Sheria mpya ya vyama vya siasa itaua vyama vyote ikiwemo CCM yenyewe

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
803
1,000
Katika mjadala unaoendelea wa sheria mpya ya vyama vya siasa,watu wengi wanaitazama kwa upande mmoja tu wa njama ya watawala kuua vyama vya upinzani kwa kutumia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Ukweli ni kuwa chama cha mapinduzi CCM nacho kitaathirika sana kwakuwa Sheria hiyo imelenga kuwafutilia mbali vijana wa CCM ya Asili.

Vijana wote walioaminiwa na Rais Jakaya Kikwete,wametungiwa sheria ya kuwaondoa kwenye siasa na kuhakikisha hawapati jukwaa lolote la Kufanyia siasa.

Katika sheria hiyo kipo kifungu kinachosomeka kuwa mwanachama atakaehama chama kwa sababu yoyote haruhusiwi kugombe nafasi yoyote mpaka uana chama wake katika chama kipya utimize miaka miwili.

Yaani Mtu akitoka CCM kwa sababu jina lake limekatwa na Polepole,basi akose kimbilio,maana hata akikimbilia upinzani huko haruhusiwi Kugombea.

Hapa kuna watu wamekusudiwa kushughulikiwa,si wengine bali ni vijana wa CCM ambao hawaridhishwi na jinsi nchi inavyoendeshwa.

Walengwa wakuu hapa ni wakosoaji kama vile.

1.Nape Moses Nnauye,huyu jamaa akalie kiti cha bunge kwa mara ya mwisho,kama sheria hii itapita basi Nape ndio basi tena,atastafishwa siasa .kwakuwa hakubaliki katika chama kutokana misimamo yake,na kwakuwa wanajua akihama atashinda ubunge na kuwa mwiba zaidi,wamemtungia na sheria inayomzuia kugombea hata kama atahama chama.

2.Bashe,huyu ni msumbufu sana kwa chama,wakishawahi kutaka kumfukuza chama lkn wakasoma alama za nyakati.

Bashe kama angefukuzwa kipindi kile na uchaguzi kurudiwa,ni wazi kuwa Bashe ngewashinda kwa chama kingine.

Sasa dawa yake ni kumvumilia ili 2020 apotezwe jumla,na dawa yake ni sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo itamzuia kugombea endapo atahamia chama chochote baada ya jina lake kukatwa.

3.Mwigulu Nchemba.
Huyu hawezi kurudi tena Bungeni,hii ni kutokana na kutoaminika kwa wakubwa kwakuwa ni miongoni mwa wafuasi wa Kinana.
Jimbo lake ameshawekwa Prof Kitila Mkumbo,na Mwigulu atake asitake atalazimishwa kumuombea kura Prof Kitila Mkumbo,Kama mwigulu ataumizwa na maamuzi haya na kuamua kuhamia chama chochote ili aendelee kugombea,basi atakutana na rungu la sheria mpya.

4. Obama Ntabaliba(Mbunge wa Buhigwe) Jimbo lake limeshakabidhiwa kwa Waziri wa fedha wa sasa Dr.Mpango.
CCM hapati nafasi na upinzani anabanwa na sheria mpya.

5.Daniel Nsanzugwanko(Kasulu Mjini)

Jimbo mpaka sasa analo Prof Ndalichako,akithubutu kuhama atakuwa kajifia kwakuwa kigezo cha miaka miwili katika chama kipya atakuwa hana,hivyo atakaa bench kuangalia bunge kwenye You tube...

Kwa kifupi kuna Orodha ndefu ya wabunge wa CCM ambao wanatiliwa mashaka kutokubaliana na vitendo vya serikali yao,na hawa wameshaorodheshwa majina yao kusubiri siku ya hukumu.

Na kwakuwa CCM mpya wanajua kuwa ni watu wenye ushawishi na wanaweza kuhama chama na kuchaguliwa tena na baadae kuisumbua serikali wakiwa huru(Upinzani) ni kwa msingi huo sheria mpya ya vyama vya siasa imeweka kizingiti ambacho kitawadhibiti wasichomoze.

Ni wakati wa Wabunge wa CCM na wabunge wa upinzani kuungana kuikataa sheria mpya,maana hiyo sheria mpya ndio kile KIBUYU alichosema Dr.Mwijage kuwa kinamaliza watu.

Msiruhusu kujiua kisiasa kwa kupitisha sheria inayowazuia msifanye siasa.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,198
2,000
Wamemlenga pia Maembe. Ndiyo maana hata mwito wake kwa katibu mkuu umewekwa kapuni.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,198
2,000
CCM wamekenua meno tu wamemlea nyoka pori ndani ya nyumba. Sasa amewakuza watoto aliowazaa yy, anaunda sheria ya kuwaondoa aliowakuta ndani ya nyumba.
 
kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
1,998
2,000
Ukiangalia vizuri ile sio sheria bali ni mkakati wa kundi au genge fulani kuyakomesha makundi mengine ili hili genge lijihakikishie kutawala watakavyo
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,970
2,000
Katika mjadala unaoendelea wa sheria mpya ya vyama vya siasa,watu wengi wanaitazama kwa upande mmoja tu wa njama ya watawala kuua vyama vya upinzani kwa kutumia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Ukweli ni kuwa chama cha mapinduzi CCM nacho kitaathirika sana kwakuwa Sheria hiyo imelenga kuwafutilia mbali vijana wa CCM ya Asili.

Vijana wote walioaminiwa na Rais Jakaya Kikwete,wametungiwa sheria ya kuwaondoa kwenye siasa na kuhakikisha hawapati jukwaa lolote la Kufanyia siasa.

Katika sheria hiyo kipo kifungu kinachosomeka kuwa mwanachama atakaehama chama kwa sababu yoyote haruhusiwi kugombe nafasi yoyote mpaka uana chama wake katika chama kipya utimize miaka miwili.

Yaani Mtu akitoka CCM kwa sababu jina lake limekatwa na Polepole,basi akose kimbilio,maana hata akikimbilia upinzani huko haruhusiwi Kugombea.

Hapa kuna watu wamekusudiwa kushughulikiwa,si wengine bali ni vijana wa CCM ambao hawaridhishwi na jinsi nchi inavyoendeshwa.

Walengwa wakuu hapa ni wakosoaji kama vile.

1.Nape Moses Nnauye,huyu jamaa akalie kiti cha bunge kwa mara ya mwisho,kama sheria hii itapita basi Nape ndio basi tena,atastafishwa siasa .kwakuwa hakubaliki katika chama kutokana misimamo yake,na kwakuwa wanajua akihama atashinda ubunge na kuwa mwiba zaidi,wamemtungia na sheria inayomzuia kugombea hata kama atahama chama.

2.Bashe,huyu ni msumbufu sana kwa chama,wakishawahi kutaka kumfukuza chama lkn wakasoma alama za nyakati.

Bashe kama angefukuzwa kipindi kile na uchaguzi kurudiwa,ni wazi kuwa Bashe ngewashinda kwa chama kingine.

Sasa dawa yake ni kumvumilia ili 2020 apotezwe jumla,na dawa yake ni sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo itamzuia kugombea endapo atahamia chama chochote baada ya jina lake kukatwa.

3.Mwigulu Nchemba.
Huyu hawezi kurudi tena Bungeni,hii ni kutokana na kutoaminika kwa wakubwa kwakuwa ni miongoni mwa wafuasi wa Kinana.
Jimbo lake ameshawekwa Prof Kitila Mkumbo,na Mwigulu atake asitake atalazimishwa kumuombea kura Prof Kitila Mkumbo,Kama mwigulu ataumizwa na maamuzi haya na kuamua kuhamia chama chochote ili aendelee kugombea,basi atakutana na rungu la sheria mpya.

4. Obama Ntabaliba(Mbunge wa Buhigwe) Jimbo lake limeshakabidhiwa kwa Waziri wa fedha wa sasa Dr.Mpango.
CCM hapati nafasi na upinzani anabanwa na sheria mpya.

5.Daniel Nsanzugwanko(Kasulu Mjini)

Jimbo mpaka sasa analo Prof Ndalichako,akithubutu kuhama atakuwa kajifia kwakuwa kigezo cha miaka miwili katika chama kipya atakuwa hana,hivyo atakaa bench kuangalia bunge kwenye You tube...

Kwa kifupi kuna Orodha ndefu ya wabunge wa CCM ambao wanatiliwa mashaka kutokubaliana na vitendo vya serikali yao,na hawa wameshaorodheshwa majina yao kusubiri siku ya hukumu.

Na kwakuwa CCM mpya wanajua kuwa ni watu wenye ushawishi na wanaweza kuhama chama na kuchaguliwa tena na baadae kuisumbua serikali wakiwa huru(Upinzani) ni kwa msingi huo sheria mpya ya vyama vya siasa imeweka kizingiti ambacho kitawadhibiti wasichomoze.

Ni wakati wa Wabunge wa CCM na wabunge wa upinzani kuungana kuikataa sheria mpya,maana hiyo sheria mpya ndio kile KIBUYU alichosema Dr.Mwijage kuwa kinamaliza watu.

Msiruhusu kujiua kisiasa kwa kupitisha sheria inayowazuia msifanye siasa.
Kama ilivyo amri inayokataza vyama vya siasa kufanya siasa na kutokuihusu CCM ndivyo na sheria hiyo itakavyokuwa. CCM imekuwa ikikiuka mambo mengi sana ikiwa na wachina kushiriki siasa bila hatua yoyote kuchukuliwa ndivyo itakavyokuwa kwenye sheria hiyo, haiwezekani nikuteue mimi kisha unihukumu mimi.
 
Nyasirori

JF-Expert Member
May 3, 2009
318
500
Sisi chama tawala haya hayatuhusu maana tunanaweza kuamua tu kwa kutamka na swala likawezekana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom