Sheria iundwe Rais alipe kodi, kwa wabunge imewezekana

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Bajeti ya Tz 2016/17 imefanikiwa kuleta mswada wa bajeti inayowawezesha waheshimiwa Wabunge kulipa kodi kwenye viinua mgongo. Ifanyike hivyo hivyo na kwa Rais, ili naye alipe kodi ya Mapato. Hata Marais wa nchi zilizoendelea wanalipa kodi ya Mapato. Kwa nini Tz , Rais halipi kodi ya Mapato?

Nawasilisha.
 
Sawasawa, ni wazo zuri! Kwa rais wetu alivyo sidhani kama atakataa kulipa kodi
 
Alipe tu...maana Hanna namna,anayepokea laki saba analipa kodi,atanunua nyanya,nguo,atapanda daladala, na kila mahitaji atajigharamia,RAIS: usafiri bure,kula bure,kulala bure,mavazi bure, na akisafiri,tena anasafiri mara kwa Mara...ana posho kubwa,na mwisho wa mwezi anakunja milioni 9 (kama ni kweli) bila kukatwa chochote,kama wa laki saba analipa na anajihudumia kila kitu,kwa nn ashindwe wa milioni tisaa?
 
Katiba ya Tanzania 1977 Ibara ya 43(2) inasema;
''Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii''.

Hii ina maana kuwa hata sheria ya Rais kulipa kodi ikipitishwa kwa sasa itabidi itumike baada ya miaka 10 ya utawala wa Rais Magufuli.

Rais akianza kulipa kodi katika kipindi chake cha utawala atakuwa anavunja katiba ambayo ameapa kuilinda na kuitetea.
 
Alipe tu...maana Hanna namna,anayepokea laki saba analipa kodi,atanunua nyanya,nguo,atapanda daladala, na kila mahitaji atajigharamia,RAIS: usafiri bure,kula bure,kulala bure,mavazi bure, na akisafiri,tena anasafiri mara kwa Mara...ana posho kubwa,na mwisho wa mwezi anakunja milioni 9 (kama ni kweli) bila kukatwa chochote,kama wa laki saba analipa na anajihudumia kila kitu,kwa nn ashindwe wa milioni tisaa?
Huu ni unyonyaji. Halafu baadae unawafukuza Chuo, watoto wa walipa kodi, kisha unamuacha Mwanao Chuoni akiwa na Div 4.30! Baba Jeisika bwana.
 
Katiba ya Tanzania 1977 Ibara ya 43(2) inasema;
''Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii''.

Hii ina maana kuwa hata sheria ya Rais kulipa kodi ikipitishwa kwa sasa itabidi itumike baada ya miaka 10 ya utawala wa Rais Magufuli.
Hayapunguzwi ila yatakatwa kodi......kukata kodi si Kupunguza,Kupunguza ni kama vile mh rais aliposema anataka kuwapunguzia mishahara watumishi wanaopata zaidi ya milioni 15,sisi hatumpunguzii...kwa maana ya kuushusha mshahara,tunauwekea kodi tu
 
Huu ni unyonyaji. Halafu baadae unawafukuza Chuo, watoto wa walipa kodi, kisha unamuacha Mwanao Chuoni akiwa na Div 4.30! Baba Jeisika bwana.
Sikujua kama na wewe ni kijana wa ufipani.Umetoa point mbovu jupita wote humu JF hv malisa hawafundishi
 
Hayapunguzwi ila yatakatwa kodi......kukata kodi si Kupunguza,Kupunguza ni kama vile mh rais aliposema anataka kuwapunguzia mishahara watumishi wanaopata zaidi ya milioni 15,sisi hatumpunguzii...kwa maana ya kuushusha mshahara,tunauwekea kodi tu
Kwa hiyo ukikata kodi kwenye mshahara wa Rais utakuwa unaongeza mshahara wa Rais?

Hivi hizi shule zinazofundisha ujinga ziko wapi ambako wengine hatuzipati?
 
kwa hiyo wewe kama umepita shule unashindwa kutofautisha kukata kodi kwenye mshahara na kupunguza mshahara. bila shaka utakuwa umesoma elimu ya India kama Nepi
 
Bajeti ya Tz 2016/17 imefanikiwa kuleta mswada wa bajeti inayowawezesha waheshimiwa Wabunge kulipa kodi kwenye viinua mgongo. Ifanyike hivyo hivyo na kwa Rais, ili naye alipe kodi ya Mapato. Hata Marais wa nchi zilizoendelea wanalipa kodi ya Mapato. Kwa nini Tz , Rais halipi kodi ya Mapato?

Nawasilisha.
Hakuna rais anaekatwa kodi kwenye mshahara wake!! Ni chief diplomatic rais yoyote wa nchi. Anakinga ya kidiplomatic
 
Obama White House analipa Kodi zote cjui kwa nni bongo haiwezekani.
 
Attachments

  • 1465622888711.jpg
    1465622888711.jpg
    25.9 KB · Views: 25
hapa unamuongelea raisi kama taasisi au mtu(individual)?.

Taasisi gani inapokea mshahara Tanzania? Anayepokea (mtu) mshahara kutokana na kodi ya wananchi wa Tanzania ndiye anapaswa kulipa PAYEE bila kujali cheo chake.

Hivi inakuwaje mtu anaomba kazi ya kuongoza wanachi kwa utashi wake bila kuombwa na wananchi wenyewe kisha akishapewa kazi hiyo anasamehewa kuchangia maendeleo ya wananchi haohao kupitia kodi?

Mbona wafanyakazi wa kawaida walioomba kazi/ajira katikati taasisi za umma kwa utashi wao wanalazimika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia PAYEE?
 
Sikujua kama na wewe ni kijana wa ufipani.Umetoa point mbovu jupita wote humu JF hv malisa hawafundishi
Ubovu wa point hiyo uko wapi? Kwani uongo, Rais halipi kodi, Rais huyo huyo anawafukuza Chuo watoto wa walipa kodi wenye vigezo. Wa kwake anayepelekwa Chuo na kurudishwa Ikulu kwa GARI la walipakodi, hajafukuzwa na ana Div 4.30 anasoma degree. Hapo Nani katoa Pumba? Kanusha hoja kwa hoja.
Acha dawa iingie.
Chama Cha Majipu (CCM) kina Kansa ya Rushwa na Ufisadi.
 
Back
Top Bottom