Sheria mpya ya ardhi.....nani anayeijua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria mpya ya ardhi.....nani anayeijua?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sijali, Sep 27, 2012.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Sina data, lakini kwa kusoma kwangu huku ughaibuni mambo si shwari Tanzania mintarafu ya umilikaji wa ardhi unaofanywa na wageni, hasa wazungu.
  Picha niipatayo katika kusoma-soma ni kwamba bwana mdogo, JK, ameachia makabaila wakuu wa Marekani na kutoka nchi jirani, kutwaa mapande makubwa ya ardhi kwa kisingizio cha kuanzisha kilimo cha kisasa.
  Kwa kujua hatari ya hawa jamaa na jinsi wanavyoabudu ardhi (maana kwao ni wachache sana wanaoweza kumiliki ardhi) nachelea mikataba hiyo inayotiwa kisirisiri itakuja kuwasaliti Watanzania hapo siku za usoni wakati watakapoamka na kuwa na uwezo wa kuitumia ardhi kisawasawa. Angalia Zimbabwe hii leo.
  Ndipo nikafikiria, kwani sheria ya sasa ya umilkaji wa ardhi Tanzania, hasa kwa wageni, inasemaje? Kuna yeyote anayejua hapa?
  Mara kwa mara unasikia Tanzania haitaki kuingia kishingoshingo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa vile inaogopa Wakenya, Warwanda kuja kutwaa ardhi, lakini hakuna yeyote apingaye wazungu!
  Magazeti ya huku mara kwa mara yanaandika juu ya wazungu wa zamani waliofukuzwa Zimbabwe na wale wanaohofia yatakayotokea Afriuka Kusini ambako suala la ardhi bado linajadiliwa, kuwa wote hawa wanakimbilia Tanzania na Msumbiji.
  Ikiwa haya ni kweli, basi Mwafrika, aidha husahau haraka au hana akili ya kufikiria wakati wa mbele.
  Yanayotokea sasa ndiyo yaliyotokea miaka 200 iliyopita wakati machifu na wafalme wetu waliporubuniwa na watu hawa na kuwapa maeneo makubwa- mara nyingi nchi nzima. Hivi hatusomi historia ya Zimbabwe, Zambia, Afrika Kusini, Kenya nk? Au hatuna uwezo wa kufikiria mbinu mpya wanazotumia?
  Mara nyingi unaposoma walivyofanyiwa mababu zetu unawadhareu kwa kutokuwa na ujanja wa kufichua mbinu za wazungu ambapo waliamriwa kutia saini mikataba bila ya wao kujua kilichoandikwa. Naona hii leo hali ni ile ile na kwa kweli hatujaerevuka katika kipindi cha miaka 200!
   
Loading...