ambao hawanunui uongozi.

CHANZO: MWANANCHI
 

Forum statistics

Threads 1,236,067
Members 474,965
Posts 29,245,549