Sheria mpya za TCRA : Vipindi vya mapenzi kama Ala za Roho na Chombeza Time kuanza saa 6 usiku

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,599
217,991
Kumbe sasa vinatakiwa kuanza saa 6 usiku badala ya saa 4 usiku , labda uchumi wa kati umesababisha watoto kuchelewa kulala .

Instagram media - CDw86kxhUX4 ( 509 X 640 ).jpg
 
Mkuu

Naona hii ya Bia yetu imerudi tena.... Natumai ya Kawe Alumni zamu yake itakuwa next month...

Vp mzigo kwaajili ya general election wameshawawekea nini?????

Sent using Jamii Forums mobile app
Anapoteza muda wake tu,watanzania weelewa kuliko yeye.Akaya seme hayo maneno kwenye umati wa watu.aone litakalo mkuta.
Huyo jiwe mwenyewe hawezi sema chochote maana anajua wachawi wa watanzania ni CCM wenzake.
 
Wapige marufuku vipindi vya michezo asubuhi.

Asubuhi ni muda wa kufanya kazi na kuzalisha, aatu wakiamka ni kusikiliza micuezo toka asubuhi hadi sa 7, watafanya kazi sa ngapi?

Michezo ni burudani, burudani ina mchango wa kawaida kwenye pato la taifa, hata Marekani ambako wameendelea michezo na burudani mchango wake ni 15% lakini watu hawaamki sa 12 na vipindi vya michezo hadi sa 7 mchana.

Vipindi vya michezo kuwekwa asubuhi ni kuzidi kulemaza nguvu kazi. Michezo iwe jioni baada ya kazi, sio muda wa kazi.
 
Kumbe sasa vinatakiwa kuanza saa 6 usiku badala ya saa 4 usiku , labda uchumi wa kati umesababisha watoto kuchelewa kulala .

Mzizi wa tatizo la msingi upo kwenye akili ndogo kuzidi kuaminiwa kuzitawala akili kubwa. Nobody cares about the essential inputs and throughputs, but only expectedly outputs.

Katika mazingira ya sasa huwezi kukumbatia mikakati ya kibiashara ya "supply driven rather than demand driven" kwa kuwa siri kubwa za walaji ktk soko ni kuwa wanao uchaguzi wao binafsi, unaoendeshwa na nguvu za utashi wa watu na mahitaji yao halisi kuhusu bidhaa ama huduma waitakayo, na pia inategemea inapatikana kwa wakati gani.

Soko kuratibiwa kiholela, ama kutawaliwa na hisia na mihemuko ya watu wasiokuwa taaluma za kibiashara ama kiuchumi, ni kutaka kuliua soko na watu kuhamia ktk vitu mbadala. Mtu huitaji kitu ambacho roho inakipenda, huwezi kumlazimisha kuchagua kitu asichokipenda.
 
Hii Nchi ilifuga uchafu mwingi sana

Tcra imeturudisha kwenye maadili
Na hii ndo shida kuu hapa nchini kwetu... KILA MMOJA YUKO BIZE KUSEMA KAMA ULIVYOSEMA... Wengine utawasikia... nchi ilikuwa na wezi sana, nchi imeibiwa sana etc.. KATIKA HAO WANAOSEMA HAYO, HAKUNA HATA MMOJA ANAYEMTAJA MWIZI....!!!

Kama ambavyo na wewe umesema kuwa, nchi ilikumbatia uchafu mwingi... NANI ALISABABISHA..!? Nani alikumbatia huo uchafu..!? SHIHATA..!? HABARI..!? MAELEZO..!? MARAIS WALIOPITA..!? CCM..!? CHADEMA..!? au nani..!?

TAJA TATIZO NA WALIOSABABISHA
 
Wapige marufuku vipindi vya michezo asubuhi.

Asubuhi ni muda wa kufanya kazi na kuzalisha, aatu wakiamka ni kusikiliza micuezo toka asubuhi hadi sa 7, watafanya kazi sa ngapi?

Michezo ni burudani, burudani ina mchango wa kawaida kwenye pato la taifa, hata Marekani ambako wameendelea michezo na burudani mchango wake ni 15% lakini watu hawaamki sa 12 na vipindi vya michezo hadi sa 7 mchana.

Vipindi vya michezo kuwekwa asubuhi ni kuzidi kulemaza nguvu kazi. Michezo iwe jioni baada ya kazi, sio muda wa kazi.
Mkuu siasa imepigwa marufuku labda kusifu juhudi za awamu. Watu hawana pa kutolea malalamiko yao hasa ya dhidi ya serikali vinginevyo una risk mengi. Sehemu pekee iliyobakia kwa Wabongo ku release tension ni kwenye michezo. Ndio establishment ilipotufikisha

Sasa unatoa wito hata huko napo wazuie! Unataka Radio na TV muda wote ziwe zunasifu na kuabudu!!!!? Hiyo sio sawa.
 
Kumbe sasa vinatakiwa kuanza saa 6 usiku badala ya saa 4 usiku , labda uchumi wa kati umesababisha watoto kuchelewa kulala .

Naunga mkono suala la kuvipangia muda wa usiku tena usiku mwingi vipindi vyenye maudhui ya ngono maana kwakweli imekua ni kero na kinyume na utamaduni wetu. Baadhi ya hivi vipindi huwezi kuvisikiliza ukiwa na mtu unayeheshimiana nae!

Wasiishie kwenye vipindi bali hata nyimbo za baadhi ya wasanii sio za mapenzi bali za kuhamasisha ngono tena ngono zembe. Nyimbo hizi zina mdhalilisha mwanamke na kuhujumu maadili ya uma hasa vijana na watoto
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom