Sheria kuzuia siasa nje ya jimbo: Ukabila, Ukanda, Uvunjifu wa Katiba kupikwa na maprofesa wa sheria

papaa musofe

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
842
1,475
Naona kuna sheria inatungwa,bahati mbaya au nzuri,au mbaya zaidi,inatungwa kipindi ambacho wizara ya sheria inaongozwa na maprofesa wawili,mmoja waziri,mwingine katibu mkuu,wote matunda ya UDSM

Sheria hii ina lengo la kuzuia siasa nje ya jimbo ambalo muhusika ni mbunge,kwa maana hiyo,muhusika atafanya siasa ndani ya eneo lake

Kama sheria hii itapita,zile ndoto za Mzee Nyerere kufuta ukabila na ubaguzi wa kimaeneo hazitatimia,sasa sheria ndio itakuwa inatuelekeza jinsi ya kubaguana na maafisa wa serikali,hasa polisi ndio watakuwa wanahakikisha mtanzania wa eneo Fulani akomee hukohuko na hana ruksa ya kuongea na kujadili maendeleo ya Tanzania na wenzie wa maeneo mengine

Mgogo wa Dodoma aliyepata ubunge hataruhusu mkurya wa Tarime aungane naye kuhubiri uzalendo na umoja wa kitaifa dodoma,dodoma wagogo tu ndio watakuwa wanahutubia wagogo wenzao,na ili kukoleza,wanaweza hata kuhutubiana kwa kabila la kigogo kwa kuwa watu wa iringa wahehe na wakinga,kisheria wamezuiwa kushirikiana na watanzania wenzao wa dodoma katika mambo ya kisiasa

Pia wakerewe nao watahutubiana ukerewe huko huko na wakerewe wenzao,wakerewe wakimuona mchaga kaja kuwasimulia uzuri wa Tanzania,basi polisi watamzuia na watamwambia hili sio jimbo lako ondoka,huku wanaongea wakerewe kwq wakerewe

Tulianza na shule za kata,wanafunzi hawavuki kata,sasa wabunge(na pengine hata madiwani)watabaki kuwa wa maeneo yao,

Mzee Nyerere alikuwa na mfumo wa kumtoa mwanafunzi chato na kumpeleka iringa akasome,lengo ni kumfanya achangamane na asahau siasa za parokia,ajihisi mtanzania na sio mtu wa Njombe,mwanza,sumbawanga,hao,marangu

Lakini tunakoelekea sasa kabla ya kufanya mkutano wa hadhara,ukitoa taarifa polisi,unaulizwa,

"Wewe ni wa wapi "

Huulizwi kama wewe ni mtanzania,ukijibu wewe ni mfipa wa Katavi unafukuzwa,unaambiwa hapa inarihusiwa mikutano ya wamasai,mbunge wa hapa ni mmasai,ondoka,hapa tayari tunabaguana kwa mujibu wa sheria,watawala wanajenga mifumo ya kuhakikisha tunabaguana kijimbo,kikata(kwa madiwani),kimkoa,kiwilaya,wa huku havuki kwenda kule

Wakiwa bungeni wabunge wanachangia bajeti ya taifa ambayo hawazuiwi kuchangia kuhusu sehemu yeyote ya Tanzania,wanachangia kuboresha bajeti ya Tanzania bungeni na wana haki ya kuhoji utekelezaji wa bajeti hiyo sehemu yeyote ya Tanzania,hii inamfanya ajione yeye ni mbunge wa BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,si mbunge wa jimbo tena,anawajibika kwa nchi nzima,

Pia mbunge ana haki mbili,ya kiubunge kwa maana kwa nchi na wapiga kura na pia ana haki ya kiraia,chama cha siasa kimempa uwanachama,sheria inazuia chama kisifanye kazi sehemu moja tu ya jamhuri,pia chama lazima kipate wanachama kwa mikoa zaidi ya kumi,

Mbunge anapotembea anatembea na haki hizi mbili,ya kueneza chama,na pia anatembea na hadhi ya ubunge,chama kilichompa ubunge kimesajiriwa nchi nzima,ana jukumu la kukieneza nchi nzima kwa kofia ya uanachama na pia ya ubunge

Nawasihi maprofesa wasiingie katika mtego wa kuharibu CV zao kwa kujenga ubaguzi

Tinataka wachaga wahutubiwe na wakinga,wakinga wahutubiwe na wakurya,wamasai wahutubie wasukuma
 
Ikipita hiyo sheria, Mbunge wa Kishimundu atakuwa haoni sababu wala umuhimu wa kuzungumzia yanayojiri na kutokea nyakanazi maana atahisi kwamba hayamhusu!

Yaani tunaleta Siasa za Ujimbo bila kujijua!

Ile Spirit ya Taifa moja, kwamba, Madhila ya Sehemu moja yanamuuma na mwingine wa sehemu nyingine itapotea!.

Iwapo ukanda mmoja utakwenda kwa chama kimoja na Ukanda mwingine ukaenda kwa chama kingine, halafu yasiwepo mazingira ya kisiasa ya vyama tofauti kwenda kutafuta uungwaji mkono katika eneo jingine la nchi, basi fahamu wazi, Utaigawa nchi baina ya makundi mawili na itakuwa vigumu kuwa na Taifa moja lenye umoja!.

Chukulia mfano Leo Chadema iwe na nguvu Ukanda wa Kaskazini, halafu CCM iwe na nguvu ukanda mwingine, Bila kuruhusu siasa, Ukanda wa Kaskazini utajiona Chadema always na Ukanda mwingine utajiona CCM always, na ni rahisi kupenyeza siasa za ukabila katika set up ya aina hii!!.

Nashauri hii sheria kama kweli wanafikiria kuitunga waache!. Italeta siasa za Ukanda na Ukabila nchini!
 
Naona kuna sheria inatungwa,bahati mbaya au nzuri,au mbaya zaidi,inatungwa kipindi ambacho wizara ya sheria inaongozwa na maprofesa wawili,mmoja waziri,mwingine katibu mkuu,wote matunda ya UDSM

Sheria hii ina lengo la kuzuia siasa nje ya jimbo ambalo muhusika ni mbunge,kwa maana hiyo,muhusika atafanya siasa ndani ya eneo lake

Kama sheria hii itapita,zile ndoto za Mzee Nyerere kufuta ukabila na ubaguzi wa kimaeneo hazitatimia,sasa sheria ndio itakuwa inatuelekeza jinsi ya kubaguana na maafisa wa serikali,hasa polisi ndio watakuwa wanahakikisha mtanzania wa eneo Fulani akomee hukohuko na hana ruksa ya kuongea na kujadili maendeleo ya Tanzania na wenzie wa maeneo mengine

Mgogo wa Dodoma aliyepata ubunge hataruhusu mkurya wa Tarime aungane naye kuhubiri uzalendo na umoja wa kitaifa dodoma,dodoma wagogo tu ndio watakuwa wanahutubia wagogo wenzao,na ili kukoleza,wanaweza hata kuhutubiana kwa kabila la kigogo kwa kuwa watu wa iringa wahehe na wajinga,kisheria wamezuiwa kushirikiana na watanzania wenzao wa dodoma katika mambo ya kisiasa

Pia wakerewe nao watahutubiana ukerewe huko huko na wakerewe wenzao,wakerewe wakimuona mchaga kaja kuwasimulia uzuri wa Tanzania,basi polisi watamzuia na watamwambia hili sio jimbo lako ondoka,huku wanaongea wakerewe kwq wakerewe

Tulianza na shule za kata,wanafunzi hawavuki kata,sasa wabunge(na pengine hata madiwani)watabaki kuwa wa maeneo yao,

Mzee Nyerere alikuwa na mfumo wa kumtoa mwanafunzi chato na kumpeleka iringa akasome,lengo ni kumfanya achangamane na asahau siasa za parokia,ajihisi mtanzania na sio mtu wa Njombe,mwanza,sumbawanga,hao,marangu

Lakini tunakoelekea sasa kabla ya kufanya mkutano wa hadhara,ukitoa taarifa polisi,unaulizwa,

"Wewe ni wa wapi "

Huulizwi kama wewe ni mtanzania,ukijibu wewe ni mfipa wa Katavi unafukuzwa,unaambiwa hapa inarihusiwa mikutano ya wamasai,mbunge wa hapa ni mmasai,ondoka,hapa tayari tunabaguana kwa mujibu wa sheria,watawala wanajenga mifumo ya kuhakikisha tunabaguana kijimbo,kikata(kwa madiwani),kimkoa,kiwilaya,wa huku havuki kwenda kule

Wakiwa bungeni wabunge wanachangia bajeti ya taifa ambayo hawazuiwi kuchangia kuhusu sehemu yeyote ya Tanzania,wanachangia kuboresha bajeti ya Tanzania bungeni na wana haki ya kuhoji utekelezaji wa bajeti hiyo sehemu yeyote ya Tanzania,hii inamfanya ajione yeye ni mbunge wa BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,si mbunge wa jimbo tena,anawajibika kwa nchi nzima,

Pia mbunge ana haki mbili,ya kiubunge kwa maana kwa nchi na wapiga kura na pia ana haki ya kiraia,chama cha siasa kimempa uwanachama,sheria inazuia chama kisifanye kazi sehemu moja tu ya jamhuri,pia chama lazima kipate wanachama kwa mikoa zaidi ya kumi,

Mbunge anapotembea anatembea na haki hizi mbili,ya kueneza chama,na pia anatembea na hadhi ya ubunge,chama kilichompa ubunge kimesajiriwa nchi nzima,ana jukumu la kukieneza nchi nzima kwa kofia ya uanachama na pia ya ubunge

Nawasihi maprofesa wasiingie katika mtego wa kuharibu CV zao kwa kujenga ubaguzi

Tinataka wachaga wahutubiwe na wakinga,wakinga wahutubiwe na wakurya,wamasai wahutubie wasukuma
Naomba nilitizame kwa upande mwingine.
Sehemu ambazo Chama kimoja kimechukua viti vingi itakuwa chama kingine kujijenga hapo kwani hawatauhusiwa .
Pia tukumbuke ya kuwa kuna watu wana kipaji cha ushawishi na watu hawa hawatakuwa na nafasi ya kushawishi watu wa maeneo tofauti na kwao.
Kwa jumla amri hii inatengeneza kombora.
 
Sasa hivi hakuna cha professor wala nini, wote wanatunga sheria wanazoagizwa na mtu. Hao maprofessor wanapambania matumbo yao hawajali hilo litakalotokea baadae, cha muhimu kwao wao ni kuhakikisha wanaishi maisha mazuri. Hii sheria iko wazi kabisa muasisi wake ni nani.
 
Tatizo wabunge wetu hawakai majimboni mwao.
Kuna sehemu wana utaratibu wa wapiga kura wa eneo husika kumtaka mbunge ajieleze kwa nini mahakama isimnyanganye ubunge ,ikipatikana idadi ya wapiga kura halali waliompigia kura wanaompinga na kumshutumu,wanapeleka hoja mahakamani

Hii pia haiwezi kuwa hoja ya kuhalalisha ubaguzi
 
Naona kuna sheria inatungwa,bahati mbaya au nzuri,au mbaya zaidi,inatungwa kipindi ambacho wizara ya sheria inaongozwa na maprofesa wawili,mmoja waziri,mwingine katibu mkuu,wote matunda ya UDSM

Sheria hii ina lengo la kuzuia siasa nje ya jimbo ambalo muhusika ni mbunge,kwa maana hiyo,muhusika atafanya siasa ndani ya eneo lake

Kama sheria hii itapita,zile ndoto za Mzee Nyerere kufuta ukabila na ubaguzi wa kimaeneo hazitatimia,sasa sheria ndio itakuwa inatuelekeza jinsi ya kubaguana na maafisa wa serikali,hasa polisi ndio watakuwa wanahakikisha mtanzania wa eneo Fulani akomee hukohuko na hana ruksa ya kuongea na kujadili maendeleo ya Tanzania na wenzie wa maeneo mengine

Mgogo wa Dodoma aliyepata ubunge hataruhusu mkurya wa Tarime aungane naye kuhubiri uzalendo na umoja wa kitaifa dodoma,dodoma wagogo tu ndio watakuwa wanahutubia wagogo wenzao,na ili kukoleza,wanaweza hata kuhutubiana kwa kabila la kigogo kwa kuwa watu wa iringa wahehe na wajinga,kisheria wamezuiwa kushirikiana na watanzania wenzao wa dodoma katika mambo ya kisiasa

Pia wakerewe nao watahutubiana ukerewe huko huko na wakerewe wenzao,wakerewe wakimuona mchaga kaja kuwasimulia uzuri wa Tanzania,basi polisi watamzuia na watamwambia hili sio jimbo lako ondoka,huku wanaongea wakerewe kwq wakerewe

Tulianza na shule za kata,wanafunzi hawavuki kata,sasa wabunge(na pengine hata madiwani)watabaki kuwa wa maeneo yao,

Mzee Nyerere alikuwa na mfumo wa kumtoa mwanafunzi chato na kumpeleka iringa akasome,lengo ni kumfanya achangamane na asahau siasa za parokia,ajihisi mtanzania na sio mtu wa Njombe,mwanza,sumbawanga,hao,marangu

Lakini tunakoelekea sasa kabla ya kufanya mkutano wa hadhara,ukitoa taarifa polisi,unaulizwa,

"Wewe ni wa wapi "

Huulizwi kama wewe ni mtanzania,ukijibu wewe ni mfipa wa Katavi unafukuzwa,unaambiwa hapa inarihusiwa mikutano ya wamasai,mbunge wa hapa ni mmasai,ondoka,hapa tayari tunabaguana kwa mujibu wa sheria,watawala wanajenga mifumo ya kuhakikisha tunabaguana kijimbo,kikata(kwa madiwani),kimkoa,kiwilaya,wa huku havuki kwenda kule

Wakiwa bungeni wabunge wanachangia bajeti ya taifa ambayo hawazuiwi kuchangia kuhusu sehemu yeyote ya Tanzania,wanachangia kuboresha bajeti ya Tanzania bungeni na wana haki ya kuhoji utekelezaji wa bajeti hiyo sehemu yeyote ya Tanzania,hii inamfanya ajione yeye ni mbunge wa BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,si mbunge wa jimbo tena,anawajibika kwa nchi nzima,

Pia mbunge ana haki mbili,ya kiubunge kwa maana kwa nchi na wapiga kura na pia ana haki ya kiraia,chama cha siasa kimempa uwanachama,sheria inazuia chama kisifanye kazi sehemu moja tu ya jamhuri,pia chama lazima kipate wanachama kwa mikoa zaidi ya kumi,

Mbunge anapotembea anatembea na haki hizi mbili,ya kueneza chama,na pia anatembea na hadhi ya ubunge,chama kilichompa ubunge kimesajiriwa nchi nzima,ana jukumu la kukieneza nchi nzima kwa kofia ya uanachama na pia ya ubunge

Nawasihi maprofesa wasiingie katika mtego wa kuharibu CV zao kwa kujenga ubaguzi

Tinataka wachaga wahutubiwe na wakinga,wakinga wahutubiwe na wakurya,wamasai wahutubie wasukuma
Maprofesa nijuavyo Mimi ni weledi vinginevyo neno process lisiwe mkulima asiyekuwa na uhakika analima ili iweje.
 
Back
Top Bottom