sheria, kanuni, miongozo, taratibu za kuzingatiwa na watumia kilaji

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,971
35,113
HAVE A GOOD LAUGH!!

Ili iwe funzo kwako na wengine wenye tabia kama zako
ZIFUATAZO NI ADHABU ZITOLEWAZO KWA UVUNJAJI WA SHERIA ZA CHAMA CHA WANYWAJI POMBE:


1. Kosa la kumtoroka mlevi mwenzako kwenye Bar – Jela miezi tisa.
2. Kuacha kunywa pombe na fedha unazo – Kifungo cha maisha.
3. Kuvunja chupa ya beer – Jela miaka miwili.
4. Kumkaribisha mume au mke wa rafiki yako bila idhini yake – Viboko ishirini vya makalio na kufungiwa kunywa nusu siku.


5. Kumchukulia dhamana mtu asiyepiga maji (pombe) – Adhabu yake ni kutolewa chamani.

6. Kumwibia pombe mlevi mwenzako ni kosa kubwa – Jela mwaka mmoja.
7. Kukataa kunywa wakati umekaribishwa – Jela miaka mitano.
8. Kukwepa ulevi wa aina yoyote adhabu ni – Kunyang'anywa mume au mke, kama huna utaozwa mume au mke kwa nguvu.


9. Kupita Bar au Grocery na kujifanya huoni hilo ni kosa kubwa faini yake ni – Kuwanunulia wanywaji wote waliokuwa kwenye Grocery au Bar kila mtu kinywaji anachokunywa na kukaa ukiwaangalia mpaka wamalize.
10. Kumcheka mnywaji mwenzako akiwa amelewa ni kosa la jinai, unachotakiwa kufanya ni kumpongeza kwa kazi nzito aliyoifanya adhabu yake ni – Kutolewa kwenye Bar muda wa dakika moja.




In Life We All Have Choices,
 
hiyo ni sawa kwasababu saizi kila kitu kinakwenda kisheria.
hata wezi nao huwa wanakuwa na sheria zao wakiwa ktk wizi.
 
Back
Top Bottom