Sheria ya Ewura,ina mapungufu au inapindishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Ewura,ina mapungufu au inapindishwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rugas, Aug 20, 2011.

 1. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wakuu Habari!
  Mi kwa siku kadhaa najiuliza juu ya sheria hii ya Ewura! iliyotumika kuifungia Bp kuuza mafuta kwa miezi mitatu baada ya kukaidi compliance order! Baada ya Ewura kutoa zuio,vituo vya Bp havikuuza mafuta km siku 4 hivi,baadae nikashangaa kusikia tena kuwa kilichozuiwa ni kuuza mafuta ya jumla,lakini vituo vinaruhusiwa kuuza mafuta kama kawaida!Mimi hapo ndo ninakoona mapungufu kwa sababu zifuatazo!
  1.Bp wanaweza kufungua maghala yao,na kubepa mafuta kwa kutumia magari mengine ,mfano magari ya Gapco,au Total na wakafikisha mafuta vituoni na biashara ikaendelea kama kawaida.(kuna tetesi kuwa hili ndilo linalofanyika sasa)

  2.Kwa kuwa wananchi wanaojua yalipo maghala ya bp ni wachache,basi hii inaweza kutumika km nafasi ya kuwaghiribu maafisa wa EWURA na rushwa ikaingia na biashara ikaendelea km kawaida bila wenye nchi kujua.

  Na mengine mengi yanaweza kujificha ndani ya hili.

  Kwa maoni yangu,sheria isitengetoa mianya kama hii,ambayo bado inapunguza udhibiti na kuendelea kuwapa viburi hawa matajili.

  Wale wanaijua vizuri sheria hii wanisaidie.......
   
 2. t

  tacocuchi Member

  #2
  Aug 20, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inchi hii waungwana imeshauzwa, ndiyo maana yule patel aliipa serikali saa 24 bei iwe imerudi palepale, ki ukweli alikuwa anajua anachokisema kwani siku chache bei ikarudishwa kama kawa. Ama kweli hili ni shamba la bibi, inauma sana lakini hamna jinsi. Wakubwa wameamua kuwa mafisadi papa na nyangumi. Nawasilisha.
   
 3. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Leo hii nimefanya biashara na kampuni hii, walichokifanya ni kuama pale Kurasini na kuamia pale Mchicha, na biashara inaendelea kama kawa hii ndo Tz bana!!!!! Inauma lakini.
   
Loading...