Sheria Mpya ya Fao la kujitoa (Withdrawal benefits) ya 2015 kwenye mifuko ya jamii ni pigo

Igniter cord

Member
Apr 27, 2015
81
26
Ndugu "wafanyakazi na wajasiriamali"...kwa heshima kubwa nawaletea hoja ambayo inagusa mstakabali wa maisha ya kila anayechangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (Social Security Funds) yote bila kujali ukubwa au udogo wa mfuko husika.

Kifupi ule mpango dhalimu wa mwaka 2012 ulioandaliwa na SSRA (Social Security Regulatory Authority) wa kuondoa "FAO LA KUJITOA (WITHDRAWAL BENEFITS)" ulipokwama, sasa wameibuka tena J1 ya tarehe 25 April 2015 kwamba sasa kwa kila atakayejitoa kwenye mfuko wowote wa hifadhi ya jamii atakatwa 3.6% ya mafao yake kwa mwaka huku makato hayo yakizidishwa kwa idadi ya miaka iliyobaki kufikia umri wa lazima wa kustaafu ambao ni miaka 60.

Kwa hesabu rahisi; kama mtu ana jumla ya sh 20,000,000 (milioni ishirini), halafu kazi aliyokuwa anaifanya imeisha, mathalani wale ndugu zetu wanaofanya kazi migodini (mfano, uchimbaji wa madini unapokoma kutokana na madini kwisha na makampuni kuondoka nchini)....mtu huyu kama akitaka kujiondoa kwa sababu sasa hana kazi tena na akiwa na umri wa miaka 35 (thelathini na mitano), hivyo kwa mujibu wa sheria hii mpya, atalazimika kukatwa sh. 20,000,000x (3.6%)x (25 years - ambao ni umri uliosalia kufikisha miaka 60); hivyo atakatwa jumla ya sh. 18,000,000 (milioni kumi na nane) na yeye kuambulia malipo ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) tu.

Kutegemea na kila mtu ana kiasi gani kwenye mfuko wa jamii husika na kutegemea pia na umri aliobakisha kufikia miaka 60, pindi anapoamua kujitoa anaweza kujikuta anakatwa pesa yote na hata kudaiwa.

Kazi kwenu ukweli ndio huu na taarifa hii ni kama nilivyo inukuu kwenye gazeti la "The Guardian la tarehe 25.04.2015", Sijui huyu Irene Isaka -mkurugenzi wa SSRA katumwa na nani?

Kama waliokopa fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii wameshindwa kuzirudisha, chonde chonde wasituletee uhayawani wao kwenye pesa tulizovuja jasho letu ambazo sisi tusiojua hata kama tutafika umri wa kustaafu tukiwa hai tulazimishwe kuzisubiri hizo pesa tukiwa makaburini.


The Social Security Regulatory Authority (SSRA) has said that 3.6 percent of potential earnings will be deducted from workers' pensions who opt to withdraw before retirement age.

SSRA Director General Irene Isaka said in a statement that workers' pension will be deducted for 0.3 per cent each month and thus equal 3.6 per year for those who opt to drop before the retirement time and not 18 per cent as it has been claimed.

The percentage will be calculated for all the remaining years before attaining age of 60 years, which means that for a worker opting to withdraw at the age of 58 the deduction will be 7.2 percent, "which is different with the one who withdraws at the age of 59 whose deduction will be 3.6 percent while who withdraws with 57 the deduction will be 10.8 per cent."

Thus for one who withdraws at the age of 55 the deduction will be 18 per cent for all the five years.

SSRA explained that before the regulations workers who opted to withdraw obtained 28 per cent more as compared to who withdraw on retiring on time.

The director general claimed that they involved all stakeholders including the government, employers and trade unions when making the new regulation, something that many union quarters dispute.

"The fact is that section 13 of the Pension Benefits (Harmonization) Rules of 2014 provides for a discount of 0.3 per cent from the benefits of a member who retired between the ages of 55-59, while the discount ends when he or she reaches 60 years," said Ms Isaka.

Besides introducing the new pension calculation formula, she also unveiled the new rules.

Ms Isaka noted that all new members who joined the scheme from last July 2014 will be managed under the new benefits formula, but this applies only to members of the Local Authorities Pensions Fund (LAPF) and the Public Sector Pensions Fund (PSPF).

For members of other social security funds including the Parastatals Pensions Fund (PPF), the National Social Security Fund (NSSF) and the Government Employees Provident Fund (GEPF) the new regulations will be applied regardless of when they joined.

Isaka admitted the mandatory retirement age is 60, but there is room for employees to retire at 55 which the authority is now permitting the funds to deduct heavily those who use that option.

However the Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA) has criticised the regulations on the grounds that the formula disadvantages some retirees, who will receive reduced pensions.

Tucta President Gratian Mukoba has rejected the new regulation on terminal benefits calculation on the grounds that it is unconstitutional and reduces pension benefits by 50 per cent.

Mukoba said that the proposed formula would cut public servants' pensions by half, marking a significant change from the current legislation, where teachers receive generous payments from pension funds.

Ubungo MP John Mnyika told this paper that the government is creating a new conflict with workers in withdrawal of benefits as it did earlier.

He said the Minister for Labor and Employment should speak up immediately over the ongoing challenges before it causes a generalized workers' strike.

Mnyika called upon for the government and the Social Services Committee of the National Assembly to sit together with workers purposely for addressing the challenge instead of waiting until crisis breaks out.

The chairman of the Civic United Front, Professor Ibrahim Lipumba told the SSRA to stop the implementation of the regulation until they reach a consensus with workers.

In August last year the Labour ministry launched the new formula that will see pensions shoot up to 72.5 percent from the current 60 to 67 percent.

The minister said under the social security schemes' pensions harmonisation rules, some of the changes made include indexation of pension benefits to enable retired people to live decent lives as per Section 32 (a) of the relevant legislation, law number 8 of 2008.

Source: The Guardian
 
serikali ya CCM ni jinsi gan inaonekana imezeeka,mfano mfanyakazi wa mgodini anafanya kazi kwenye mazingira hatarishi ki-afya,mnakata hiyo pesa wakati hana uhakika wa kufikisha umri husika.naungana na wanaojuta kuwa watanzania
 
ila wameileta kipindi kizuri.!mwaka wa uchaguzi hii sheria wakiipitisha tu kabla ya uchaguzi itakua moja ya nyundo itakayotumika kuiangamiza CCM.kwani idadi ya wafanyakazi wa sekta binafsi na wajasiliamali wanaochangia mifuko ya jamii ni kubwa
 
Kwani hili suala halitarudi tena Bungeni,najua Mh
Mnyika na Kafurila na ukawa wotw kiujumla hawawezi kukubali hili suala kuwa wapo kwa ajili ya wananch na si matumbo yao
 
Nami nataka kujua kama imeshaanza kufanya kazi. Kama haijaanza nijitoe sasa hivi nichukue changu
 
Aisee halafu faizafoxy aje hapa alete utumbo wake,simpendi huyu mama wakala wa shetani ccm.ccm hadi itumalize wote ndo itulie,mwaka huu wakiiba kura bora nchi igeuka kuwa mto wa damu kuliko kuwahadaa watu na amani ya kishenzi,huyu malaya Irene Isaka aliyemtuma kamdanganya,nina hasira sana na hawa mbwa ccm,nimefanya kazi migodini najua ugumu wa kazi na mateso wanayopata wafanyakazi wa migodi na %100 ukifanya kazi zaidi ya miaka 5 huwezi kuwa mzima,leo hii na pesa uliyovuna waipore.Hakika naichukia ccm kuliko kitu chochote duniani.
 
Huu sasa ni wizi. Sasa mwenye mil 4 na ana miaka 28 tu hiyo hela haitoshi hata hizo 3.6 mara miaka iliyobaki. Watabaki wanamdai au?

Natamani aje muhusika atoe majibu mazuri kwa swali zuri na la msingi kama hili!
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Back
Top Bottom