Sheria Namba 8 haiwezi kuwa Juu ya Katiba ya Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria Namba 8 haiwezi kuwa Juu ya Katiba ya Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Barubaru, Feb 16, 2012.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sheria Namba 8 haiwezi kuwa Juu ya Katiba ya Zanzibar. Written by Harith Ghassany // 15/02/2012 // Habari // 1 Comment

  Na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa – Zanzibar.


  Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar.
  Vipi sheria ya Mabadiliko ya Katiba iweze kufanya kazi Zanzibar wakati Zanzibar ni Nchi iliyo na mipaka yake Kikatiba? Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi wazi katika Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza kwamba: “Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar”. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba kupitia kifungu chake cha 19-(1) kinachohusiana na makosa na adhabu kwa watakaotoa maoni nje ya hadidu rejea za rasimu ya Katiba: kifungu hicho pamoja na sheria yenyewe ya marekebisho ya Katiba, mwisho wake CHUMBE !!

  Pili, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984,
  Toleo la 2010, inaeleza wazi kuwa, Katiba ya Zanzibar ndiyo yenye nguvu za kisheria nchini kote, ambapo ikitokezea sheria yo yote kutofautiana na Katiba ya Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana. Hii ni kuonesha nguvu na uwezo iliyonayo Katiba ya Zanzibar mbele ya sheria namba 8 ya mabadiliko ya Katiba, na kwamba, Katiba ya Zanzibar ndio “(The Grundnorm, which is the highest form of validity, being of the highest authority, providing efficient and affordable legal representation).

  Tatu, hata hiyo Mahakama ya Rufaa, nayo haina uwezo, wala mamlaka, wala haki Kikatiba ya kuitafsiri Katiba ya Zanzibar maana Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza katika kifungu cha 99 kinachohusiana na kazi na uwezo wa Mahakama ya Rufaa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezi kutafsiri Katiba ya Zanzibar. Kwa maneno mengine, Katiba ya Zanzibar inajitegemea, na kwa mantiki hiyo, Wazanzibari watahukumiwa kwayo tu, na si kwa sheria ya mabadiliko ya Katiba wala nyengine yo yote ile.

  Nne, pamoja na vitisho vilivyomo kwenye kifungu cha makosa na adhabu ndani ya muswaada na sheria ya mabadiliko ya Katiba, bado sheria hiyo haiwezi kuwa JUU ya Katiba. Na sheria yo yote, itakayokwenda kinyume na Katiba, sheria hiyo pia inakuwa batili (unconstitutional). Tunakusudia kusema kwamba, hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, yenyewe, ambayo bado inatumika hadi sasa, inadhamini UHURU wa wananchi kutowa mawazo na maoni yao kwa uhuru kabisa. Kifungu cha 18, kinachohusiana na haki ya uhuru wa mawazo kinaeleza: “Kila mtu – (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake”. Aidha, kifungu kinachofuata cha 19-(1) nacho kinaeleza: “Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo”. Pia, Katiba hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano, Sehemu ya Tatu, inayohusiana na haki na wajibu muhimu, inaeleza kwenye kifungu cha 13-(2) kuwa: “Ni marufuku kwa sheria yo yote iliyotungwa na mamlaka yo yote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lo lote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake”. Neno ubaguzi, linatafsiriwa na Katiba hiyo hiyo ya Muungano kwenye kifungu cha 13-(5) kuwa ubaguzi ni pamoja na kunyima haki ya maoni ya kisiasa. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba inakwenda kinyume na Katiba kwa kuikana haki hiyo muhimu ya maoni ya kisiasa.

  Tano, UHALALI wa sheria ya mabadiliko ya Katiba hauwezi kupatikana kwa kupitishwa na Bunge pekee. Ni LAZIMA sheria hiyo ya mabadiliko ya Katiba, pia ipitishwe na kuridhiwa na kukubaliwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
  Baada ya hoja na maelezo hayo, ni ukweli usio na shaka kuwa, sheria ya mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar, na kwa ajili hiyo, Wazanzibari Kikatiba, tunao uhuru na haki ya kutoa maoni yetu bila ya hofu wala woga; kama ambavyo Serikali yetu nayo kupitia Katiba ya Zanzibar, ina wajibu wa kudhamini uhuru huo. Ikiwa ni kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba, na si ule Muungano wa Katiba pia ni haki yetu ya Kikatiba. Zama za kutishana na kupigana zimekwisha. Hata Rais Kikwete katika hotuba yake alilisema hilo, na namnukuu: “Kwa upande wa mchakato wa kupata Katiba mpya, nawasihi Watanzania tujiandae kwa maoni ya kutoa kwenye Tume ya Katiba mara itakapoanza kazi. Tutofautiane bila kupigana”. Mwisho wa kunukuu. Tunamtaka Rais Kikwete atembee juu ya kauli yake hiyo kama ambavyo nasi tutatofautiana kwa misingi ya HOJA bila ya kupigana.
  Jamhuri ya Watu wa Zanzibar KWANZA!
   
 2. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  umetumwa?
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  kujitenga mnaogopa,mmebaki lakini kelele kila siku!!!huku jussa anasema uzini wameshindwa sababu kuna wakristo wengi na wabara..hamueleweki nini mnataka,hivyo ni halali kuendelea kutawaliwa na bara kiuchumi na kijeshi(maana hamna jeshi yakhe)
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  We bora ungeendelea kukaa korokoroni tu.
  Unapenda sana chokochoko.
   
 5. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  'Wanasharia' waliobobea lol........ Umemsikia mdini mwenzio na muhindi/mwarabu mwenzio Jusa alivyoropoka jana.... Endeleeni na ubaguzi na udini wenu, fahamuni come 2015 hakuna jiwe litasalia juu ya lingine.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimeyapenda sana maneno hayo.

  Jamhuri ya watu wa Znz laazima ipatikane.
   
 7. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Watafahamu kama hawaelewi hawa Watanganyika,tunamsubiri huyo sitta aje na makaratasi yake tumueke kitako.
   
 8. W

  We know next JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mhh yameanza tena haya... napita tu!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  @Barubaru, sisi huku Singida tuligundua mapema kuwa muswada wa mwaka jana ulikuwa na matatizo makubwa, usingefaa kabisa kwa mkoa mwetu wa Singida ukizingatia kuwa tunajua vema mipaka ya mkoa wetu, rasilimali na mambo mengine muhimu. Ndio maana tukamwambia mbunge wetu Mh Tundu Lissu ule muswada ni mbovu na asiukubali kabisa. Tunashukuru amefanya hivyo na kwa kuungana na wenziwe toka CHADEMA walifunga safari kuonana na rais na sasa marekebisho yamefanyika. Sio perfect lakini haki zetu kama 'MKOA' hazijaminywa sana. We can live with that!

  Sasa kwa 'Nchi' ya Zanzibar, naamini kuna wabunge zaidi ya 40 kwenye bunge lile lile aliko mbunge wa 'MKOA' wetu wa Singida. Kwa bahati nzuri nilipata fursa ya kuangalia mjadala wa muswada mwaka jana na mwaka huu (wakati wa marekebisho).

  Tukianza na mwaka jana, mara baada ya mbunge wa 'MKOA' wetu wa Singida Mh Tundu Lissu kueleza mapungufu ya muswada ule, wabunge wa nchi jirani yaani ZANZIBAR walisimama mmoja baada ya mwingine wakamtukana sana tena sana huku wakisema muswada safi! Yuko mmoja alifikia hatua ya kumkashifu jina lake (Lissu) kwa kusema kuwa lina maana 'nahisi' mbaya huko Zanzibar. Kwa kumbukumbu zangu, hawakuwa na tatizo na ule muswada na walishangazwa/kuchukizwa sana na hoja za kuukosoa maana kwao ulikuwa muswada mzuri! Hakuna pahala walisema kuna mgongano wa vifungu vya sheria sio no 1 wala no 2 au hata no 8. Muswada murua!

  Mambo hayakuishia hapo, mara baada team Lissu kuonana na rais, nayo team ya CUF akiwemo Jussa na Mnyaa (wote toka Zanzibar) walienda kuonana na rais na kutoa mapendekezo. Jussa tunaambiwa kasoma sheria hivyo naamini sheria No 8 anaijua vema lakini ndio hivyo tena, inawezekana juice ya magogoni ilifanya kazi ya ziada!

  Kwa kumalizia Barubaru, kumbukumbu za bunge (hansard) zinaonesha muswada/marekebisho ya sheria ya kutunga katiba mpya yameungwa mkono na wawakilishi wa wananchi yaani wabunge toka mkoa wetu wa Singida, na Tanzania bara yote PAMOJA na wale wabunge wa Zanzibar. Labda nikuulize uliwasiliana na wakina Mnyaa, Hamad Rashid, Sanya, na wengine kuhusu 'potential' problem na muswada/sheria ya kutunga katiba mpya? Nirudie sisi tuliwasaliana na mbunge wetu wa mkoa wa Singida ili kulinda kila kilicho ndani ya mipaka yetu ya Mkoa wa Singida. Wewe na wenzake mulifanya nini? posho walilipwa lakini!
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wewe endelea kupayuka kwenye keyboard huko huko doha

  in Tz mainland no one loose anything if the union gets fragility
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Hatakuwa na jibu la maana hapo maana umempa za usoni !
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kama mlijua kuna tatizo kwenye muswada kwa nini mliupitisha?
  kama mnaweka mitego, itawasaidia?

  Kama mnaitaka Znz yenu, kwa nini wale wawakilishi wenu kwenye bunge la JMT huwa wa kwanza kuwarushia maneno makali yeyote anayesema kwamba huu muungano una mushkeli?

  You dont know what you want, you have never, and you will never know what you want.
  And for this, CCM will continue to use Znz kama tank za akiba ya maji ya Mvua, pale wanapotaka kupitisa vitu kirahisi ndani ya chama chao, they get a majority vote from you - they know mtasema ndiyooooo!!!

  Reserve tank - rain water harvesting, that's what you are.

  Na huo ndio ukweli MCHUNGU.
   
 13. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa Kamanda.Muungano hauna maana tena...kwanza wenyewe wameshakufa
   
 14. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jitengeni haraka mkaungane na wanajangwa wenzenu hatuwahitaji. We are tired!!!
   
 15. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huyu Makame Silima kweli hamnazo. Jiulize ni lini Wazanzibari waliulizwa kuhusu Muungano in the first place, kabla ya kuuliza kuua Tanganyika!

  Sera ya CCM ni Serikali 2 kuelekea Serikali 1. Ndiyo maana ikaamua kuua kwanza Tanganyika, halafu kitachofuata ni Zanzibar kufa na kubaki na Serikali moja ambapo Ugunja na Pemba itakuwa mikoa kama DSM na Pwani.

  Kwakuwa Wazanzibari mnakubaliana na hilo ndiyo maana CCM na CUF wamefunga ndoa kutengeneza SUK. Ndiyo maana CCM na CUF walipitisha kwa nguvu moja mabadiliko hayo ya 8 ya katiba mpya.

  Na kwakuwa Wazanzibari mnakubaliana na hali hiyo ndiyo maana Jumapili mmechangua Raza wa CCM kuwa mwakilishi wa Uzini kwa 91%.

  Wazanzibari mmekuwa kama mwanamke asiyetosheka kila kuchwao kumlalamikia mme wenu Tanganyika, lakini ikifika usiku (mkienda Dodoma) penzi mnatoa tena kiulani.
   
 16. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Yuko wapi huyo makame silima ? Au unaongea baba yako nyerere
   
 17. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Ohaa Yakhee
  Walio upitisha mswada wa katiba sio Cuf wala wabunge kutoka zanzibar,walio upitisha mswada na ccm,katiba bunge la muungano wazanzibari wasiopungua sitini,waliobakia zaidi ya mia tatu ni kutoka tanganyika,hivi wewe kwa aliki yako wazanzibari ndani ya bunge watali chalenge bunge na kuuzuiya mswada ?

  Haya tunaambiwa kuwa wabunge kutoka zanzibar ni theluthi mbili katika bunge,ukiangalia katika hawa hawa walitoka zanzibar kuna cuf na ccm,wa ccm wanafata sera ya ccm na cuf wanasera zao,sizani kuwa wabunge wa ccm watakwenda kinyume na mswada huo,kwani huo mswada wa katiba haukuundwa ki democracy bali umeandikwa zaid kisiasa na ubinafsi,zaid ccm kujilinda katika hadhi yao ya uwongozi.

  Haya unasema cuf imekula ndoa na ccm zanzibar,wewe kweli hupo dunia hii na hujui nini siasa,hujui nini serikali,na hujui hio serikali ya SMZ yenye mfumo wa umoja wa kitaifa inaendeshwa vipi.

  Kilichounganishwa ni ASP na TANU tu,bado kuna cuf na ccm ndoa iliopo zanzibar ni katika uwongozi wa madaraka na sio ule wa kisiasa,wamegawana wizara tu,na katiba ya smz,inasema kuwa chama chochote kitakacho shinda ndio kitakaongoza sera zake.

  Chombo ambacho chenye uwezo wa kupinga mswada wa katiba au kuvunja muungano,au kupinga suala lolote la muungano ni baraza la wakilishi tu ,ambalo ndio lenye nguvu zote,lakini kutokana na udhaifu wetu sisi wazanzibari,walio shika mpini wa baraza la wakilishi,ni rais wa zanzibar,spika wa baraza la wakilishi,Jaji mkuu wa zanzibar,hawa wote ni wana ccm na wameapa kuulinda muungano na kulinda katiba ya ccm,kwa maana hiyo wazanzibari tuna kazi kubwa katika kuikomboa zanzibar kupata haki zetu ambazo tunazo nyimwa kitaifa na kimataifa.
   
 18. T

  Taso JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Unakuza bure kitu kidogo mno.

  Wapigania haki au watu wa jamii zinazojaribu kumng'oa dikteka au wapigania uhuru wakati wa kumpinga mkoloni ndio walikuwa wanaongea na kuimba nyimbo za ipo siku, lazima tutapata nchi yetu, kwa sababu mkoloni alikuwa hataki kukuachia, kwa hiyo ulibaki unaota na kupambana na kuimba na kusali. Kesi yetu hii tofauti sana, ndogo sana, ni kiasi cha Rais za Zanzibar kutangaza, au wabunge wa Zanzibar kwenda Dodoma, kusimama kwenye kiti na kusema unanimously hatutaki Muungano. Simple as that. Nothing more.

  Mbona kitu kidogo sana?

  Nani kawashikilia kwa nguvu?

  Kwa nini hamjiondoi?
   
 19. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,593
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Kama zanzibar mnataka nchi yenu, si mumshinikize raisi wenu shain aachane na muungano na baraza la wawakilishi, mbona hilo linawezekana sana?.
  Kabla ya kuwakaba watanganyika, wakabeni viongozi wenu wakuu, au susieni harakati zote za kisiasa huko zenji mpaka pale mtakapojitoa katika muungano.
  Haiingii akilini, kura za raisi wa jmt mnapiga, kura za wabunge wa jmt mnapiga, sasa kama mnataka zanzibar yenu kwa nini mshiriki michakato yote hii inayoipa legitimacy jmt?

  As the matter of fact, tanganyika haipungukiwi chochote na nyinyi kujitenga, kama kweli mpo siriasi nadhani ni vyema mkaanza mchakato kwa hekima na busara ili tutengane kwa amani.
   
Loading...