Iweje sheria iwe upande mmoja tu wa kunyonya?
Gari ikiwa haina bima ni kosa kwa mujibu wa sheria, kwahiyo polisi trafiki watakukamata mara moja! Lakini kwanini sheria hiyo hiyo haielekezi wazi ulazima wa mtoa bima kumlipa punde mteja wao bila kuzungushana? Mbaya zaidi kwanini meno ya polisi yakate upande mmoja tu wa kumshuritisha mtu akate bima ya gari, lakini wanakutelekeza unapofuatilia kulipwa.
Kwanini sheria isingewekwa wazi kwamba Mteja wa bima alipwe ndani ya siku 3 baada ya ajali kuthibitishwa na polisi na endapo akichelewa pesa iwe inaongezeka na baada ya siku 15 kama atakuwa hajalipa mtoa huduma akamatwe kwa nguvu!
Nini maana ya kumlazimishwa mtu kuwa na bima halafu asilipwe ajali inapotokea hadi wengine huamua kutengeza magari yao wenyewe?
Bongo kampuni nyingi za bima wakishapokea pesa za mteja hukimbilia kuzitumia kujengea nyumba zao na kuacha akaunti zikiwa tupu kiasi kwamba hawana uwezo wa kumlipa mteja wao akipatwa na tatizo zaidi ya kumzungusha kwasababu hakuna sheria inayowabana!