Sheria mpya ya madini wadau mpooo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria mpya ya madini wadau mpooo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MARIJANI, Apr 18, 2010.

 1. MARIJANI

  MARIJANI Member

  #1
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  [​IMG]
  Tanzania imepoteza rasilimali ya madini nyingi na mapato mengi huku umasikini wa wananchi ukiongezeka. Sasa sheria Mpya ya madini inakuja Bungeni tarehe 19 na 20 April 2010 kwa hati ya dharura ambayo wabunge wanatakiwa kujadili na kupitisha siku hiyo hiyo! Tunauliza, kwanini hati ya Dharura bila ushirikishaji na majadiliano ya kutosha?

  Ewe Mbunge, Hatima ya Nchi hii sasa ipo mikononi mwako, kataa kuburuzwa kwa masilahi ya wengine, Jadili kwa umakini, pinga usiri, sheria kandamizi na nyonyanji ya nchi. Tanzania tajiri na yenye ustawi inawezekana!

  Tangazo Hili linaletwa kwenu na:
  Agenda Participation 2000 kwa ushirikiano na

  Revenue Watch Institute (RWI)
  Ghorofa ya Tano
  Ubungo Plaza
  Simu: +255 22 2460036/39
  Sms + 255 782 550379/ 0758318914


  SOURCE MICHUZI
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Naogopa hii maneno ya kupinga huu muswada inakuja kwakuchelewa!...Lakini , kuna uharaka gani wa kuleta muswada huo kwa dharula hivyo, wakati madini yako huko chini kwa mamilioni ya miaka?...Je muswada huo una maslahi ya kiasi gani kwa mtanzania, au ni njia ya haraka ya kupatia fedha ya kampeni?..?
  KUWENI MACHO ENYI WABUNGE, MUSITUUZE KWA BEI CHEAPER, kisa mnataka kupitishwa kwenye term ingine!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  NImeiona hiyo draft bill, haina mabadiliko ya maana na ya msingi. Nadhani kilio kikubwa ni kuhakikisha kuwa rasilimali madini inainufaisha nchi, hilo halijafanyika kupitia muswada utakaowasilioshwa kesho. Sidhani kama kuongeza mrahaba (au mrabaha sijui kiswahili sahihi ni kipi) kutoka asilimia 3 hadi 4 kutaifanya nchi inufaike sana. nadhani yalitakiwa mabadiliko makubwa katika umiliki wa na udhibiti wa rasilimali hii, hilo halijazungumziwa kiundani katika muswada mpya.
  Kuhusu kupinga, nafahamu kuwa kwa muda mrefu wanaharakati wamekuwa wakipigia kelele suala hili la madini kunufaisha nchi. Serikali imefanya uhuni kwa kuahidi kwua italifikiria hilo katika mabadiliko ya sheria. Kwa muda mrefu Ngeleja na wizara wamekaa ba hii bill bila kuiweka hadharani. Wanaharakati wengi wameipata this weekend
   
 4. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kuna kila dalili ya mchezo mchafu hapa. Nakumbuka ule msemo usemao "Mali ya mjinga huliwa na mwerevu"
   
Loading...