Sheria ndogo ndogo (by laws) zinatengeneza wigo mpana wa ubaguzi kwa wafanyabiashara

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Moja ya majukumu ya halmashauri na manispaa ni kutunga sheria kupitia baraza la council ambazo husainiwa na waziri mwenye dhamana. Ajabu sheria hizi zinazo tungwa hazizingati Hali ya usawa kwa wadau ambao ndiyo watumiaji wa sheria hizi hususani wafanya biashara.

Pamoja na upitishwaji wa sheria hizi kutumika nyingi ya sheria haziwafiki wadau Kama mwongozo wa serikali za mitaa unavyotamka. Sheria zinaishia kwenye mabaraza ya vijiji bila ushirikishi wa wananchi matokeo yake wananchi wanasomewa matumizi ya sheria ambazo hawajashirikishwa Kama wadau.

Nasemea hili hususani kwa wafanya biashara wa bar na grocery ambao wanatakiwa kufungua biashara zao kuanzia saa tisa na kuwekewa limit ya muda mpaka saa tano usiku,lakini biashara zingine haziguswi na sheria hizo Kama wanavyoguswa na kuumizwa wafanyabiashara wa Pombe.

Wajasiliamali hawa ni Watanzania,wanaolipa Kodi sambamba na wengine,lakini hapo hapo wauzaji wa Pombe za jumla wakiruhusiwa kuuza bidhaa hiyo hiyo kuanzia asubuhi.

Kwa mantiki hii tuna Jenga Taifa la wanyonge dhidi ya wanaolindwa na sheria bila bughudha.

Athari yake ni kubwa kwa jamii kwa kuwa tunatanua mianya ya rushwa kwa viongozi na askari POLISI kuwavizia wafanya biashara hawa kwa malengo ya kuwakamata kwa kufungua biashara kabla ya wakati na kufunga kwa kuzidisha muda.

Ina tengeneza umungu mtu kwa watendaji wa serikali za vitongoji mpaka kata bila kuzingatia haki za mwananchi kufanya biashara bila kubughudhiwa.

Ukiangalia viwanda vya bidhaa hizi haziwekewi limit ya uzalishaji,Depot haziwekewi limit na hata maduka ya jumla hayawekewi limit,halmashauri hizi hazioni kuwa zina tengeneza sheria kandamizi ilihali zikitaka wafanya biashara hawa walipe kodi,leseni na ghasia nyingine nyingi.

Ikiwa muda wa biashara unabanwa wafanya biashara hawa watawezaje kuhimili kulipa mapato ya serikali kwa wakati.

Kwa maoni yangu Serikali ilitazame jambo hili kwa umakini mkubwa Sana,ni heri sheria kali ikawekwa kwa watumishi wa umma kutokunywa wakiwa kazi kuliko kudhibiti biashara ambazo ni chanzo cha mapato ya serikali.
 
Back
Top Bottom