JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Kusitisha ajira maana yake ni kumalizika kwa mahusiano ya kikazi baina ya mwajiri na mwajiriwa au mfanyakazi, kusitisha ajira kihalali, kuachisha kazi isivyo halali, kusitisha kazi kwa makubaliano, mwajiri kusitisha kazi, kuachishwa kazi, kuacha kazi, kustaafu, kuritaya, mwenendo mbaya wa kazi, utovu wa nidhamu sehemu za kazi, kupunguzwa kazi, ridandasi, madhara ya kusitisha kazi isivyo halali, madhara ya kuachisha kazi isivyo halali
36. Kwa lengo la Sehemu hii Ndogo - (a) ''kusitishwa kwa ajira” kunajumuisha-
(i) kusitishwa ajira kwa haki chini ya sheria za kawaida zisizoandikwa;
(ii) kuacha kazi kwa mfanyakazi kwa sababu kuendelea kwake na kazi kunakuwa kugumu kwa sababu ya mwajiri;
(iii) kushindwa kuongeza mkataba kwa kipindi maalumu katika masharti yaleyale au yanayofanana nayo kama kulikuwa na matarajio ya kawaida ya kuongeza
(iv) kushindwa kumruhusu mfanyakazi kurudi kazini baada ya kuchukua likizo ya uzazi inayotolewa chini ya Sheria hii au likizo nyingine ya uzazi iliyokubaliwa; na
(v) kushindwa kumwajiri tena mfanyakazi kama mwajiri amesitisha ajira ya wafanyakazi wengi kwa sababu ileile au inayofanana na hiyo na ameamua kuwaajiri tena mmoja au zaidi kati yao;
(b) ''sitishwa ajira” ina maana inayofanana na “kusitishwa kwa ajira”. Kuachishwa kusiko kwa haki