Sheria mbili kandamiza za uchaguzi Tanzania.

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kwenye uchaguzi ngazi ya Udiwani hapa kwetu Tanzania kuna sheria mbili ambazo kwa maoni yangu ni kandamizi.

Katika sifa mbili ambazo zinamzuia mtu kuwa mgombea wa Udiwani kisheria, nukuu au rejea ya sheria zilizotajwa ni kandamizi. Sheria ya uchaguzi ya Udiwani inasema kuwa mtu atazuiliwa kuwa mgombea wa udiwani iwapo

  1. Yumo kizuizini kwa mujibu wa sheria ya kuweka watu kizuizini ya mwaka 1962
  2. Yuko uhamishoni, kwa zaidi ya miezi sita kwa mujibu wa sheria ya uhamishoni (Deportation Ordinance)

Tafsiri yangu kwenye sheria hizi ni kwamba mpaka sasa Rais anayo mamlaka "kisheria" ya kuwaweka watu kizuizini bila hata kupata kibali cha mahakama. Kwa hiyo tunapozungumzia mabadiliko ya katiba tutilie mkazo na mabadiliko ya sheria kandamizi zilizopo. Wanasheria wanaweza kutusaidia sifa zitakiwazo mtu kuwekwa kizuizini kwa amri ya Rais.

Kwenye sheria ya "Deportation Ordinance" hapa anayehusika ni Mkuu wa Wilaya. Kwa sheria hii Mkuu wa wilaya anayo mamlaka ya kumhamisha mtu kwa mfano kutoka Misenyi kwenda Tandahimba na akatoa na muda anaotaka mtu huyo aliyehamishwa akae huko. Kwa maana nyingine Mkuu wa wilaya anayo mamlaka ya kukupiga marufuku "kisheria" kuonekana kwenye Wilaya "yake" hata kwa maisha yako yote.

Ingawa sheria hizi ni kandamizi zimeingiaje kwenye sheria za uchaguzi wa Udiwani?
 
Back
Top Bottom