Sheria kali kwa wanao wanao wapa kipondo waume zao....

Chumchang Changchum

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
4,565
2,000
WANAUME nchini hapa wamepokea kwa furaha kusainiwa kwa sheria itakayokabiliana na vitendo vya unyanyasaji hususan majumbani.
Sheria hiyo iliyosainiwa na wiki iliyopita na rais Uhuru Kenyata, inatarajiwa kuwapa ahuweni wanaume waliokuwa wakipigwa na wake zao na kushindwa kuripoti matukio hayo polisi.
Matukio ya wanaume nchini Kenya kupigwa na wake zao yamezidi kuongezeka na kuhatarisha amani katika familia.
Baadhi ya wanaume walisema wamekuwa wakipigwa na wake zao mara kwa mara na kuwafanya kutokua na amani kwenye ndoa zao.
Walisema kinga hiyo ya kisheria itakuwa ni fundisho kwa wanawake wenye kuendekeza tabia za kuwapiga kwa kudai kuwa wameshindwa kutimiza mahitaji ya ndoa na familia madai ambayo wameyakataa.
Kukithiri kwa matukio hayo kunasababisha kuanzishwa chama cha kutetea haki za wanaume na kutaka kuitishwa kwa mgomo wa wanaume kwenye ndoa mpaka sheria hiyo itakapopitishwa.
Mmoja wa waathirika wa vipigo hivyo ni Simon Kiguta, ambaye alipigwa na kujeruhiwa vibaya na mkewe ambapo tukio hilo liliamsha hasira za wanaume wengi nchini hapa.
Chanzo cha Gazeti la Uhuru...
Langu mimi enyi wanawake wa Kenya legezeni kidogo msiwapige Mabraza wetu....
Na nyinyicharge wanaume wenzetu msijilegeze gangamaleni ebo!
 

mensaah

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
984
1,000
Wanaume wa Kenya acheni kutia aibu, mwanaume anapigwa na mkwewe!, hadi rais awatungie sheria ya kuwalinda utadhan ninyi ni special group kwenye jamii mnatia AIBU
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom