Sheria iwachukulie hatua wahaini wa uperation tokomeza

mwl.lukiko

Member
May 2, 2013
26
45
wiki iliyopita tulishudia mawairi wanne (4) wa serikali wakijiuzuru nafasi zao kutokana na kile kilichoitwa ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa operation tokomeza. Ni dhati yangu kuwapongeza viongozi hawa waliochukua hatua ya uwajibikaji yaani "Ministerial Responsibilty" kama moja ya taratibu za kiutawala. lakini nina maswali mawlili hapa:

1. Je, kujiuzuru ndio mwisho wa sheria?
2. Je, vitendo hivi vilifanywa na mawaziri?

Hakuna asiyejua kuwa mawaziri ni political figures tu lakini utendaji haswa wa wizara uko chini ya katibu mkuu wa wizara husika. huyu ndiye mtu anayejua hasa A-Z za wizara, huyu ndiye mtu ambaye watendaji waliochini yake wanamtii maana ndiye mwajiri wao, huyu ndiye anayejua mitandao yote ya uovu unaofanyika chini ya wizara husika. Waziri anaweza kuondolewa kwenye wizara wakati wowote na akaja waziri mwingine; anapoingia huyu mpya anategemea sana msaada wa katibu mkuu ili kuweza kufanya kazi zake sawasawa. Ikiwa katibu mkuu na watu wake wataamua kumuingiza chake waziri wanaweza kufanya hivyo kirahisi sana.

Katibu mkuu ndiye anaeajiri watu kwenye wizara, hivyo ni rahisi sana watu kumtii katibu mkuu wakamdharau waziri. Kwa mfumo huo wa kiserikali ambao unampa katibu mkuu wa wizara mamlaka makubwa kuliko hata ya waziri hatuoni kuwa hawa ndio watu wa kuwawajibisha hata kabla hatujamfikia waziri?

Nitatoa mfano wa wizara ya maliasili na utalii. Wakati wizara hii ilipokuwa chini ya Ezekieli Maige kama waziri, katibu mkuu wake alikuwa Ladislaus Komba. Wizara hii iliboronga sana kiasi kwamba ilibidi waziri kuondolewa na katibu mkuu akabadilishwa. baada yao wakaingia Balozi Kaghasheki akiwa waziri na Mhe. Maimuna Tarishi akiwa katibu mkuu mpaka sasa. Nakumbuka kauli ya Balozi kaghasheki alipokuwa akikabidhiwa wizara ile akawaambia watendaji wake kuwa "kama mkuharibu, ntahakikisha kuwa kabla sijaondolewa mimi nawaondoa ninyi kwanza." sitaki kuamini kuwa Kaghasheki alikuwa anatania, ila najua hakujua kuwa yeye sio muajiri kwenye wizara hiyo. Hadi anaondoka kwenye wizara hiyo sijasikia kuwa Kaghasheki kamfukuza mtu kazi. Lakini pia nafikiri ni uoga wa kaghasheki kufanya maamuzi. Ndio inawezekana aliogopa vitisho vya vigogo wa nchi hii ambao wanajihusisha na kuihujumu nchi kupitia ujangili. Aliogopa kifo....maskini Kaghasheki....hakujua kuwa alipewa kisiki cha mpingo ambacho wenye shoka walishindwa, yeye akaja na fyekeo akatisha kuwafyeka....amabo sasa wamemfyeka yeye.

Lakini hoja yangu ni kutaka kuonesha kuwa tusizugwe na kujiuzuru kwa mawaziri tukawasahau wale waliofanya unyama huu. wako wapi makatibu wakuu, wako wapi makamishina waliopewa kusimamia operation hii, wamechukuliwa hatua gani? wakowapi askari waliotumwa kutekeleza unyama ule, je wamehojiwa kujua walitumwa na nani kufanya vile? tusiishie hapo tukafumbwa macho ndugu zangu kuna zaidi ya hapo.

Jambo la mwisho, nataka kusema kuwa kilichofanyika wakati wa operation tokomeza ni unyama dhidi ya ubinadamu ambao hata tunaweza kuushitaki kama "Crimes against Humanity" sheria ichukuliwe dhidi ya wahusika wote. kujizuru ni hatua ya kisiasa wala si ya kisheria ndio maana katika adhabu zinazotolewa chini ya penal code [Cap. 16 R.E. 2002] hakuna adhabu ya kujiuzuru. watu wote wafunguliwe kesi na sheria iwachukulie hatua.

Mwandishi wa page hii anapatikana kwa namba 0652 989692
 

mwl.lukiko

Member
May 2, 2013
26
45
Definetily naizungumzia Tanzania hapa kwa ajili ya haki za wanyonge walioonewa vibaya kwenye operation hii
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
sijui heading ya uzi kama iko sawa!!!!
uhaini ni kitu tofauti na unachoshitaki kwa jamii.

uhaini ni kosa la kuasi dhidi ya serikali halali, kama vipi rekebisha.
 

kababu

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,593
2,000
ndio maana ikaundwa kamati ya kimahaka kuwasaka na kuwachukulia hatua wote waliohusika.

hivyo km kuna jamaa yako mwanajeshi aliyekuwa kwenye operation mficheni mapema
 

mwl.lukiko

Member
May 2, 2013
26
45
haya kabab, ila hata kama yupo mi wamdake tu, vitendo hivi havikubaliki hata awe ndugu yake JK akamatwe tu
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,233
2,000
Kilichofanywa na kamati ya Lembeli ni uhuni. Tuhuma zilikaa kiujumla jumla sana na hivyo huwezi kuzitumia kwa kuwachukulia hatua watendaji. Hata akina Kagasheki walijiuzulu kisiasa tu.

Nakuhakikushia kuwa baada ya tume ya kimahakama kuundwa na kukamilisha kazi yake ndo mbivu na mbichi zitajulikana. Hivyo kabla ya kumnyoshea yeyote kidole mtu tusuburi uchunguzi wa kimahakama.
 

MORIA

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
559
250
Kilichofanywa na kamati ya Lembeli ni uhuni. Tuhuma zilikaa kiujumla jumla sana na hivyo huwezi kuzitumia kwa kuwachukulia hatua watendaji. Hata akina Kagasheki walijiuzulu kisiasa tu.

Nakuhakikushia kuwa baada ya tume ya kimahakama kuundwa na kukamilisha kazi yake ndo mbivu na mbichi zitajulikana. Hivyo kabla ya kumnyoshea yeyote kidole mtu tusuburi uchunguzi wa kimahakama.

Kweli uchunguzi wa kimahakama unahusika, ila ninamashaka na haki kupindishwa ukizingatia mahakimu walihusika ktk ile operation.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom