Sheria ya Bodi ya Mikopo (HESLB) bado ni kansa kwa wanufaika

inspectorbenja

JF-Expert Member
Oct 14, 2012
462
394
Mara kwa mara wanufaika wa bodi ya mikopo wamekuwa wakilalamika juu ya kitu kinachoitwa retention value fee kinachotozwa na bodi. Yaani kila mwaka mtu anatozwa 6% ya ya deni ili kutuinza thamani ya shilingi.

Hiki ndio kilio watu wamekuwa wakiomba kipengele hiki kandamizi kiondolewe. Watu wengine wamekiwa wakiomba hata mbele ya viongozi wakuu wa nchi. Mfano wakati wa mei mosi lilizungumzwa, mhe rais alipoenda sua. Kuna mhadhiri alilizungumzia mbele ya rais. Lakini kwa bahati mbaya huwa linapuuzwa wala hakuna kiongozi mkubwa anayeonekana kuguswa nalo.

Bhati mbaya zaidi,mara zote bodi wanapotoa majibu au ufafanuzi,wamekuwa wakibwabwaja bwabwaja tu na kutolea ufafanuzi wa vitu ambavyo hata sisi hatuhitaji,siyo jero wala kilio. Yaani wamekuwa wakileta ngojera tu. Hata majibu ambayo amejibiwa mwalimu Iddy, wamebwabwaja bwabwaja tu, kilio cha mwalimu Iddy ilikuwa ni hii 6% anayotozwa mtu kila mwaka. Sasa wanavyisema mwalimu Iddy kaelewa na atakuwa balozi mwema sijui yeye binafsi wamemuondolea hiyo 6%

Kipengele hiki ni kandamizi, mbona watu wanaoidai serikali kwa miaka nenda rudi na wanambiwa wasubiri wao hawaikwekei serikali 6% kila mwaka kutunza thamani ya shilingi.

Jamani 6% ya kila mwaka inatuua, enyi viongozi wetu na bodi mtuonee huruma jamani. Tamzania ni yetu wote
 
Hakuna anayekopesha pesa halafu akuombee umalizane na deni lake kisha usiwe mteja wake tena ni lazima afanye namna ya kukubakiza ili aendelee kukukamua. Kumbuka hiyo ndio biashara yake na ndiko anakopatia faida.
 
Umasikini wa WaTz yeye ndo anaona ni uzalendo.MHUJUMU UCHUMI MKUBWA NI YEYE anawaumiza na kuwatapisha hela WaTz kwa kesi inayomhusu yeye.
 
Tutofautishe private business na government institutions.
Hakuna anaye kopesha pesa halafu akuombee umalizane na deni lake kisha usiwe mteja wake tena ni lazima afanye namna ya kukubakiza ili aendelee kukukamua. Kumbuka hiyo ndio biashara yake na ndiko anakopatia faida.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom