Sheria kandamizi ya magazeti;Katiba mpya haiwezi kuwa suluhu ya tatizo hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria kandamizi ya magazeti;Katiba mpya haiwezi kuwa suluhu ya tatizo hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Salary Slip, Aug 17, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,025
  Likes Received: 37,775
  Trophy Points: 280
  Miongoni mwa watu ambao wamesikitishwa na kuathirika na uamuzi wa kimabavu wa serikali wa kulifungia gazeti la mwanahalisi mimi ni mmoja wao.Mimi ni msomaji na mpenzi wa gazeti hili ambalo kwakweli limekuwa mstali wa mbele kufichua maovu ya serikali na viongozi wake.Ushahidi kuwa gazeti hili hutoa tuhuma za kweli ni pale tunaposhuhudia serikali kushindwa kulifikisha mahakani pale linapoibua tuhuma nzito kwa mfano hii iliyohusu usalama wa taifa na utekaji wa Dr.Ulimboka.Kama tuhuma hizi zilikuwa ni za uongo na uzushi kama serikali inavyodai mbona hawakulifikisha gazeti hili mahakamani?

  Tangu gazeti hili lifungiwe ni wazi tunakosa kujua mambo mengi sana na kwa kweli tunakosa haki ya kupata habari.Bila shaka kwa watawala hali hii ni afueni na furaha kwao kwani baadhi ya madhambi yao umma utakosa kuyajua.

  Bunge ndio chombo pekee ambacho tulitarajia kingeweza kuibadili kama sio kuifuta kabisa sheria hii.Bahati mbaya sana bunge letu limejaa watu wasio na uzalendo na wasiojua wajibu wao.Nasema hawajui wajibu wao kwasababu wengi wao wanadhani wajibu wao ni kuilinda na kuitetea serikali na chama chao na sio kumtetea mwananchi.Hata ikitoka hoja ya kufuta sheria hii naamini itapingwa kwa nguvu zote.Kibaya zaidi hata kiongozi wa bunge ndio kinara wa kulinda serikali.

  Sasa wadau mimi nafikri kama kubadilisha sheria hii kupitia katiba mpya ni jambo linalowezekana basi ni wakati muafaka wa kufanya hivyo.Wadau wanaohusika waelimishe umma juu ya ubovu wa sheria hii, ili kupita katiba mpya kama inawezekana, umma wa watanzania uifutilie mbali sheria hii.

  Sheria hii ni janga la kitaifa kama ulivyo ufisadi.
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,025
  Likes Received: 37,775
  Trophy Points: 280
  Mkuu una hoja ya msingi.Kinachotakiwa ni wahusika kuchukua hatua.
   
 3. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Haihitaji katiba mpya kwani hata katiba ya sasa inatoa suluhu kwa jambo hili. Ibara ya 18(1) inasema hivi:

  {Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati}

  Hakuna chombo cha habari kilichowahi kupeleka kesi mahakamani kwa mujibu wa kifungu hivi bali vinabaki vinalalama tu kama mtumwa anayeonewa.
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mpaka wasukumwe!
   
 5. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  hivi magazeti ta tanzania yanataka uhuru gani tena . kikwete amewaachia huru muandike chochote mtakacho au mnataka nini zaidi
   
Loading...