Sheria mpya, Jeshi la zima moto na uokoaji kupewa silaha za kazi gani

Jana nimesikiliza taarifa ya habari nikasikia hii kitu. Mzee wangu akaniangalia kwa mshangao akaniuliza "zima moto silaha za nini?"

Bi mkubwa akanisaidia kumjibu kwa kumuambia kuwa moto ni kitu cha hatari hivyo wanahitaji silaha ili kupambana nao.

Mimi nikadakia nikawaambia labda neno silaha lina tafsiri pana. Watuambie silaha wanazomaanisha ni silaha gani. Kwasababu zimamoto sioni mantiki ya wao kumiliki bunduki, mabomu, vifaru na aina nyingine ya silaha kama hizo.

Basi tukaendelea kula na habari ikawa inaendelea.
Bado upo kwa washua!?
 
Kwamba moto Sasa unaenda kuzimwa kwa bunduki na mabomu ya machozi

Halafu Kuna mpumbavu mmoja ameshiba mashudu ya alizeti eti anatwambia twende Burundi, ili tugundue Nini......!
 
Kwa hiyo watakuja jeshi la zimamoto tu ili wapigane na magaidi na kuzima na Moto kwa wakati mmoja.kazi ya majeshi mengine Ni nini?. Akili zingine shida sana. ndiyo maana waliotuzidi akili mnawaita mabeberu
Aisee nimefurahi sana umegundua akili sina na ndivyo huwa nafurahi nikionekana humu kichwani hazimo
 
Naona nchi haina wataalamu wa mambo ya usalama na kama wapo basi ni vilaza.Sijaona haja ya zimamoto kuitwa jeshi na kupewa silaha wakati wao kazi yao ni laini tu kama kukuna nazi.

Halafu hata wabunge wetu ni tatizo wameshindwa kureason kabisa wao kazi kupitisha tu.Masisiemu bana.
 
Hakuna chochote bana.hizo ni mbinu tu za wajanja kujitengenezea namna ya kula.Jeshi la polisi likoboreshwa linaweza kufanya mambo yote hayo yakiusalama na zima moto likabaki na jukumu lake la msingi.Tofauti na hapo ni ubabaishaji mtupu.
Mkuu upo sahihi lakini tofauti na sheria
 
Yaan zimamoto wafike bila polisi kuwahi pia ndicho unachojaribu kusema.

Haiwezekeni ufanye mambo ya uokoaji na kulinda mali wakati kuna chomba cha kufanya huo wajibu.

Kwanza head count ya zimamoto tu shida.

Hapo hujatazama changamoto za vifaa vyao leo unawaongezea mabunduki nayo yanunuliwe.
Zimamoto ni askari, kutaka askari wakalindwe na Polisi hiyo ni sawa na kusema askari wa jeshi lingine wakawalinde askari wa jeshi lingine hiyo ni dharau.

Polisi ni wachache sana hawawezi kujigawa kila sehemu wawepo, hii nchi kubwa sana mkuu, kwanini Zimamoto wasijilinde wenyewe? Kwanini walindwe na Polisi ilihali wote wamepitia mafunzo?

Uliwahi kuhudhuria passing out ya askari wa Zimamoto?

Sent from my SM-N960N using JamiiForums mobile app
 
Habari wakuu
Bunge liko katika mchakato wa kupitisha muswada wa sheria mpya ambayo itaisimika jeshi la zima moto na uokoaji kuwa jeshi kamili
Sheria hiyo inaelekeza kuwa jeshi hilo litapewa silaha (bunduki) zake kama yalivyo majeshi mengine hapa nchini

maswali ya kujiuliza, Hivi katika shughuli za kuzima moto na uokoaji kunahitajika silaha kwa matumizi gani?

Serikali haioni inaenda kuongeza gharama kwa kununua silaha kwa jeshi la zimamoto?

Zimamoto inahitaji zaidi vifaa vya kuzimia moto, kama magari na fire extinguishing tools zote
Jeshi la zimamoto na uokoaji linahitaji zaidi vifaa vya kazi na kujengewa uwezo wa kutimiza malengo yake makuu kuliko kubeba silaha za moto

Ni jeshi muhimu na la maana sana katika kuokoa watu na Mali zao…
 
Vifaa ni pamoja na bunduki mkuu.
Zimamoto hawezi kwenda kuokoa mali za watu bila ulinzi, akae asubiri Polisi wakamlinde huo muda unatoka wapi?

Zimamoto aende kuokoa Supermarket ya mtu inaungua na wananchi wanajisombea mali we unadhani atawezaje kuwadhibiti mikono mitupu?

Lazima awe na chuma kulinda mali na kujilinda mwenyewe maana waafrika tunajuana vizuri

Sent from my SM-N960N using JamiiForums mobile app
 
Vifaa ni pamoja na bunduki mkuu.
Zimamoto hawezi kwenda kuokoa mali za watu bila ulinzi, akae asubiri Polisi wakamlinde huo muda unatoka wapi?

Zimamoto aende kuokoa Supermarket ya mtu inaungua na wananchi wanajisombea mali we unadhani atawezaje kuwadhibiti mikono mitupu?

Lazima awe na chuma kulinda mali na kujilinda mwenyewe maana waafrika tunajuana vizuri

Sent from my SM-N960N using JamiiForums mobile app
So ataanza kuzima moto au kutumia bunduki?

min most cases polisi nao hufika kwenye maafa hata kabla ya zimamoto

anyways
 
Wanasiasa akili zao wanazijua wenyewe

Nilitegemea Hilo jeshi likiongezewa vifaa vya uokoaji Kama vile gari za maji, boti za kisasa ,na vingenevyo

Usikute wao malengo yao ni kupambana na upinzani at all costs

Habari wakuu
Bunge liko katika mchakato wa kupitisha muswada wa sheria mpya ambayo itaisimika jeshi la zima moto na uokoaji kuwa jeshi kamili
Sheria hiyo inaelekeza kuwa jeshi hilo litapewa silaha (bunduki) zake kama yalivyo majeshi mengine hapa nchini

maswali ya kujiuliza, Hivi katika shughuli za kuzima moto na uokoaji kunahitajika silaha kwa matumizi gani?

Serikali haioni inaenda kuongeza gharama kwa kununua silaha kwa jeshi la zimamoto?

Zimamoto inahitaji zaidi vifaa vya kuzimia moto, kama magari na fire extinguishing tools zote
Kipaumbele kikubwa cha jeshi la zima moto kuwa imara ni upatikanaji wa vifaa bora na vya kisasa katika shughuli zake, waongeze helicopter za jeshi la zimamoto zitakazoweza kutoa huduma kama vile kuungua kwa msitu,meli,ghorofa nk.
Sioni ubaya wa kuwapa silaha kama kifaa. Ila sio first priority katika suala zima la planning and implementation na wasisahau hizi sheria baada ya miaka 5 ndiyo zinakuja kuleta utata tena
 
Back
Top Bottom