SHERIA MKONONI; Aliyedaiwa kuwa kibaka auawa na wananchi wenye hasira kali!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SHERIA MKONONI; Aliyedaiwa kuwa kibaka auawa na wananchi wenye hasira kali!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiganyi, May 7, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Leo asubuhi maeneo ya chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha Elimu DUCE mkabala na Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Mgulani katika barabara ya Chang'ombe Camera ya Fullshangwe imenasa tukio la kibaka huyu ambaye amekutwa akiwa ameuwawa huku tairi likiwa linawake pembeni. inasadikiwa alikutwa katika nyumba za jirani na eneo hilo akitaka kuiba hivyo wananchi wenye hasira kali wakamkamata na kumpiga na kuchoma tairi ili kumuunguza, hata hivyo haijulikani nani alimuokoa asiungue na tairi hilo japokuwa amepoteza maisha
  [​IMG]
  Wanafunzi wakiushangaa mwili wa kibaka huyo aliyepigwa na wananchi wenye hasira na kuuwawa wakati akitaka kuiba katika moja ya nyumba kwenye eneo hilo.
   
 2. Kamtori

  Kamtori Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hawa vibaka hata wakipelekwa sero wanaachiliwa because wanashirikiana na mapolice, its not a good idea but how do we reduce the number of these people in the streets, mapapa wengi dagaa wengi pia its veeeeeeery frsutrating.
   
 3. fige

  fige JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wasio na hatia husingiziwa wezi na kuuliwa kwa mtindo huu.Ni hatari sana haufai kuushabikia ,watu wengi hawataelewa ninachosema mpaka wapoteze wanaowahusu bila hatia.
   
 4. paty

  paty JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,253
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  not fair, watZ tuwe na huruma jamani
   
 5. Mfarisayomtata

  Mfarisayomtata JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 419
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  SAUT mwanza hadi sasa washaua watu wa hivi wa4 sasaivi ni vita kali kati ya raia na wanachuo, polisi wa doria wamemwagwa kama sijui nini kwenye mitaa ya chuo.
   
 6. King2

  King2 JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli. Wezi Mafisadi akina ngeleja tuna waacha. 2nawaonea vidagaa.
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,325
  Likes Received: 2,615
  Trophy Points: 280
  ukiona maiti kama hivi ndio moyo wa huruma unakuingia, lakini pindi unapoibiwa hasira utayokua nayo itakufanya japo urushe hata kajiwe kadogo ili mradi utulize munkari.
  jana maeneno ya magomeni kagera nimeshuhudi jamaa mmoja akitokwa simu na kibaka, kibaka nusura agongwe na gari katika harakati za kukimbia.
  sio siri vibaka wanatakiwa waadabishwe!
   
 8. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ingependeza mawazili na mafisadi wote wafanywe kama huyo kijana. Yani inatakiwa hiyo picha ya kijana aliyelala hapo chini iwe ya Ngeleja au Malima au Chami auEkelege... Ningefurahi sana... WaTZ tuanze kuwasaka hawa wakina ngeleja na kuwachoma moto pia...
   
 9. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  so sad
   
 10. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ww pia n fisadi ukipata mwanya
   
 11. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nilishaibiwa mara nyingi na nikapandwa na hasira to the maximum, ila idea ya kuua mtu haijawahi kuingia akilini mwangu!
  Tusiwe wepesi wa kuwahukumu hawa watu jamani, wengine ni victims wa maisha magumu yaliyosababishwa na mifumo mibaya ya kitabaka inayotokana na utawala mbovu wa kifisadi.
  Wengine wanatajirika kwa kuwauzia hawa watu madawa ya kulevya! Malipo hapa hapa duniani, siku moja anaestahili kuuawa atajulikana tu!
  Wamenyimwa elimu, maarifa na wanaona wengine wanakula maisha.
  SIUNGI MKONO TABIA WANAYOFANYA ILA NAWAHURUMIA.
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kile usichotaka kufanyiwa

  nawe usimfanyie mwenzako!

  Nao vibaka hawasikii wala hawaoni!
   
 13. lusubilo lucas

  lusubilo lucas Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Watanzania ni watu wa ajabu sana tunashindwa kuangalia chanzo cha tatizo na kujifanya eti tuna hasira na vibaka ambao nao ni waathirika wa uongozi mbaya ambao ni zao la uongozi mbovu
   
 14. s

  sheizashafi Member

  #14
  Dec 20, 2013
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamalizwe wote coz Watu kama Hao ni warudisha maendeleo nyuma...
   
 15. kmbwembwe

  kmbwembwe JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2013
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,425
  Likes Received: 1,394
  Trophy Points: 280
  Polisi wanakimbizana na hela wananchi sasa wanakamata na kuhukumu. Utawala wa sheria umeyeyuka kwa sheria kukosa haki.
   
 16. m

  mgadagu Member

  #16
  Dec 20, 2013
  Joined: Dec 20, 2013
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kagongwa na gari
   
 17. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2013
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,489
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  CC # mabina
   
 18. m

  mgadagu Member

  #18
  Dec 20, 2013
  Joined: Dec 20, 2013
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hujawahi ibiwa we we unasema tu
   
 19. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2013
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,325
  Likes Received: 2,615
  Trophy Points: 280
  sijawahi kuibiwa nini? na ninasema nini?
   
 20. sikajiji

  sikajiji JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2013
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 581
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Subiri siku utakapoporwa kusha wanakupigia keleze za mwizi huku wakikupiga ndipo utakapojua suala la kuchukua sheria mkononi ni zuri au baya utakapokuwa kuzimu.
  [​IMG]
   
Loading...