Sheria juu ya ku-uziana mali.....

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
733
Hivi sheria inasemaje endapo mtu kauziwa mali mf. Nyumba, kiwanja, gari, n.k...
Lakin baada ya mauziano kukamilika ikatokea muuzaji au mtu wa karibu wa muuzaji akahitaji kuirudisha mali iliyokwisha uzwa..

Sasa hapa sheria ipoje na inasemaje? Je, Mnunuaji atakuwa na haki ya KUKATAA kurudisha mali kwa bei aliyo uziwa? Na je ana haki ya kuongeza bei ya ile mali aliyoinunua? Na kama atatakiwa kuongeza thamani haitakiwi kuzidi asilimia ngapi ya bei ya kununulia?
Hapo sheria zetu za nchi zipoje na zinasemaje hapa...

==============+
kALEnga kidamali
 
Kama waliuziana na taratibu zote za kisheria zilifuata aliyenunua ana haki zote na maamuzi yoyote nahicho kitu.
Kuuza au kukataa ni maamuzi yake hamuwezi kumpangia chochote.
 
Umenikumbusha mzee mmoja aliuza nyumba manzese 150m baadae akaona wenzake wanauza 250 hadi 300m akataka arudishe ela kwa mnunuzi lakini akashindwa.
 
mkuu unapouziwa kitu kwa uhalali tayari unapata haki ya kuweza kutumia,kukigawa au kukiuza kwa taratibu zilizowekwa kisheria.

Sasa inategemea na hicho kitu , maana kama ni ardhi ina taratibu zake, mwisho wa siku kama mtu atahitaji hicho kitu tena inabidi athibitishe makubaliano ya kwanza hayakuwa halali
 
Back
Top Bottom