Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu namba 225 (4) inasema Upelelezi usipokamilika ndani ya siku 60 mshatakiwa kuachiwa huru. Hiki ni kitu ambacho hakitekelezwi ipasavyo na mahakama na baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakikaa muda mrefu mahabusu
Hayo yameelezwa Februari 10, 2020 na wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe katika maadhimisho ya siku ya sheria na mapendekezo ya maboresho ya mifumo ya utoaji haki
"Kuna haja ya wizara ya katiba na sheria kusisitiza utekelezaji katika hili kwani mbali na kuwapa haki watuhumiwa pia itapunguza msongamano wa mahabusu magerezani ambao wanaelezwa kuwa wengi kuliko wafungwa," amesema.
Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Anna Henga ameshauri makosa yote yawe na dhamana kwa kubadilisha masharti ya dhamana kulingana na aina ya kosa jambo litakalosaidia kudumisha dhana ya mtu kutoonekana kuwa na hatia mpaka pale mahakama itakapothibitisha
"Pia tunaunga mkono kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya maadhimisho ya sheria kuwa bado kuna changamoto kubwa ya upelelezi wa kesi, jambo linaloashiria kwamba Serikali ipo tayari kuchukua hatua katika kudumisha ustawi wa haki za binadamu hususani katika eneo la mfumo wa utoaji haki," amesema.