Sheria ya Bodi ya Kitaaluma ya Walimu Tanzania ya Mwaka 2018

Apr 29, 2019
36
25
THE TANZANIA TEACHERS'PROFESSIONAL BOARD ACT NO 6 OF 2018

UTANGULIZI
Tanzania ni Nchi ambayo inaongozwa kwa sheria,Kanuni,Miongozo na Taratibu Mbalimbali ambapo Msingi wake ni Katiba.Kwahiyo kwa Kuzingatia Misingi ya Haki na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Ibara 18(a)"kila mtu anao uhuru wa kuwa na Maoni na kueleza fikra zake".Hivyo haya ni Maoni Binafsi Juu ya "The Tanzania Teachers' professional Board Act No 6/2018."

MADHARA/KUTOFAA KWA SHERIA HII KWA WALIMU TANZANIA
1.Gharama kubwa kwa Walimu.Sheria hii itaambatana mzigo mkubwa Sana wa gharama ambazo Mwalimu anapaswa kuingia/kulipa kutoka kwenye kipato chake kama ifuatavyo;
i. Gharama za kila Mwaka kwaajili ya Mafunzo
ii. Ada ya Lesseni Ambayo inapaswa kuhuishwa kila Mwaka.
iii. Ada Ya Usajili ambao utafanyika kwa kila Mwaka
iv. Gharama za kuthibitisha vyeti vya Kitaalum kwaajili ya Usajili.Hili Mwalimu asajiriwe anahitaji kuthibitisha vyeti vyake km takwa la kisheria na mamlaka za kufanya Kazi hii ni Mahakama/Kamishina wa Viapo ambapo Kimsingi kuna gharama
(The Tanzania Teachers'professional Board Act No 6/2018 Section 19(2)(a)(b).

2. KUWA NA MAMLAKA MBILI TOFAUTI ZA NIDHAMU KWA WALIMU,ZENYE SHERIA TOFAUTI NA ADHABU TOFAUTI.
Kwa Mujibu wa Sheria Ya Tume Ya Utumishi Wa Walimu No 25 ya Mwaka 2015 na Kanuni zake za Mwaka 2016 zinaeleza Mamlaka za Nidhamu kwa Walimu wa Shule za Msingi na sekondari za Serikali kuwa ni; Mwalimu Mkuu/Mkuu wa Shele,Kamati ya Nidhamu ya Wilaya,Tume Ya Utumishi Wa Walimu Makao Makuu na Mh Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Kanuni za Tume Ya Utumishi Wa Walimu za Mwaka 2016 Kanuni 12(1)(2)(3) na 7(1). Na Wakati huo huo Sheria ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania No 6 ya Mwaka 2018 ikionesha kuwa nayo ni Mamlaka ya Nidhamu kwa Mwalimu wa Ngazi ya Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada kwa shule za Umma na Binafsi K/f Cha 6(1)(e)(f),7(a-d) na 8(1).Hali hii itaongeza usumbufu na Manyanyaso kwa Walimu kwani kosa Moja linaweza kusikilizwa na Mamlaka tofauti na bado vinaweza Kutoa adhabu tofauti Mfano; Mamlaka Moja inaweza kumfukuza Mwalimu Kazi wakati Ktk mamlaka nyingine Mwalimu akiwa Ameshinda. Hii utasababisha migongano ya kisheria na bado ni Kwenda kinyume Cha sheria za Nchi kwa Kutoa adhabu mbili tofauti kwa kosa Moja na mtu mmoja(Penal code Cap 16 R.E 2019 Section 21 "A person shall not be punished twice,either under the provisions of this Code or Under the provisions of any other law to be).

3. WAJUMBE WA BODI YA KITAALUMA YA WALIMU TANZANIA PAMOJA NA KAMATI YA UCHUNGUZI KUTOKUWA WANA TAALUMA YA UALIMU.
(A).Kwa Mujibu wa Sheria ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania,Mwalimu ni mtu aliyepata Mafunzo Ktk Chuo/Taasisi inayotambulika na Bodi na kufaulu kwa Mujibu wa sheria yake Ktk Ngazi ya Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada na kusajiriwa na Bodi.
Hivyo Sheria inaonesha Bodi itakuwa na Wajumbe Tisa(9) ambapo M/Kiti atateuliwa na Rais Kifungu Cha 5(1)(a) Cha Sheria Ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania NO 6/2018 ambaye ni lazima Atakuwa Mwalimu na Kifungu Cha 5(1)(b)(iii) kinatoa Mwanya wa Mjumbe mwingine atakaependekezwa Cha Chama Cha Walimu ingawa pia sheria haijasema kuwa lazima awe Mwalimu.Na Wajumbe Wengine 7 Waliobakia watateuliwa na Waziri anaehusika na Elimu na Sheria imeweka wazi Taasisi watakazotoka ambapo hawatakuwa Walimu Kif Cha 5(b)(i,ii,iv,v,vi,vii na viii). Kwahiyo Bodi inayoshughulikia Mambo ya Taaluma ya Ualimu na Nidhamu ya Walimu Wajumbe Wake 7/9 siyo Walimu. (B). Kamati ya Uchunguzi Ktk Mashauri ya Nidhamu ya Walimu itakuwa na Wajumbe watano lakini Walimu ni Wawili Kati yao(Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Ualimu Tanzania No 6 ya Mwaka 2018 k/f Cha 42(1)(a-d) na k/f Cha 8(1) na (2)(b).

4. SHERIA KUWASAJIRI NA KUWATAMBUA WATU AMBAO HAWAJASOMA NGAZI YEYOTE YA TAALUMA YA UALIMU NA KUWA WALIMU
Sheria hii itawasajiri na kuwatambua watu ambao hawajasoma kabisa Ualimu ambao watafanya Majukumu ya Ualimu km Walimu Wengine waliosoma Ngazi Mbalimbali za Taaluma Ya Ualimu eti kwa kigezo kuwa watafanya Majukumu ya Ualimu chini ya Usimamizi wa Walimu (K/f Cha 28(1)(c) Cha Sheria Ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania No 6/2018).

5. WALIMU KUONGEZA VYOMBO VYA AJIRA/WASIMAMIZI WA WALIMU.
Sheria hii inaongeza Chombo ambacho ni Bodi ambacho kinaenda kumsimamia Mwalimu dhidi ya Vyombo Vingine lukiki vinavyoshughulika na Ajira ya Mwalimu wakati hitaji la Walimu ikiwa ni kutaka kuwa na Chombo kimoja tu.Vyombo Vinavyoshughulika Moja kwa Moja na Walimu ni TSC,TAMISEMI,WIZARA YA ELIMU,WIZARA YA UTUMISHI WA UMMA,WIZARA YA FEDHA NA SASA BODI YA WALIMU.
Hali hii inaleta urasimu kwa Mwalimu Katika kupata Haki zake.

6. SHERIA YA BODI YA TAALUMA YA UALIMU TANZANIA KUTOWATAMBUA WALIMU WA SHAHADA YA UZAMILI NA UZAMIVU.
Katika sherii hii No 6 ya Mwaka 2018 ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania inawatambua watu ambao hawajasoma Ualimu Kabisa,Waliosoma Ngazi ya Cheti, Ngazi ya Diploma ya Juu, Diploma na Shahada tu ila siyo Shahada ya Uzamili na Uzamivu ingawaje wapo Ktk shule zetu za Sekondari na Msingi Tanzania Bara.

7. SHERIA YA BODI YA TAALUMA YA UALIMU TANZANIA NO 6 YA MWAKA 2018 KUTOA MAMLAKA KWA BODI KUTOA HUKUMU ZA WALIMU KWENDA JELA KWA MAKOSA YA KINIDHAMU/KITAALUMA.
Sheria inatoa mamlaka hayo kwa Bodi Kutoa adhabu za Vifungo vya Kati ya miezi mitatu mpk Mwaka Mmoja Jela.

Kwahiyo niwaombe Walimu na Wadau Wengine kuisoma Sheria Vizuri Ili kuweza kupaza sauti Juu ya Sheria hii kwa Mstakabali wa Elimu Ya Watoto Wetu na Taifa letu la Tanzania kwa Ujumla.

====

Na.Alex Sonna,Dodoma

Chama cha walimu Tanzania (CWT) kimesema kitaendelea kupinga na kukataa juu ya zoezi la uanzishwaji wa Bodi ya kitaaluma ya Walimu Tanzania kwani bodi hiyo imelenga kumkandamiza Mwalimu badala ya kumsaidia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo April,13,2021 Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya amesema majukumu yaliyooneshwa kwenye bodi hiyo yanafanana nay ale yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa walimu (TSC) iliyopo sasa.

“Mnamo mwaka 2019 ,CWT kilialikwa kutoa maoni kuhusu uanzishwaji wa Bodi hiyo ,kimsingi sisi CWT,tuliikataa kwa nguvu zote baada ya kusoma sheria hiyo tukajiridhisha pasi na shaka kwamba chombo hiki kililenga kumgandamiza mwalimu badala ya kumsaidia ,aidha majukumu yaliyo kwenye bodi hiyo yanafanana na yale yanayofanywa na Tume ya utumishi wa walimu ”amesema Bi.Ulaya

Bi.Ulaya ameelezea kuwa Mnamo Tarehe 12 April,2021 CWT tulialikwa na katibu wa bunge kukutana na kamati ndogo ya Bunge ya sheria juu ya kanuni za uendeshaji wa bodi hiyo ambayo msingi wake ni sheria mama ambayo sisi CWT tulikataa tangu mwanzo,katika kikao hicho cha tarehe 12,April,2021 Chama cha Walimu Tanzania kiliendelea na msimamo wake wa usitishwaji wa chombo hiki na kuimarisha utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)

Aidha,Rais huyo wa CWT ametaja sababu kadhaa za msimamo kupinga uwepo wa bodi hiyo kuwa ni pamoja na gharama za bodi ambapo uendeshwaji utategemea pesa ya mwalimu mfukoni na ada ni elfu hamsini kwa mwaka pamoja na kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu .

“Bodi hii tunaipinga kwa nguvu zote kwa sababu ,uendeshaji wa bodi hii utategemea pesa ya walimu mfukoni kwa ajili ya usajili,leseni na ada kwa mwaka ambayo si chini ya Tsh.50,000/=,gharama za kusikiliza mashauri,gharama za semina ya kila mwaka ambayo ni lazima kuhuisha leseni hiyo ,kushindwa kufanya hivyo mwalimu atanyang’anywa leseni na hivyo kupoteza sifa ya kufundisha na sababu nyinyine ya kuikataa bodi hii ni kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu na majukumu yakifanan”amesema.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Chama hicho Dinah Mathaman amesema kuwa
wanachohitaji walimu kwa sasa ni utulivu na siyo kuwaongezea chombo
ambacho kinaongeza mzigo wa kwa mwalimu.
“Kama tunavyoshuhudia kila mwaka matokeo na taaluma imeendelea kupanda
kutokana na walimu kufanya kazi yao kwa tija,kama ni hizo semina ,mwajiri anapaswa aone umuhimu wa kumnoa mwalimu kwa kumpa semina kutokana na bajeti aliyoiandaa kutoka katika ofisi yake na siyo semina na mafunzo kugharamiwa na mwalimu.”amesema Dinah
Hata hivyo ameiomba Serikali kuendelea kuwaamini kwamba wana taaluma ya kutosha na
wana uwezo mzuri wa kufundisha.

“Walimu tunafanya kazi kwa bidii na ukiangalia ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kinachotakiwa ni serikali kuendelea kuamini walimu pamoja na kuwatia moyo “amesema.

Naye Katibu Mkuu wa chama hicho Mwl. Deus Seif amehoji kuwa kuna nini cha ziada anachotakiwa afanye mwalimu wakati ufaulu unaongezeka kila mwaka .

Mwl Seif amesema kuwa,tayari wana TSC ambayo inawasimamia lakini pia inatoa nafasi pana kwa mwalimu kujitetea hata lipotokea tatizo tofauti na bodi ambayo mwalimu akiwa na tatizo itampasa atoke alipo na kuifuata bodi ilipo tena kwa gharama zake.

Aidha Naibu Katibu Mkuu wa CWT Mwl. Japhet Maganga ,amesema hawaikubali
bodi hiyo kwani TSC haijawahi kusema imeshindwa kutekeleza majukumu yake ambayo yanatarajiwa kutekelezwa na Bodi hiyo. pia alisema Bodi hiyo haina manufaa yoyote kwa mwalimu zaidi ya kwenda kumdidimiza mara baada ya kuanza kufanya kazi.
 
THE TANZANIA TEACHERS'PROFESSIONAL BOARD ACT NO 6 OF 2018

UTANGULIZI
Tanzania ni Nchi ambayo inaongozwa kwa sheria,Kanuni,Miongozo na Taratibu Mbalimbali ambapo Msingi wake ni Katiba.Kwahiyo kwa Kuzingatia Misingi ya Haki na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Ibara 18(a)"kila mtu anao uhuru wa kuwa na Maoni na kueleza fikra zake".Hivyo haya ni Maoni Binafsi Juu ya "The Tanzania Teachers' professional Board Act No 6/2018."

MADHARA/KUTOFAA KWA SHERIA HII KWA WALIMU TANZANIA
1.Gharama kubwa kwa Walimu.Sheria hii itaambatana mzigo mkubwa Sana wa gharama ambazo Mwalimu anapaswa kuingia/kulipa kutoka kwenye kipato chake kama ifuatavyo;
i. Gharama za kila Mwaka kwaajili ya Mafunzo
ii. Ada ya Lesseni Ambayo inapaswa kuhuishwa kila Mwaka.
iii. Ada Ya Usajili ambao utafanyika kwa kila Mwaka
iv. Gharama za kuthibitisha vyeti vya Kitaalum kwaajili ya Usajili.Hili Mwalimu asajiriwe anahitaji kuthibitisha vyeti vyake km takwa la kisheria na mamlaka za kufanya Kazi hii ni Mahakama/Kamishina wa Viapo ambapo Kimsingi kuna gharama
(The Tanzania Teachers'professional Board Act No 6/2018 Section 19(2)(a)(b).

2. KUWA NA MAMLAKA MBILI TOFAUTI ZA NIDHAMU KWA WALIMU,ZENYE SHERIA TOFAUTI NA ADHABU TOFAUTI.
Kwa Mujibu wa Sheria Ya Tume Ya Utumishi Wa Walimu No 25 ya Mwaka 2015 na Kanuni zake za Mwaka 2016 zinaeleza Mamlaka za Nidhamu kwa Walimu wa Shule za Msingi na sekondari za Serikali kuwa ni; Mwalimu Mkuu/Mkuu wa Shele,Kamati ya Nidhamu ya Wilaya,Tume Ya Utumishi Wa Walimu Makao Makuu na Mh Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Kanuni za Tume Ya Utumishi Wa Walimu za Mwaka 2016 Kanuni 12(1)(2)(3) na 7(1). Na Wakati huo huo Sheria ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania No 6 ya Mwaka 2018 ikionesha kuwa nayo ni Mamlaka ya Nidhamu kwa Mwalimu wa Ngazi ya Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada kwa shule za Umma na Binafsi K/f Cha 6(1)(e)(f),7(a-d) na 8(1).Hali hii itaongeza usumbufu na Manyanyaso kwa Walimu kwani kosa Moja linaweza kusikilizwa na Mamlaka tofauti na bado vinaweza Kutoa adhabu tofauti Mfano; Mamlaka Moja inaweza kumfukuza Mwalimu Kazi wakati Ktk mamlaka nyingine Mwalimu akiwa Ameshinda. Hii utasababisha migongano ya kisheria na bado ni Kwenda kinyume Cha sheria za Nchi kwa Kutoa adhabu mbili tofauti kwa kosa Moja na mtu mmoja(Penal code Cap 16 R.E 2019 Section 21 "A person shall not be punished twice,either under the provisions of this Code or Under the provisions of any other law to be).

3. WAJUMBE WA BODI YA KITAALUMA YA WALIMU TANZANIA PAMOJA NA KAMATI YA UCHUNGUZI KUTOKUWA WANA TAALUMA YA UALIMU.
(A).Kwa Mujibu wa Sheria ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania,Mwalimu ni mtu aliyepata Mafunzo Ktk Chuo/Taasisi inayotambulika na Bodi na kufaulu kwa Mujibu wa sheria yake Ktk Ngazi ya Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada na kusajiriwa na Bodi.
Hivyo Sheria inaonesha Bodi itakuwa na Wajumbe Tisa(9) ambapo M/Kiti atateuliwa na Rais Kifungu Cha 5(1)(a) Cha Sheria Ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania NO 6/2018 ambaye ni lazima Atakuwa Mwalimu na Kifungu Cha 5(1)(b)(iii) kinatoa Mwanya wa Mjumbe mwingine atakaependekezwa Cha Chama Cha Walimu ingawa pia sheria haijasema kuwa lazima awe Mwalimu.Na Wajumbe Wengine 7 Waliobakia watateuliwa na Waziri anaehusika na Elimu na Sheria imeweka wazi Taasisi watakazotoka ambapo hawatakuwa Walimu Kif Cha 5(b)(i,ii,iv,v,vi,vii na viii). Kwahiyo Bodi inayoshughulikia Mambo ya Taaluma ya Ualimu na Nidhamu ya Walimu Wajumbe Wake 7/9 siyo Walimu. (B). Kamati ya Uchunguzi Ktk Mashauri ya Nidhamu ya Walimu itakuwa na Wajumbe watano lakini Walimu ni Wawili Kati yao(Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Ualimu Tanzania No 6 ya Mwaka 2018 k/f Cha 42(1)(a-d) na k/f Cha 8(1) na (2)(b).

4. SHERIA KUWASAJIRI NA KUWATAMBUA WATU AMBAO HAWAJASOMA NGAZI YEYOTE YA TAALUMA YA UALIMU NA KUWA WALIMU
Sheria hii itawasajiri na kuwatambua watu ambao hawajasoma kabisa Ualimu ambao watafanya Majukumu ya Ualimu km Walimu Wengine waliosoma Ngazi Mbalimbali za Taaluma Ya Ualimu eti kwa kigezo kuwa watafanya Majukumu ya Ualimu chini ya Usimamizi wa Walimu (K/f Cha 28(1)(c) Cha Sheria Ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania No 6/2018).

5. WALIMU KUONGEZA VYOMBO VYA AJIRA/WASIMAMIZI WA WALIMU.
Sheria hii inaongeza Chombo ambacho ni Bodi ambacho kinaenda kumsimamia Mwalimu dhidi ya Vyombo Vingine lukiki vinavyoshughulika na Ajira ya Mwalimu wakati hitaji la Walimu ikiwa ni kutaka kuwa na Chombo kimoja tu.Vyombo Vinavyoshughulika Moja kwa Moja na Walimu ni TSC,TAMISEMI,WIZARA YA ELIMU,WIZARA YA UTUMISHI WA UMMA,WIZARA YA FEDHA NA SASA BODI YA WALIMU.
Hali hii inaleta urasimu kwa Mwalimu Katika kupata Haki zake.

6. SHERIA YA BODI YA TAALUMA YA UALIMU TANZANIA KUTOWATAMBUA WALIMU WA SHAHADA YA UZAMILI NA UZAMIVU.
Katika sherii hii No 6 ya Mwaka 2018 ya Bodi ya Taaluma Ya Ualimu Tanzania inawatambua watu ambao hawajasoma Ualimu Kabisa,Waliosoma Ngazi ya Cheti, Ngazi ya Diploma ya Juu, Diploma na Shahada tu ila siyo Shahada ya Uzamili na Uzamivu ingawaje wapo Ktk shule zetu za Sekondari na Msingi Tanzania Bara.

7. SHERIA YA BODI YA TAALUMA YA UALIMU TANZANIA NO 6 YA MWAKA 2018 KUTOA MAMLAKA KWA BODI KUTOA HUKUMU ZA WALIMU KWENDA JELA KWA MAKOSA YA KINIDHAMU/KITAALUMA.
Sheria inatoa mamlaka hayo kwa Bodi Kutoa adhabu za Vifungo vya Kati ya miezi mitatu mpk Mwaka Mmoja Jela.

Kwahiyo niwaombe Walimu na Wadau Wengine kuisoma Sheria Vizuri Ili kuweza kupaza sauti Juu ya Sheria hii kwa Mstakabali wa Elimu Ya Watoto Wetu na Taifa letu la Tanzania kwa Ujumla.
Haifai na wazo la kuwepo bodi hiyo lizikwe mara moja. Huu ni upuuzi meingine wa kuongeza manyanyaso na unyonyaji kwa kapato kadogo ka mwalimu... Haifai hata chembe.
 
Ninashauri bodi ya walimu uwepo ila taasisi kama TSC, na CWT zifutwe. Na si kweli kwamba kukaa kwenye bodi kila mwaka utajisaliji upya bali kila mwaka utalipia leseni au ada yako. Na ada hiyo inakuwa sawa kwà wanachama wote tofauti na CWT inakata fedha za walimu kila mwrzi kwà kupitia asilimia fulani ya mshahara wako.
 
Back
Top Bottom