Sheria: Mambo 10 ya kuzingatia unapojitetea mahakamani

Oct 26, 2021
98
287
1: Kama unahojiwa na Wakili Mahakamani usijibu bila kutafakari alichokuuliza

2: Wakili asikuogopeshe kwa ukali, anapokuuliza kwani ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha ulichopanga kusema

3: Usilazimishe kujibu kitu ambacho hukijui ni bora kusema sijui kuliko kulazimisha kujibu

4: Usipaniki kiasi cha kutoa neno lolote la kashfa, kejeli, au tusi mahakamani unaweza kuongeza kosa la kuidharau Mahakama

5: Kama hukuelewa vizuri kosa ulilosomewa ni bora kukaa kimya, kwakuwa ukikaa kimya unaandikiwa umekataa kosa

6: Kanuni ya sheria ni kuwa, ni kazi ya aliyekushitaki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa umetenda kosa na si kazi yako kuthibitisha kuwa haujatenda kosa

7: Kama ulitenda kosa katika harakati za kujitetea usidhuriwe iambie mahakama kuwa ulitenda kosa ukijilinda (self defence) inaruhusiwa, hata kama uliua waweza kuachiwa

8: Kama ndugu yako hana akili timamu na ametenda kosa iambie mahakama. Hii ni kwasababu kutokuwa na utimamu wa akili ni kinga inabidi aachiwe lakini hatarudi nyumbani atapelekwa vituo vya wasio na akili

9: Inakubalika na ukaachiwa huru kusema kuwa sikuwa eneo la tukio wakati likitokea kama kweli haukuwapo

10: Kama wanaokushtaki wanashahidi na unamjua kuwa kuna kipindi aliwahi kuchangnyikiwa au kufanya tukio lolote la uhalifu kabla, ni nafasi nzuri kuhoji uwezo na uadilifu wake.
 
UP6ii.jpg
 
Hiyo ya anayekushtaki ni jukumu lake kuthibitisha kwa kuleta ushahidi wa wewe ulitenda kosa, na sio mshitakiwa aumize kichwa kuielewesha mahakama sikutenda kosa
 
Ushauri nasaha;

1) JIBU UNACHO ULIZWA KUTOKANA NA UFAHAMU WAKO.

2) Usijifanye mjuaji.

3) Usijibu kutetea au kuvutia kwa waliokuleta mahakamani (Kama umeletwa na jamhuri basi usiumize kichwa kujibu kwa kuficha maovu yao, utaaibika).

Mwisho wa siku, wewe ni shahidi na kama kuna utumbo au makosa waliofanya hao waliokuleta mahakamani basi wewe hayakuhusu!!!!
 
Back
Top Bottom