Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili (10 Laws of the Mind and Universe/Universal Laws)

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,217
Ni kutoka katika Jitambue Sasa.

Unaweza ukaziita Ni KANUNI AU SHERIA AU LAWS.

Akili ya mwanadamu ni sehemu ambayo watafiti wengi wamekuwa wakihamasika kuielewa. Akili ni sehemu pana sana kwa mwanadamu. Ni sehemu ambayo haionekani wala haishikiki lakini ina matokeo makubwa sana kwa mwanadamu. Akili imezaa vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu, mawazo, imani, misimamo n.k. Kama unapenda sana kujifunza na kufahamu mengi lazima utakuwa unatamani kufahamu siri kuu za akili. Kuelewa siri kuu za akili ni kufahamu Sheria ambazo zinaiongoza akili. Katika mada hii utapata kuona mwanga kuhusiana na akili na kuweza kujifahamu vyema.

SHERIA/KANUNI HIZO NI:

  1. Sheria ya Chanzo na Matokeo
  2. Sheria ya Uhuru wa Kufikiria
  3. Sheria ya Umakini/focus
  4. Sheria ya Mawazo
  5. Sheria ya Ubinafsi
  6. Sheria ya Uumbaji
  7. Sheria ya Hisia
  8. Sheria ya Ubadili
  9. Sheria ya Usawa wa Akili
  10. Sheria ya Kutokea.Nini maana ya Sheria za Akili?

Mapinduzi makuu ya sasa ni ufuatiliaji wa asili na jinsi akili ya mwanadamu ilivyo. Sayansi ya kufuatilia akili ya mwanadamu ilivyo ni sayansi ambayo inategemewa kuleta mapinduzi makubwa kwani akili ya mwanadamu ina sayansi kubwa sana. Asilimia kubwa ya maisha ya mwanadamu inatengenezwa na akili yake hivyo katika elimu hiyo utaweza kufahamu mengi sana kuhusiana na mwanadamu na jinsi akili yake inavyofanya kazi vyema.

Mlolongo huu wa mada utakuwa na mada kumi, ambapo kila mada itaelezea sheria yake kwa undani kwani kuweka mada moja kuelekeza mad azote hizi kutapelekea uchache wa maelekezo.

Sheria
Kwa lugha nyingine huita "Laws". Sheria ni kama maelekezo ya suala au jambo Fulani. Wengi wanafahamu sheria ya mvutano, ni sheria inayosema kuwa ukirusha kitu juu basi huvutwa kwenda chini kuelekea ardhini. Ni sheria ambayo uwe unaijua au usiijue ukijirusha gorofani lazima uanguke chini. Sheria kuwepo haimaanishi mpaka uijue ndipo matokeo yake huonekana bali hata ukiwa haujui bado sheria itafanya kazi yake katika mangilio wake unavyotaka.

Zipo sheria mbalimbali ulimwenguni ambazo zimekuwa zikilinda taratibu nyingi. Je umewahi kujiuliza kama kuna sheria au taratibu Fulani ambazo ukizielewa utaweza kufahamu jinsi akili inavyofanya kazi? Ni sawa na mkulima, akipanda maembe atavuna maembe, hata kama anajua kuwa anavuna anachopanda au hajui kuhusiana na uhusiano uliopo kati ya anachovuna na anachopanda bado atapata matokeo sawa. Hivyo ni vyema kufahamu sheria hizo. Ni vyema kufahamu kwani itakusaidia kuweza kuongoza matokeo. Ukiwa unajua kuwa taratibu Fulani hupelekea matokeo Fulani inakusaidia kutengeneza wakati ujao katika njia njema na kupata matokeo mazuri.

Mfano wa sheria nyingine ni sheria za rangi, kila mmoja anafahamu ukichanganya nyekundu na njano unapata machungwa, ni sheria kwani lazima itokee hivyo. Uwe unajua hilo wakati unachanganya au haujui lakini lazima matokeo yake yatokee. Ukichanganya blu na yellow utapata kijani, hiyo ni lazima. Labda uwe haujachanganya vyema au tatizo linguine lakini zikishachanganyika matokeo yake ni mengine.

Lengo la kutoa mifano hiyo ni kukupa mwangaza wa kuwa kuna sheria hapa ulimwenguni. Sheria ni taratibu ambazo zipo. Taratibu hizo hupelekea matokeo Fulani katika taratibu Fulani. Ni vyema kufahamu taratibu za msingi kuelewa mengi kwani ulimwengu upo kwa taratibu maalum. Kama tungekuwa hatujui kuwa ukiruka gorofani utaanguka chini na kufa kwani ukiruka unaanguka chini ni wangapi wangekuwa wamekufa kwa kutojua hayo? Lakini anayeuuzia hayo au kufanya maamuzi bila kujali au kwa kujali lazima taratibu zichukue nafasi yake na kupelekea matokeo yake.

Sheria zilikwepo tangu mwanzo wa ulimwengu na zitazidi kuwepo. Huenda kuna sheria nyingi ambazo bado hatujazijua kutokana na uelewa wetu lakini haimaanishi hazipo, bado zipo tu. Galileo Galilei alipofahamu kuwa kuna Gravity na kuelezea sheria ya kuvutwa vitu chini haimaanishi kabla yay eye kuelezea ilikuwa haipo. Bali alichofanya yeye ni kuifahamu sheria na sio kuianzisha sheria. Unaweza ukatumia sheria kwa mafanikio. Mfano kutokana na uelewa kuwa kuna kani ya mvutano wa tumetengeneza meli (kwa kuhakikisha haizami), tumetengeneza ndoo na vyomba vya kuhifadhi maji kwa kuziba chini, n.k vyote hivi ni kutusaidia kuweza kuishi katika cheria tulizozikuta.



SHERIA KUU ZA AKILI YA MWANADAMU.

Kama dunia ilivyo na sheria zake, serikali zilivyo na sheria zake, dini zilivyo na sheria zake, tamaduni Fulani za watu zilivyo na sheria zako fahamu kuwa hata akili nayo ina sheria zake. Kuna sheria za biolojia, jeographia, fizikia, n ahata saikolojia. Fahamu kuwa na hata akili ina sheria zake. Sheria hizo hutawala maisha ya mwanadamu kwani kila mwanadamu ana akili yake lakini akili zote zina asili moja na sheria moja, tofauti ni utumiaji.

Fahamu kuwa unaweza kuiongoza akili yako na kuitawala akili yako. Akili ni chombo kizuri sana kwa kubadilika lakini pia ni chombo kibaya sana kwa kupotoka.

Mada za Kuhusiana na Sheria hizo zinafuta, na kila sheria itaelezewa katika mada yake na mifano hai ambayo itakufunua mwangaza na kuelewa vyema jinsi akili ya mwanadamu ilivyo ya ajabu.


Sheria Ya 1: Chanzo na Matokeo.




Mawazo yetu ndiyo yanayounda uhalisia wetu na sio vingine. Hii ni sheria ya kale sana tangu enzi za wanadamu wa kale waliopenda kuwa watafutaji wa ukweli wa ulimwengu walikutana nayo. Ni sheria ambayo inafahamika sana na imetafsiriwa katika maelezo tofauti tofauti katika imani tofauti tofauti.
Ni sheria Kuu.

Kama ilivyo leo, hakuna anayefahamu ni kwanini kuna sheria kama vile ya Gravity, sheria za sayansi, n.k. Na hata katika sheria hii hakuna anauejua kwanini sheria hii ipo lakini hiyo haijalishi, kinachopaswa kwetu sisi wanadamu ni kuielewa vyema na kujua jinsi inavyofanya kazi ili nasi tuweze kuishi nayo.

Wazo ndio chanzo, vingine vyote ni matokeo tu.
Watu wengi hasa ambao hawajasoma sana wanafikiri kuwa vitu vya kifizikia ni halisi, wanafikiri ni kweli vitu hivyo vipo kifizikia. Kutokana na uelewa wao huo wanakuwa wanaamini sana ulimwengu wa nje yao na kusahau ulimwengu wa ndani yao. Huwezi kuelewa ulimwengu wa nje bila kuelewa ulimwengu wa ndani, ulimwengu wa nje ni matokeo ya ulimwengu wa ndani. Kutokana na kutoelewa huko watu wamekuwa wakiteseka na kuamini hawawezi kubadili maisha yao kwani hawajui chanzo cha maisha yao. Hawafahamu kuwa maisha yako ni matokeo ya uelewa wako wa ndani yako.

Mfano mzuri katika kuelewesha hilo ni sawa na tunaangalia sinema, kumbe sinema hiyo inatokana na matukio yaliyopo ndani ya ufahamu wetu. Sio sinema iliyopo nje yetu bali chanzo chake cha matukio kinatokana na ufahamu wetu. Sinema yake ni kama display tu ya ufahamu wetu. Kutoelewa hayo wanadamu wengi wamekuwa watumwa na wanateseka kutokana na kutofahamu chanzo cha hayo yote ni nini.

Kumbuka kuwa tunapoangalia sheria za kifizikia tunafahamu dhahiri kuwa HAKUNA JAMBO LISILO NA CHANZO. Na sheria hii ndipo iliposimamia. Hakuna jambo lisilo na chanzo na ndio maana inaitwa sheria ya chanzo na matokeo kwani kila tokeo lina chanzo chake. Hakuna matokeo yasiyo na chanzo kamwe.

Hivyo kama kila jambo lina chanzo chake, tunapaswa kufahamu kuwa uhalisia/reality ni illusion/Uongo kwani reality inatengenezwa na sisi wanadamu wenyewe na sio kwingine. Reality au uhalisia unaoishi unatokana na milango yako ya ufahamu, akili yako, imani yako na uelewa wako.

Kila kitu kina chanzo, huo ni uhalisia. Kila kitu kilianza kama ufahamu, mfano mzuri ni Computer, madirisha, nyumba, simu, nguo, sanaa, na vyote ambavyo vimetokana na ujuzi wa mwanadamu vilianza kama WAZO, baada ya kufanyiwa kazi vikatokea katika dunia ya kifizikia. Lakini hapo kabla vilikuwa ni Mawazo na sio physical things.

Chunguza sana sheria hii, kila tokeo unaloliona lina chanzo chake, kufahamu sheria hii inakusaidia kuwa mtafutaji wa ukweli. Badala ya kupoteza nguvu katika matokeo unapaswa kufuatilia chanzo cha tokeo kwani kubadili chanzo ni kubadili matokeo.

Walimu wakubwa wa ulimwengu huu wote wamefundisha sheria hii, wanaweza wakawa hawajakuambia moja kwa moja kutokana na kuwa uelewa wa wanadamu unatofautiana kwa jinsi wanavyoutumia lakini walimu hao wamekuwa wakitufundisha vyema kwa mifano. Mfano mzuri ni kuwa


  • Unavuna unachopanda: Ukipanda maembe utalima maembe, ukipanda magugu utavuna magugu. Sheria hii ni sawa na kukuambia kuwa kila tokeo lina chanzo, kubadili chanzo ni kubadili matokeo. Huwezi kuvuna maembe katika tawi la mchungwa.
  • Sheria ya Karma: Ni sheria ya mashariki inayosema kuwa kila WAZO, TENDO na MANENO yana matokeo yake katika ulimwengu wako. Kutokana na hilo wakafundisha kuwa kuna Karma ya matendo, Kuna karma ya maneno na kuna karma ya mawazo. Hivyo kila tutendacho, tusemacho na tunachofikiria kina matokeo katika dunia yetu. Nimesema dunia yetu kwani kila mwanadamu anaishi katika dunia yake. Sheria hii nayo nitakuja kuieleza vyema.
  • What goes around comes around: Nayo ni sawa na kusema kuwa kunachokijia ni matokeo ya kilichotoka kwako. What comes around is the result of whats goes out of you. Unachokipata ni matokeo ya ulichokitoa.
Tutakapokuja kufahamu kuwa tunaishi katika ulimwengu unaoumbwa kutokana na ufahamu wetu, kwa kufahamu hayo ni hatua moja ya kwanza katika kuweza kubadili maisha yako na kuweza kuelewa kwanini wanadamu wengine nao wanaishi katika uhalisia tofauti na wewe. Kwa kuanza kuelewa hili utaweza kujiuliza mengi na kujikuta unafahamu chanzo cha mengi badala ya kupoteza muda katika matokeo. Wengi hupoteza muda kubadili matokeo kumbe matokeo ni matokeo, huwezi kuyabadili bali unaweza kubadili chanzo chake.


Maya Angelou aliwahi kusema sentensi moja nzuri sana -
Kama haupendi unachokiona kibadili, kama hauwezi kukibadili badili mtazamo wako.


Kwa kuweka sheria hii katika uelewa mzuri na kwa kufupisha vyema ni kusema kuwa:

Mawazo yetu yanaumba ulimwengu wetu, mawazo yetu ndio kiaishiria ya kinachofuatia. Kila jambo lina chanzo, chanzo kikuu na chanzo ambacho ndio cha mwanzo kabisa ni WAZO. Tunaishi katika dunia ambayo inatengenezwa na uelewa wetu. Ndio maana kila mwanadamu anaishi katika dunia yake kutokana na kuwa uelewa unatofautiana baina ya wanadamu.
BADILI MAWAZO YAKO KUBADILI DUNIA YAKO.


SHERIA YA PILI INAENDELEA HAPA
 
Nimekuwa nikiweka Posts katika jukwaa la Jamii Intelligence lakini nyingine zimekuwa zikichukua muda sana kupitiwa na takribani ilikuwa inachukua siku moja nzima mpaka mbili na zaidi mods walikuwa hawajazipitia. Kutokana na tatizo hilo nimependa kuweka katika thread hii kwani zitakuwa posted moja kwa moja.

Napenda kuwakaribisha kwa maswali na kushirikiana kueleweshana vyema. Pia nitashukuru kama mods Invisible na wingine watapitia na kunisaidia kuweka katika jukwaa la Jamii Intelligence ili wengi wapate kujifunza na kushirikiana kueleweshana.

Asanteni sana. Mbarikiwe.
 
Last edited by a moderator:
Apollo mimi nadhani hizi sio sheria bali ni kanuni. Sheria hupinduliwa, lakini kanuni hazipinduliwi!

Mfano kanuni ya kutafuta eneo la mraba, mstatili itaendelea kuwa vile vile miaka na miaka. Kinachoweza kubadilika na kupatikana njia mbdala tu lakini will reach at the same destination!

Napenda kanuni, SIPENDI SHERIA/LAW!
 
Last edited by a moderator:
We jamaa utawachanganya maelfu kwa maelfu..............sometimes little knowledge is healthier than super knowledge!

Ahsante kwa haya madini adimu!

Ubarikiwe na Mungu wangu!

Hapana ndugu yangu, Naamini kuwa watu kama mimi ambao nao wanapenda sana kujitambua na kufahamu mengi kuhusu Maisha na Ulimwengu kwa ujumla. Ndio lengo la maisha. Tunapaswa kutumia maisha yetu kufahamu ukweli. Sio vyema kumaliza maisha yetu bila kufahamu. Maisha yanatufundisha kila siku na hayataacha kutuma masomo.

Kwa wale ambao wanapenda kujifunza na kufahamu zaidi nawakaribisha sana, lakini kwa wale ambao hawataki kujifunza wala kufahamu mitazamo zaidi ya waliyonayo nao pia wako sawa katika ulimwengu wao. Kila mmoja ana nafasi ya kujifunza.

Nashukuru sana ndugu yangu, nawe ubarikiwe sana.
 
Apollo mimi nadhani hizi sio sheria bali ni kanuni. Sheria hupinduliwa, lakini kanuni hazipinduliwi!

Mfano kanuni ya kutafuta eneo la mraba, mstatili itaendelea kuwa vile vile miaka na miaka. Kinachoweza kubadilika na kupatikana njia mbdala tu lakini will reach at the same destination!

Napenda kanuni, SIPENDI SHERIA/LAW!

Asante sana, nadhani ni kweli kabisa. Nitarekebisha.
 
Kuna sehemu umesema kila binadamu anaishi katika dunia yake, i could suggest ingalikuwa kila binadamu anaishi katika ulimwengu wake na sio dunia yake! Dunia ni moja tu, hakuna zaidi ya hii, bali ulimwengu ni mwingi na kila binadamu anaishi katika ulimwengu wake katika reality yake katika ufahamu wake!
 
Kuna sehemu umesema kila binadamu anaishi katika dunia yake, i could suggest ingalikuwa kila binadamu anaishi katika ulimwengu wake na sio dunia yake! Dunia ni moja tu, hakuna zaidi ya hii, bali ulimwengu ni mwingi na kila binadamu anaishi katika ulimwengu wake katika reality yake katika ufahamu wake!

Asante.

Maana ya dunia sio sayari bali kumaanisha "Reallity". Hata ukisema ulimwengu bado upo sahihi. Lakini kikuu ni kufahamu kuwa kila mwanadamu anaishi katika uhalisia/ulimwengu/reality/dunia yake. Ni kama msemo wenye tafsiri na sio kwa kuchukuliwa moja kwa moja.

Nashukuru sana.
 
Naomba kila uandikapo makala/ishus fikirishi kama hizi ukumbuke kum mention mtu anaitwa UNDENIABLE ni fan mkubwa sana wa hizi fikra fikirishi!

Ubarikiwe tena!
 
Last edited by a moderator:
Asante.

Maana ya dunia sio sayari bali kumaanisha "Reallity". Hata ukisema ulimwengu bado upo sahihi. Lakini kikuu ni kufahamu kuwa kila mwanadamu anaishi katika uhalisia/ulimwengu/reality/dunia yake. Ni kama msemo wenye tafsiri na sio kwa kuchukuliwa moja kwa moja.

Nashukuru sana.

Ahsante sana, umemaliza!
 
Niliandika mimi kwa kiswahili katika kujifunza vyanzo tofauti tofauti. Sijaandika ya kingereza kwani nilipenda watumiaji wa kiswahili waielewe vyema, kwani hao ndio walengwa wangu hasa.

Ukithubutu kuandika kwa kiingereza (japo ndo inanoga zaidi), wachangiaji watapotea kama ndege ya malaysia! labda km sio wabongo, coz wabongo tunajuana!
 
Fafanua kuhusu Karma naona umeelezea tofauti na nachofahamu.

Karma ni uhalisia wa ulimwengu kuwa, kila chanzo kina matokeo yake. Ni sawa na kusema tenda mema upate mema. Ulivyo hivi sasa ni kutokana na matendo yako, mawazo yako na maneno yako yaliyopita. Karma ni kama mkia ambao unakufuata kutokana na ulivyo na utendavyo.

Karma ni kama mkusanyiko wa matendo yako, mabaya na mema, pamoja na matokeo yake mabaya na mema. Ni msemo unaoaminika hasa katika imani za Mashariki kama vile Hinduism na Buddhism. Kila mwanadamu ana Karma yake, Karma inapaswa kuwa safi kwa kutenda mema, kuwaza mema na kisema mema. Kila hali imetokana na Karma fulani, inaweza ikawa sio yako au ikawa ya mwenzio ambayo ikakuadhiri na wewe kutokana na muunganiko wa Karma zenu.

Wapo waliofika mbali na kusema kuwa, Unapokufa Karma inaondoka na wewe, kama ulitenda mema karma yako inakuwa nyepesi na sio nzito. Karma ya mabaya ni nzito kulinganisha na roho yako, karma ya mema ni nyepesi sana. Ukifa kama ulikuwa na Karma nyepesi nafsi yako inakuwa nyepesi na kuruhusu nafsi yako kurudi katika chanzo kikuu (ulipokwepo kabla ya kuzaliwa), lakini kama ulikuwa na karma mbaya, nafsi yako inazidi kushikiliwa katika ulimwengu wa chini kwa uzito wa karma na unaendelea kuzunguka katika ulimwengu wa chini, wengine huzaliwa upya katika form tofauti tofauti ya uhai bila kujitambua kuwa umerudi lakini deeply inside roho inakumbuka. Kukumbuka ulipopitia katika maisha yako ni mpaka uungane na roho yako kwani inahifadhi maisha yako yote. Wapo walioona hayo, wengine walibahatika mpaka kukumbuka walipokwepo zamani.

Huo ni mtazamo ambao sikupenda sana watu waanze kuuelewa, lakini cha msingi fahamu kuwa Karma ni matokeo ya matendo yako na mawazo yako. Hukufuata kama vile kivuli kikufuatavyo, nakaribisha na wewe uelezee uelewa wako wa Karma ili nami nifahamu zaidi.
 
Back
Top Bottom