sheria mpya ya mafao yazidi kuleta balaa uzalishaji wasimama kabisa KMCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sheria mpya ya mafao yazidi kuleta balaa uzalishaji wasimama kabisa KMCL

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Muangila, Aug 1, 2012.

 1. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Uzalishaji ndani ya mgodi wa Bulyanhulu KMCL umesimama kabisa kuanzia jioni ya leo tar.01.08.12 kufuatia wafanyakazi kutaka mpaka wapatiwe ufafanuzi kuhusu mustakabali wa fedha zao walizochangia NSSF na PPF hali hiyo imeanza jana baada kikao kati ya mwakilishi kutoka SSRA na wafanyakazi kuvunjika hali hii imepelekea mwajiri kusimamisha uzalishajikwa saa 48 mpaka kieweke.Wakati huo huo makamu wa rais wa BARRICK duniani ameingia nchini kwa mazunguzo na serikali kuhusiana na sheria hii.
   
 2. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ngoja tuone lazima wataachia serikali legelege hata hawajui wanafanya nini ...mkuuu wa mkoa wapi na wapi na waalim..nashindwa hata kuelewa nani anafanya nini.......yaani wamejenga majumba kwa faida ya mishahara yetu lkini wanataka kutudhulumu
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Celebrating 50 years of Independence!
   
 4. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  dah! kwanini hawakumuuliza dhaifu leo swala la mafao? wahariri wetu nao!!!
   
 5. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hata iweje hiyo sheria haiwezi kubadilika. JK ameshakula pesa yote kwenye hiyo mifuko ya jamii, ikikubaliwa kubadilisha sheria, lazima JK adhalilike, itakuwa ni sawa na kumvua nguo adharani...
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ila ni kwa nini wagome hawa wa MIGODI PEKEE? wafanya kazi wengine wako wapi? Hii nchi mageuzi yatacheleweshwa na WAFANYAKAZI, haiwezekani ishu siriazi kama hii, wanagoma wafanya kazi wa MIGODI PEKEE,
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mbona wameanza salimu amri migodini?
  Nimeona waraka leo kwa ajili ya mgodi wa GGM, ukisema fao hili litakuwepo kwa wale waliosaini mikataba kabla sheria hii haijapitishwa, hii ni kutokana na mikataba na mazingira ya kazi ya watu wa GGM.

  Pia waraka huo umeendelea kueleza kuwa, wafanyakazi wa migodi watachagua mfuko wa kujiunga unaotoa fao hilo(nimesahau kidogo jina)

  My take, wanaweza wakasalimu amri kwa watu wa migodini.

  Nitautafuta waraka huo niuweke hapa.
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  kwa wafanya kazi wengine inakula kwao, make wafanya kazi wengine ni kama hawana uchungu na hizo pesa na wanabakia kulalamikia mitaani tu,
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mazingira ya kazi ya migodi ni magumu sana.
  Afu huwa wagumu kweli kuelewa sijui kwa nini, huchukui hata sh.100 ya miner bure na wana solidarity.

  Si rahisi mtu kuwa 'miner' wa mgodi wa underground kwa miaka 25.

  Labda wengine wanaona wanaweza kaa kazini kwa miaka angalau 30.

   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  Kampuni ya African Barrick Gold imeusimamisha mgodi wake wa Bulyanhulu kwa masaa 48, kuanzia jioni ya August 1st. Uongozi wa Bulyanhulu umechukuwa uamuzi huo jioni hii baada ya mgomo wa siku mbili wa wafanyakazi. Mgomo huo ambao ulianza jana asubuhi July 31st ulisababishwa na sheria ya kufuta fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Baada ya wafanyakazi kuona uongozi wa Barrick Bulyanhulu umelala sana na hakuna jitihada zozote za kupata official reports from SSRA. Jana asubuhi wafanyakazi wakaamuwa kuanzisha mgomo mpaka hapo watakapoitiwa watendaji wa juu wa SSRA ili waelezwe na wafafanuliwa juu ya mafao yao na wao kutoa kilio chao juu ya hiyo sheria mpya. Baada ya wafanyakazi kukusanyika na kujadili. Ilionekana ni bora aje mbunge Jafu ambaye anakusanya maoni, au Waziri wa Kazi. Lakini uongozi ulifanya jitihada na kumleta Afisa uhusiano wa SSRA toka Dar office. Afisa uhusiano aliondoka bila kutowa jawabu la kuridhisha kwa wafanyakazi. Hivyo wafanyakazi waliamuwa waendelee na mgomo mpaka atakapoletwa Jafu au waziri mwenye dhamana. Hivyo wafanyakazi wakaendelea na mgomo mpaka wakati wa kutoka jioni. Jioni waliukabidhi mgomo kwa wafanyakazi wa zamu ya usiku. Zamu ya usiku waliupokea mgomo kwa mikoni miwili na kuahidi mgomo watauendeleza mpaka asubuhi na kuwarudishia waasisi wa mgomo huo. Kweli bwana, pamoja na vitisho vyote toka utawala, lakini jamaa wa usiku waliendelea kukaza uzi mpaka asubuhi. Ilipofika leo asubuhi, waanzilishi wa mgomo walikuja kupokea mgomo wao. Shift ya leo asubuhi iliendelea na mgomo huku mijadala na uongozi ikiwa inaendelea. Lakini wafanyakazi wakashikilia uamuzi wao wa kuonana na Jafu ama waziri mwenye dhamana. Ulipofika muda kama wa saa kumi na moja jioni, uongozi ukatoa taarifa kwa wafanyakazi wote. Kwamba uongozi umeamuwa kusimamisha shughuli za uchimbaji kwa masaa 48 kuanzia muda huo wa jioni. Wafanyakazi ambao ilibidi waingie kwa zamu ya usiku jioni hii hawakuingia kazini. Na waliokuwepo walirudi nyumbani kusubiri kwa masaa 48. Nje ya geti wafanyakazi walikuta police wakiwa wametawanywa. Lakini hakukuwa na tukio lolote la vurugu ama utumiaji nguvu. Wafanyakazi waliingia kwenye ma-bus ya kampuni na kurudi nyumbani kwa amani.
  Source: Shuhuda wa tukio.
   
 11. l

  laboratory Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DHAIFU alisaini hakujua kuwa ,alishakula ten percent ya BARRICK,na kila cku anaenda mikono nyuma UNITED STATES,,kuomba,,sasa leo BARRICK wanashindwa kupata DHAHABU,, mpaka CHIEF EXECUTIVE OFFICER WA BARRICK,, kaja ,kujua kumetokea nini?mpaka wafanyakazi wagome?wanagundua ni ujinga ,wa GOV DHAIFU,,sasa itabidi sheria waibadili tu ,,bila hivyo DHAHABU HAKUNA ,na hela zao walishazila na wanaendelea kuzila..
   
 12. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mazingira ya Kazi ni magumu sehemu nyingi sana, Cheki mfano wa hivi viwanda vy wahindi na wachina Wafanyakazi wana mazingira magumu sana, na ni kwa nini ilegezwe kwa wafanya kazi wa sehemu fulani tu, Mimi nazani kuna presha ya wamiliki wa Migodi na watakuwa wametishia kustisha uchimbaji,
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa kama mpaka makamu wa raisi wa Barrick anakuja then ujue huo mgodi utakuwa ni kama Cash Cow kwao!
   
 14. m

  maswitule JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,385
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Napendekeza na sie wengine tugome kuanzia kiwanda cha mchina urafiki, madereva wa mabasi, malori nk. mgomo uanzie Ubungo terminal. pendekezeni tarehe wakuu
   
 15. The last don

  The last don JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Hawa wazushi wa SSRA wao wamekuja na tamko hili . SSRA_1.jpg
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Yani ndio hicho nashangaaa,yani sector nyingine wamekula jiiiii yani hawana wasiwasi.
   
 17. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa kugoma ni vigumu sana na kumbuka hii Sheria inawahusu sana wafanya kazi wa sekita Binafisi make kwa upande wa serikali wao hii kitu wanaijua kabisa,

  Hakuna Umoja na hakuna wa ku initiate huu mgomo kwa sababu Sekta binafisi nyingi hazina Vyama, Chukulia mfano wa wafanya kazi wa Mashirika/NGOs za ndani na za nje ya Nchi mfano, Waorld vision, Plan international na kazalika, so inakuwa ngumu

  SOLUTION NI KILA IDALA KUGOMA KIVYAO, WA KIWANDA CHA WACHINA WANAGOMA KIVYAO, wa kiwand wahini wanagoma kivyao
   
 18. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Bora mimi mjasiriamali, sina fao lolote la kujitoa ila nahurumia staff wangu ninaowalipia vijisarafu kila mwezi maana biashara ikidoda nafunga nahama nchi wabaki na NSSF yao
   
 19. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  hii sheria ni kandamizi idara zote! Si migodi peke yao. Mbaya zaidi mbunge gamba aliyeipitisha ndo analeta mbwembwe! Upuuzi mtupu
   
 20. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi wa migodini hawaitaki kabisa hii sheria mpya, na lazima itabadilishaw. maana haina manufaa yoyote kwa mfanyakazi!
   
Loading...