Kottler Masoko
Senior Member
- May 28, 2010
- 193
- 28
Zaidi ya wanachama 15 wa mfuko wa pensheni wa mashirika ya umma (PPF) wameandamana hadi Makao Makuu ya mfuko huo kushinikiza kulipwa fao lao la kujitoa. Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika ofisi za PPF baadhi ya wananchama hao wamesema wanashangazwa na mfuko kutowalipa fao hilo ikiwa baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii ikiendela na malipo kwa wanachama wake.
Akitolea ufafanuzi suala hilo meneja huduma kwa wateja PPF Godfrey Mollel amesema mfuko huu kwa sasa umesitisha malipo ya fao la kujitoa kwa wananchama wake tangu mei 11 mwaka huu. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya kutoa malipo ya fao la kujitoa kwa mwananchama hadi afike miaka 55 na sheria hiyo itumike mara baada ya kushughulikiwa kwa changamoto zilizopo.
TUNAOMBA WADAU TUTENGENEZE PETITION KUZUIA HUU UKANDAMIZI